tangazo

tangazo

Thursday, March 27, 2014

UINGEREZA WAFANYA MABADILIKO YA UOMBAJI VIZA KWA WATANZANIA


DAR-ES-SALAAM.

 

Ubalozi wa Uingereza nchini umesema KUWA unakusudia kufanya mabadiliko ya utaratibu wa maombi na utoaji viza kwa Watanzania wanaotaka kwenda nchini Uingereza kwa kufungua ofisi zitakazotoa huduma hiyo Mjini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi wa masuala ya viza ya Uingereza kwa nchi za Afrika  Kashif Chaudry, amesema  AMEYASEMA HAYO MJINI Dar es Salaam ambapo ameONGEZA KUWA  wanakusudia kuanza kulipia huduma hiyo kwa njia ya simu za mkononi.


Chaudry amesema kupitia utaratibu huo mpya, maombi yote ya viza sasa yatakuwa yaKIfanyika nje ya jengo la ubalozi na kutaja eneo moja Mjini Dar es Salaam kuwa ndiKo ambako watu wanaweza kuomba na kupata viza za kuingia nchini Uingereza.


Amelitaja eneo hILO kuwa ni katika jengo la Viva Towers lililopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi Mjini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo inalenga kupunguza usumbufu kwa watu wanaoomba kibali cha kuingia Uingereza.

MAALIM SEIF ARIDHISHWA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI


ZANZIBAR.

 

MakamO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi mitatu inayoendelea KATIKA uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

 

Miradi hiyo inahusisha ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege, ujenzi wa uzio wa eneo la uwanja wa ndege, pamoja na ujenzi wa jEngo jipya la abiria (Terminal 2).

 

Akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi hiyo huko uwanja wa ndege wa Zanzibar, Maalim Seif amesema KUWA hatua iliyofikiwa inatia moyo, na kuwataka wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo  kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati.

 

Amesema KUWA Serikali kwa upande wake itaweka mkakati wa makusudi ili iweze kumaliza kuwalipa fidia wananchi ambao bado hawajalipwa, na kuruhusu ujenzi wa uzio uweze kukamilika kwa Wakati.

 

Mapema meneja wa mradi wa ujenzi wa uzio huo Bw. Frederick Nkya, alimueleza MakamO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwamba hadi sasa tayari asilimia 73 ya ujenzi huo imeshakamilika.

 

Hata hivyo amesema changamoto kubwa inayowakabili ni eneo la mita elfu tatu na mia moja ambapo sehemu kubwa ya eneo hilo bado wananchi hawajalipwa fidia.

 

Amefahamisha kuwa hadi sasa eneo la mita elfu mbili na mia saba ndilo ambalo halijafanyiwa tathmini kuweza kuwalipa wananchi walioko katika maeneo ya mradi huo.

 

Miradi ya ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka (Taxiway) pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege (Apron) katika uwanja huo inafadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo mradi wa ujenzi wa uzio wenye urefu wa mita 11,690  katika uwanja huo, unatekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pekee, ambapo zaidi ya shilingi bilioni sita zitatumika hadi kukamilika kwa mradi huo.

 

AKIZUNGUMZIA mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria meneja wa mradi huo NDUGU Ibrahim Zhang amesema KUWA ,kazi hiyo sasa inaendelea vizuri.

 

Mradi wa ujenzi wa jEngo jipya la abiria awali ulitiwa saini mwezi wa Septemba 2009 KATI ya Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano na Kampuni ya ujenzi ya Beijing Construction Engineering Group ya China, lakini baadae serikali iligundua kuwa ukubwa wa jengo uliopendekezwa mwanzo haukidhi haja.

 

HATA HIVYO KUFUATIA KASORO HIYO Serikali ilikubaliana na mkandarasi kuongezwa ukubwa wa jengo kutoka mita 15,600 hadi mita 17,800 kwa ongezeko la fedha dola za kimarekani milioni 11 nukta 8, na kufanya gharama za mradi huo kufikia dola la kimarekani milioni 82 nukta 2.

