ZANZIBAR
SERIKALI IMESEMA
HAITARUDI NYUMA KUTEKELEZA AZMA YAKE YA KULIENDELEZA ENEO LA MICHENZANI MJINI
UNGUJA HIVYO AMELITAKA SHIRIKA LA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR-ZSSF AMBALO NDILO
LINALOTEKELEZA MRADI HUO KUHAKIKISHA KUWA LINAKABILIANA NA CHANGAMOTO ZOTE
ZINAZOTOJITOKEZA KATIKA UTEKELEZAJI WAKE.
RAIS WA
ZANZIBAR A,BAYE PIA NI MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN
AMESEMA HAYO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI NA WATENDAJI WA SHIRIKA
HILO PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI WAKATI ALIPOFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO
YA UJENZI WA MNARA WA KUMBUKUMBU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA
ZANZIBAR.
KATIKA
MAELEZO YAKE KWA MHE RAIS MKURUGENZI MKUU WA ZSSF BWANA ABDULWAKIL HAJI HAFIDH
ALIELEZA KUWA MRADI HUO WA KULIENDELEZA ENEO LA MICHENZANI UNAKABILIWA NA
TATIZO LA UMILIKI WA BAADHI YA MAENEO LIKIWEMO LA MAKONTENA HIVYO AKAIOMBA
SERIKALI KUSAIDIA KUYATATUA.
ALIUTAKA
UONGOZI WA ZSSF KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAFANYA BIASHARA WALIOPO KATIKA ENEO LA
MAKONTENA JUU YA NAMNA YA KUPISHA UJENZI KATIKA ENEO HILO NA KUELEZA KUWA
ANAAMINI KWAMBA WATAAFIKI KWANI NAO WANGEPENDA KUFANYA SHUGHULI ZAO KATIKA
MAENEO MAZURI YENYE KUVUTIA.
ALIWAELEZA
VIONGOZI WALIOKUWEPO KATIKA ENEO HILO KUWA AMEAMUA KUTEMBELEA MRADI HUO ILI
KUJIONEA MWENYEWE MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WAKE KWA KUWA AMEKUWA AKISIKIA NAMNA
UJENZI HUO UNAVYOENDELEA KUTOKA KWA WATU MBALIMBALI.
AWALI
MKURUGENZI MKUU WA ZSSF BWANA ABDULWAKIL HAJI HAFIDH ALIMUELEZA MHE RAIS KUWA
UJENZI WA MNARA HUO WENYE MITA 33 UNAENDELEA VIZURI NA UMESHAFIKIA MITA 21.
ALIELEZA
KUWA CHANGAMOTO KUBWA KATIKA KUTEKELEZA MRADI WA KULIBORESHA ENEO LA MICHENZANI
KWA KUJENGA MAJENGO YA BIASHARA NA MAKAAZI NI NAMNA YA KUWAHAMISHA KWA MUDA
WAFANYABIASHARA WA MAKONTENA PAMOJA NA UTATA WA UMILIKI WA BAADHI YA MAENEO
HAYO KUTOTAMBULIWA NA SERIKALI WAKATI WATU WANAYAMILIKI.
WAKATI
HUO HUO
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN
AMEITAKA ZSSF KUZINGATIA KWA MAKINI UENDESHAJI WA MRADI WA KIWANJA CHA
KUFURAHISHIA WATOTO ILI KUHAKIKISHA KUWA KIWANJA HICHO KINAENDESHWA KIBIASHARA
NA KIWEZE KUREJESHA FEDHA ZILIZOWEKEZWA.
AKIZUNGUMZA
MARA BAADA YA KUTEMBELEA ENEO LA KARIAKOO LINALOJENGWA KIWANJA HICHO DK SHEIN
AMELITAKA SHIRIKA HILO KUZINGATIA PIA MASUALA YA USALAMA WA WATU WATAKAOTUMIA
KIWANJA HICHO HASA MILANGO YA KUINGILIA NA KUTOKEA.
AKITOA
MAELEZO YAKE KWA MHE RAIS, MKURUGENZI MKUU WA ZSSF BWANA ABDULWAKIL HAJI HAFIDH
ALIELEZA KUWA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO UMESHAVUKA ASILIMIA 50 NA KINATARAJIWA
KUKAMILIKA NA KUANZA KUTUMIKA IFIKAPO MWEZI JULAI MWAKA HUU.
HATA HIVYO
ALIFAFANUA KUWA SUALA LA KUCHELEWA KUWASILI VIFAA VYA UJENZI NDIO LIMESABABISHA
MRADI KUTOKWENDA KWA KASI ILIYOKUSUDIWA LAKINI ALIELEZA KUWA VIFAA HIVYO
VINATARAJIWA KUWASILI NCHINI HIVI KARIBUNI.
ALIFAFANUA
KUWA KIWANJA HICHO KITAKUWA NA PEMBEA 12 PAMOJA NA HUDUMA NYINGINE KAMA MADUKA
61, SEHEMU ZA KUFANYIA MAONESHO PAMOJA NA HARUSI ,VYOO 30 PAMOJA NA SEHEMU
KUBWA YA KUEGESHA MAGARI.
RAIS WA
ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALITEMBELEA PIA SKULI YA
SEKONDARI YA LUMUMBA ILIYOPO MJINI UNGUJA AMBAKO ALIKAGUA MAZINGIRA YA SKULI
HIYO KONGWE HUMU NCHINI.
No comments:
Post a Comment