WATANZANIA WAFANYA UKAHABA CHINA


BEIJING.

Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bernard Membe amesema kuwa, mabinti wa Kitanzania wamekuwa wakifanyishwa biashara ya ukahaba huko China.

kiongozi huyo ameyasema hayo alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu wizara yake nchini China na kubainisha kwamba, watoto wa kike wenye umri wa hadi miaka 14 wamekuwa wakifanyishwa biashara ya ukahaba China kutokana na kusafirishwa na baadhi ya Watanzania wasio waaminifu.

 Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania amebainisha kwamba, mwezi uliopita alipata mwaliko nchini humo na kubaini kuwapo biashara hiyo katika mji wa Guangzhou. 

 Membe amesema kuwa, kutokana na taarifa hizo, ameitaarifu Wizara ya Mambo ya Ndani kuunda timu kwenda nchini humo na pia kubaini wanaoendesha biashara hiyo kuhakikisha inakomeshwa mara moja.

 Amesema imebainika wapo baadhi ya Watanzania wanakwenda China kwa kutumia hati bandia za kusafiria za nchi nyingine.

KESI YA VIONGOZI WA JUMIYA NA TAASISI ZA KIISLAM BADO KIZUNGUMKUTI KWA SERIKALI


ZANZIBAR.

 

Kesi inayowakabili viongozi wa jumuiya NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR  imeakhirishwa hadi julai 3 mwaka huu AMBAPO IMEWEKEWA pingamizi na Mkurugenzi wa mashtaka KUHUSU  dhamana ILIYOTOLEWA KWA WASHTAKIWA HAO.

 

Mapema muendesha mashitaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka DPP Raya Mselem aliwasilisha pingamizi ya kupinga UAMUZI WA Mahkama kuu kusikiliza ombi la dhamana ya watuhumiwa hao.

 

LICHA YA MAHAKAMA KUU KUTOA DHAMANA KWA WATUHUMIWA BADO UPANDE WA MASHTAKA UNAPINGA SUALA HILO NA UMEAMUA KUKATA RUFAA ILI WASHTAKIWA WAREJESHWE TENA RUMANDE BAADA YAKUKAA NDANI MWAKA MMOJA NA MIEZI MINNE.

 

Hata hivyo wakili wa upande wa utetezi Abdalla Juma aMEIomba mahkama hiyo kuakhirisha shauri hilo  hadi mahAkAma ya rufaa itakapokaa na kusikiliza RUFAA HIYO.

 

HATA HIVYO Jaji ISACK Sepetu hakupingana na hoja hiyo.

 

Watuhumiwa WALIOFIKA MAHAKAMANI LEO ni PAMOJA NA AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH  Farid Hadi Ahmed,AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR FADHILATU SHEIKH Mselem  BIN AlY, NAIBU AMIRI WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR ZANZIBAR AL-USTADH Azan Khalid Hamdan.

 

WENGINE  NI KATIBU WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR AL-USTADH Abdalla Saidi, MAUSTADH MusSa Juma Mussa, SUleiman Juma Sleiman, Khamis Ali Sleiman, hasSan Bakari Sleiman, Gharibu Ahmada Juma, na Majaliwa Fikirini Majaliwa.

 

Mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu mali,  Uchochezi,Ushawishi , kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa

Kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne AL-USTADH Azan Khalid ambae anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo VINAWEZA v kusababisha uvunjifu wa amani.

 

Vitendo hivyo vinadaiwa   kufanyika kati ya Oktoba 17,18 na 19 mwaka ,2012 katika maeneo tofauti katika manispaa yaa mji wa Zanziba ambapo washitakiwa hao wote waMEkana makosa yote hayo.

 

viongozi hao walipewa dhamana na mahakama kuu ya zanzibar tarehe 27 mwezi wa pili mwaka huu baada yakutekeleza masharti yaliyowekwa.

Monday, March 17, 2014

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA ELIMU ZILIZOPO NCHINI


ZANZIBAR.

VIJANA NCHINI WAMESHAURIWA KUTUMIA FURSA ZA KUJIPATIA TAALUMA KATIKA NYANJA MBALI MBALI KUTOKA KATIKA VYUO NA TAASISI ZA ELIMU HAPA NCHINI ILI VIWAJENGEE UWEZO WA KUJITEGEMEA WENYEWE KIMAISHA.

 

USHAURI HUO UMETOLEWA  NA  WALIMU WA VYUO NA TAASISI MBALI MBALI HAPA ZANZIBAR KATIKA KONGAMANO LA VIJANA WENYE TATIZO LA AJIRA NCHINI HUKO KATIKA UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZAMANI, KIKWAJUNI MJINI HAPA WAKATI WAKIWASILISHA MAELEZO KUHUSIANA NA KUJIUNGA, TAALUMA WANAZOZITOA, MAHITAJI YA SOKO YA FANI HUSIKA NDANI NA NJE YA NCHI, ADA INAYOHITAJIKA  ILI KUWAJENGEA UWELEWA NA KUCHUKUA HATUA ZA MAAMUZI SAHIHI YA KUJIKWAMUA KIMAISHA.

 

WALIMU HAO KUTOKA  TAASISI YA SAYANSI NA TECHNOLOGIA KARUME, CHUO CHA SAYANSI YA AFYA MBWENI,KITUO CHA UFUNDI MKOKOTONI, CHUO CHA MAENDELEO YA UTALI ZANZIBAR,KUMBU KUMBU YA MWALIMU NYERERE, UONGOZI WA FEDHA CHWAKA,ZANZIBAR SCHOOL OF HEALTH (SHAA) MOMBASA PAMOJA NA TAASISI YA BUISSNESS & TECHNOLOGY MWANAKWEREKWE WAMESEMA KUWA NI LAZIMA VIJANA KULIWEKA SUALA LA ELIMU MBELE ILI WAPATE TAALUMA HUSIKA KWA MAENDELEO YAO NA TAIFA KWA JUMLA.

 

VIONGOZI HAO WAMEWAOMBA VIJANA KUJIUNGA NA VYUO NA TAASISI HIZO KWA GHARAMA NAFUU ILI KUJINUFAISHA HIVI SASA NA HAPO BAADAE.

 

NAO VIJANA HAO KUTOKA SEHEMU MBALI MBALI NCHINI WAMEISHUKURU JUMUIYA YA MAENDELEO  YA VIJANA WA MIKUNGUNI (MYDO) KWA KURATIBU KUWEPO KWA KONGAMANO HILO AMBALO LIMEWAPA FURSA NZURI  YA KUPATA UWELEWA NA KWAMBA SUALA LA ELIMU KWA AJIRA WATALIFANYIA KAZI IPASAVYO KUILINGANA NA HALI ZAO ZA KIFEDHA.

RIPOTI YA KILIMANJARO YATOLEWA


ZANZIBAR

BODI YA KUCHUNGUZA AJALI YA MELI YA MV. KILIMANJARO 2 LEO IMEKABIDHI RASMI RIPOTI YA AJALI HIYO BAADA YA KUMALIZA KAZI HIYO KWA WAZIRI WA  MIUNDO MBINU NA MAWASILIANO RASHID SEIF SULEIMAN OFISINI KWAKE KISAUNI NJE KIDOGO YA MJI WA ZANZIBAR.

AKIKABIDHI RIPOTI HIYO MWENYEKITI WA BODI HIYO KHAMIS RAMADHAN ABDALLAH AMESEMA KAZI HIYO WALIYOPEWA WAMEWEZA KUIMALIZA KWA MUJIBU WA SIKU WALIZOPEWA NA WALIKUWA HURU BILA YA KUINGILIWA NA MKONO WA SERIKALI WALA TAASISI YOYOTE.

AIDHA ALISEMA BODI ILIFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU LAKINI WALICHUKULIA KAZI HIYO NIYANYUMBANI NA NIWAJIBU WAO KUFANYA KWA MASLAHI YA WANANCHI WA ZANZIBAR.

HATA HIVYO ALISEMA HAPO AWALI KAZI HIYO WALIPANGIWA KUIFANYA KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA LAKINI KUTOKANA NA UZITO WA KAZI HIYO NA MAJUKUMU MENGINE WALILAZIMIKA KUOMBA MWEZI MMOJA AMBAPO KAZI HIYO WALITAKIWA KUIKABIDHI KESHO NA BADALA YAKE WAMEWEZA KUIKABIDHI LEO.

KWA UPANDE WAKE WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO RASHID SEIF SULEIMAN AMEIPONGEZA BODI HIYO KWA KUFANYA KAZI BILA YA UPENDELEO NA ZAIDI WALIZINGATIA UHALISIA WA KAZI YAO NA SIYO KUBABAISHWA NA MTU.

AIDHA ALISEMA CHOMBO HICHO HAKIKUUNDWA KWA KUTAFUTWA NANI MBAYA WALA MKOSA WA AJALI HIYO BALI KIMEUNDWA KWA AJILI YA KUANGALIA MAPUNGUFU YALIYOPO NA KUWEZA KUREKEBISHWA ILI WAZANZIBARI WASIZIDI KUUMIA.

HATA HIVYO ALISEMA DALILI NZURI IPO KATIKA RIPOTI HIYO NA KAZI ILIYOBAKI NI KUISOMA KWA KINA NA KISHA KUKABIDHI KATIKA MIKONO YA SERIKALI KUU KWA MUJIBU WA TARATIBU ZILIZOPO.

AIDHA ALIISHUKURU SANA BODI HIYO KWA VILE ILIKUWA HURU NA KUWEZA KUFANYA KAZI KWA KINA BILA KIZUIZI CHA MTU WALA SERIKALI.

BODI HIYO YA WAJUMBE WATANO AMBAYO ILIYOUNDWA CHINI YA SHERIA YA USAFIRI WA BAHARINI KIFUNGU NO. 4552 NA 4551 YA MWAKA 2006 IMEUNDWA KUFUATIA AJALI YA MELI YA MV. KILIMANJARO 2 ILIYOTOKEA MIEZI MIWILI ILIYOPITA KATIKA MKONDO WA NUNGWI ILIPOKUWA IKITOKEA PEMBA KUJA UNGUJA.

Monday, March 10, 2014

mdhibiti na mgaguzi mkuu wa serikali akutana na chama cha cuf


MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU TANZANIA BW. LUDOVICK UTOUH, AMEKUTANA NA UONGOZI WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) KUJADILIANA JUU YA MASUALA YA FEDHA YA CHAMA HICHO KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU, KUANZIA MWAKA 2010 HADI MWAKA 2012.

AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO KILICHOFANYIKA OFISI KUU ZA CUF BUGURUNI, BW. LUDOVICK AMESEMA NI JAMBO LA FARAJA KUONA CHAMA HICHO KIMEONESHA NJIA KWA VYAMA VYENGINE, KIKIWA CHA MWANZO KUKAGULIWA NA CHOMBO HICHO.

BW. LUDOVICK AMBAYE ALIONGOZA UJUMBE WA OFISI YA MDHIBITI NA MKUGUZI MKUU WA HESABU, AMEELEZEA KURIDHISHWA NA MUENDELEZO WA MASUALA YA FEDHA NDANI YA CHAMA HICHO, NA KUAHIDI KUTOA RIPOTI KAMILI KATIKA KIPINDI CHA SIKU 21.

KIKAO HICHO PIA KILIMUHUSISHA KATIBU MKUU WA CUF AMBAYE PIA NI MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.

WAKATI HUO HUO MAALIM SEIF AMEFANYA MAHOJIANO NA KAMPUNI YA GLOBAL PUBLISHERS LIMITED YA DAR ES SALAAM, INAYOCHAPISHA MAGAZETI YA UWAZI, CHAMPION, RISASI, IJUMAA NA AMANI.

PAMOJA NA MAMBO MENGINE KAMPUNI HIYO ILITAKA KUJUA JUU MAENDELEO YA CHAMA HICHO, PAMOJA NA MAFANIKIO, CHANGAMOTO NA UTENDAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA.

KUHUSU MAENDELEO YA CHAMA HICHO MAALIM SEIF AMESEMA CHAMA HICHO HAKIJAFIFIA KAMA INAVYODAIWA NA BAADHI YA WATU, NA BADALA YAKE KIMEZIDI KUIMARIKA KATIKA MIKOA MBALI MBALI YA TANZANIA.

AMESEMA LENGO KUU LA CHAMA CHA SIASA NI KUSHIKA HATAMU ZA DOLA, NA KWAMBA TAYARI CHAMA HICHO KIMEKUWA SEHEMU YA SERIKALI KATIKA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR.

AKIPOULIZWA KUHUSU MADAI YA KUKIDHOOFISHA CHAMA HICHO KUTOKANA NA KUSHIKILIA WADHIFA WA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR AKIWA PIA NI KATIBU MKUU WA CUF, MAALIM SEIF ALISEMA KAZI KUBWA YA KATIBU MKUU NI KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA CHAMA AMBAYO HUFANYWA NA WASADIZI WAKE WAKIWEZO NAIBU MAKATIBU WAKUU PAMOJA NA WAGURUGENZI.

HIVYO AMESEMA NAFASI HIYO HAIATHIRI UFANISI WA CHAMA HICHO, NA KAMWE HAIWEZI KUWA SABABU YA KUZOROTESHA MAENDELEO YA CHAMA, NA KUTOA MIFANO KWA RAIS JAKAYA KIKWETE AMBAYE NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA DKT. ALI MOHD SHEIN AMBAYE NI MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR.

MAALIM SEIF PIA ALIZUNGUMZIA JUU YA SUALA LA DAWA ZA KULEVYA AMBAPO ALISEMA OFISI YAKE IKIWA IMEPEWA JUKUMU HILO, IMEKUWA IKIPANGA MIKAKATI YA KILA AINA KUONA KUWA TATIZO HILO LINADHIBITIWA.

HATA HIVYO AMEKIRI KUWEPO UGUMU WA KUKABILIANA NA TATIZO HILO KUTOKANA NA JIOGRAFIA YA ZANZIBAR AMBAYO IMEKUWA NA NJIA NYINGI ZISIZO RASMI, ZINAZOFIKIRIWA KUINGIZWA DAWA HIZO UKITOA VIWANJA VYA NDEGE NA BANDARI ZINAZOTAMBULIKA.

AMESISITIZA HAJA KWA WATENDAJI WA MAMLAKA ZA VIWANJA VYA NDEGE NA BANDARI KUWA WAADILIFU, NA KUEPUKANA NA VISHAWISHI VINAVYOWEZA KUPELEKEA UINGIZAJI WA DAWA ZA KULEVYA KATIKA MAENEO HAYO.

AIDHA AMESEMA KWA SASA WAMEKUWA WAKIWEKA UDHIBITI KATIKA MAENEO HAYO YALIYO RASMI, PAMOJA NA KUSAMBAZA ELIMU KWA VIJANA WAKIWEMO WANAFUNZI, JUU YA ATHARI YA DAWA HIZO.

AMEHIMIZA MASHIRIKIANO BAINA YA VYOMBO VYA DOLA NA WANANCHI KATIKA KUKABILIANA NA TATIZO HILO AMBALO LIMEKUWA LIKIWAATHIRI ZAIDI VIJANA AMBAO NDIO NGUVU KAZI YA TAIFA.

“TATIZO HILI HALITOMUATHIRI MTOTO WA FULANI TU BALI TUJUE KUWA VIJANA WENGI HATA WATOTO WA VIONGOZI NA MATAJIRI WANAATHIRIKA, KWA HIVYO KITU CHA MSINGI NI MASHIRIKIANO BAINA YA VYOMBO VYETU VYA DOLA NA WANANCHI”, ALISISITIZA MAALIM SEIF.

Tuesday, March 4, 2014

UZINDUZI WA MIAKA HAMSINI YA MUUNGANO


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK ALI MOHAMED SHEIN AMEWATAKA WATANZANIA KUTAMBUA KUWA KUUNDWA KWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NI MATOKEO YA MAKUBALIANO YA WANANCHI WENYEWE CHINI YA VIONGOZI WAASISI WA MUUNGANO HUO MAREHEMU MWALIMU JULIUS NYERERE, RAIS WA JAMHURI YA TANGANYIKA NA MAREHEMU MZEE ABEID AMANI KARUME RAIS WA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.

KWA HIYO AMESEMA WANANCHI WANA KILA SABABU YA KUUTETEA, KUULINDA NA KUUNDELEZA NA PIA NI WAJIBU WAO KUJIVUNIA MUUNGANO HUO KWA MANUFAA YA WATU WOTE.

AKIZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO HUKO KWENYE UKUMBI WA SALAMA KATIKA HOTELI YA BWAWANI MJINI UNGUJA LEO, DK. SHEIN AMESEMA MIAKA 50 YA MUUNGANO IMESHUHUDIA MAENDELEO MAKUBWA AMBAYO YAMEMGUSA KILA MWANANCHI.

AMEBAINISHA KUWA KUDUMU KWA MUUNGANO HUO KUNATOKANA NA DHAMIRA ZA DHATI ZA UMOJA WALIOKUWANAO WAASISI WAKE, SERA NZURI ZA VYAMA VYA TANU, AFRO SHIRAZI NA CCM PAMOJA NA JUHUDI ZINAZOENDELEZWA NA VIONGOZI WALIOFUATIA PAMOJA NA KUUNGWA MKONO NA WANANCHI.

ALIONGEZA KUWA MBALI ZA BUSARA ZA WAASISI WA MUUNGANO LAKINI KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA ZA UPANDE WA KIJIOLOJIA NA KIJAMII ZINAONESHA KUWA WATU WA ZANZIBAR NA TANGANYIKA NI WATU WAMOJA HIVYO MUUNGANO WAO SI TUKIO LILILOKUJA BILA SABABU MAALUM.

DK SHEIN ALIWAKUMBUSHA WANANCHI UHUSIANO USIOTENGANIKA KATI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MWAKA 1964 NA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ULIASISIWA TAREHE 26 APRILI MWAKA 1964 NA KUSISITIZA KUWA HIZO NDIZO NGUZO KUU KWA MUSTAKABALA WA NCHI.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALIWAELEZA WANANCHI WALIOHUDHURIA HAFLA HIYO KUWA MIAKA 50 YA MUUNGANO IMETOA FURSA KWA WANANCHI WA PANDE ZOTE MBILI KUISHI WAPENDAPO KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BILA YA KUBUGHUDHIWA KWA KUWA UHURU HUO UPO NDANI YA KATIBA ZOTE MBILI.

KWA HIYO AMEWATAKA WATANZANIA KUZINGATIA KAULI MBIU YA MAADHIMISHO HAYO AMBAYO NI UTANZANIA WETU NI MUUNGANO WETU,TUULINDE, TUUIMARISHE NA TUUDUMISHE KAULI AMBAYO ALISEMA INATHIBITISHA UMUHIMU WA UTANZANIA WETU.

ALIKIRI KUWA MUUNGANO UMEKUWA NA CHANGAMOTO ZAKE LAKINI ALIELEZA PIA JITIHADA MBALI MBALI AMBAZO ZIMEKUWA ZIKICHUKULIWA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO KWA LENGO LA KUIMARISHA MUUNGANO.

KABLA YA HOTUBA YAKE, DK. SHEIN ALIZINDUA NEMBO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 KWA KUPONYEZA KITUFE.

AWALI AKIMKARIBISHA RAIS, MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI ALIELEZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO YATAAMBATANA NA SHUGHULI MBALI MBALI ZITAKAZOWASHIRIKISHA WANANCHI KWA NJIA YA MAKANGOMANO, MICHEZO NA BURUDANI NA KUFIKIA KILELE CHAKE TAREHE 26 APRILI,2014 HUKO KATIKA KIWANJA CHA UHURU DAR ES SALAAM.

ALIELEZA PIA KUWA KATIKA MIAKA 50 MALENGO YA MUUNGANO YAMEKUWA YAKITEKELEZWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA NA KUELEZA KUWA WATANZANIA HAWANA BUDI KUWASHUKURU WAASISI WA MUUNGANO PAMOJA NA VIONGOZI WALIOFUATIA KWA KUTELEKEZA KWA DHATI AZMA YA MUUNGANO YA KUWALETEA MAENDELEO.

SHEREHE HIZO ZA UZINDUZI ZILIHUDHURIWA PIA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS MAALIM SEIF SHARIF HAMAD PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE WAKIWEMO MAWAZIRI WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO NA SERIKALI WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR.

RAIS SHEIN NA WAMAREKANI


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR WANAJIVUNIA UHUSIANO MZURI ULIOPO KATI YAO NA SERIKALI NA WANANCHI WA MAREKANI.

AKIZUNGUMZA NA UJUMBE KUTOKA JIJI LAVELLEJO KATIKA JIMBO LA CALIFONIA NCHINI MAREKANI ULIOONGOZWA NA MEYA WA JIJI HILO MSTAHIKI OSBY DAVIS, IKULU DK. SHEIN ALIELEZA PIA KUWA ZANZIBAR INARIDHISHWA NA UHUSIANO HUO AMBAO UMEJENGWA NA HISTORIA INAYOWAUNGANISHA WATU WA ZANZIBAR NA WA MAREKANI KWA KARNE NYINGI.

ALIBAINISHA KUWA UHUSIANO KATI YA ZANZIBAR NA MAREKANI ULIANZA KATIKA KARNE YA 19 KATIKA NGAZI YA UKONSELI NA HADI NCHI MBILI HIZO ZIMEJENGA HISTORIA YA URAFIKI WA KWELI KATI YA SERIKALI ZETU NA WATU WAKE NA NDIO MAANA HADI LEO UHUSIANO HUO UMEKUWA MZURI HUKU PANDE ZOTE ZIKIWA NA ARI YA KUUIMARISHA.

ALIIELEZEA ZIARA YA UJUMBE HUO KUTOKA JIJI LA VALLEJO KUWA SIO TU NI MUHIMU KATIKA KUWAUNGANISHA WANANCHI WA MAREKANI NA WENZAO WA ZANZIBAR BALI NI UTHIBITISHO WA URAFIKI ULIOPO KATI YA ZANZIBAR NA MAREKANI.

ALIONGEZA KUWA WATU WA NCHI HIZO WAMEKUWA WAKITEMBELEANA NA KUSAIDIANA KWA MIONGO MINGI NA VIJANA WENGI WA ZANZIBAR WAMEKARIBISHWA NCHINI MAREKANI NA WENGINE WAMEPATA FURSA ZA MASOMO NA KUISHI HUKO BILA VIKWAZO.

KWA HIYO ALISDEMA NDIO MAANA ZANZIBAR INGEPENDA KUONA KILA SIKU UHUSIANO WAKE NA MAREKENI UNAIMARIKA.

ALIBAINISHA KUWA KUTOKANA NA UHUSIANO MZURI HUO ZANZIBAR AMBAYO NI SEHEMU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMEKUWA IKIPOKEA MISAADA MBALIMBALI AMBAYO IMEKUWA CHACHU KATIKA KUIMARISHA MAENDELEO HUMU NCHINI.

MIONGONI MWA MISAADA HIYO ALIUELEZA UJUMBE HUO NI UJENZI WA BARABARA HUKO MKOA WA KASKAZINI PEMBA AMBAZO ZIMEJENGWA KWA MSAADA WA WATU WA MAREKANI KUPITIA MFUKO WA CHANGAMOTO ZA MILENIA NA ZINATARAJIWA KUZINDULIWA HIVI KARIBUNI

ALIONGEZA KUWA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR WAMEFURAHISHWA NA UAMUZI WA SERIKALI NA WATU WA MAREKANI KWA KUWAJUMUISHA TENA KATIKA AWAMU YA PILI NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MFUKO WA CHANGAMOTO ZA MILENIA UAMUZI AMBAO UNAONESHA KUWA MAREKANI NA ZANZIBAR NI MARAFIKI WA KWELI.

KWA HIYO DK. SHEIN ALIUTHIBITISHIA UJUMBE HUO DHAMIRA YA KWELI YA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR YA KUENDELEZA NA KUUENZI UHUSIANO WAKE NA MAREKANI.

DK. SHEIN ALISISITIZA KUWA ZANZIBAR NA MAREKANI WANA MALENGO YANAYOFANANA NA DHAMIRA MOJA HIVYO KUIMARISHA UHUSIANO KATI YAO NDIO NIA NA NI WAJIBU WA KILA UPANDE.

ALIUTAKA UJUMBE HUO AMBAO UTAFANYA MAZUNGUMZO NA WADAU MBALIMBALI KATIKA SEKTA BINAFSI HUSUSAN SEKTA YA UTALII KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR KATIKA KUENDELEZA UTALII KATI YA ZANZIBAR NA JIMBO LA CALIFONIA NA MAREKANI KWA UJUMLA.

KWA HIYO ALIMUELEZA MSTAHIKI MEYA HUYO KUWA ZIARA HIYO IMEFUNGUA UKURASA MPYA KATIKA KUENDELEZA NA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATI YA WATU WA ZANZIBAR NA WATU WA JIMBO LA CALIFONIA NA MREKANI KWA UJUMLA.

KWA UPANDE WAKE MSTAHIKI MEYA WA VALLEJO BWANA OSBY DAVIS ALISEMA KUFIKA KWAO ZANZIBAR WANAJIONA WAMEFIKA NYUMBANI NA KUMSHUKURU MHESHIMIWA RAIS KWA KUMPA FURSA YEYE NA UJUMBE WAKE KUONANA NAYE.

ALIELEZA KUWA KUWA NI FAHARI NA HESHIMA KUBWA KWAOU KUPATA FURSA YA KUONANA NA MHE RAIS WA ZANZIBAR, NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE KIKWETE NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WAKE.

AMESEMA KUWA ZIARA YAKE HIYO NDIO NI MWANZO WA ZIARA NYINGI KAMA HIZO KUTEMBELEA ZANZIBAR NA TANZANIA KWA JUMLA.

ALIBAINISHA KUWA WANANCHI WA MAREKANI WENYE ASILI YA AFRIKA WANAJIVUNIA KUTAMBUA ASILI YAO NA NDIO MAANA WAMEANZISHA JUHUDI ZA KUIMARISHA UHUSIANO NA ASILI YAO.

MSTAHIKI MEYA DAVIS ALIFAFANUA KUWA KUSEMA HIVYO SIO KWAMBA WAO SI WA MAREKANI LAKINI NI UKWELI KUWA WATU WA MAREKANI WANA ASILI ZAO WENGINE WANATOKA JAPAN, WENGINE UJERUMANI, WENGINE WA CHINA NA KADHALIKA HIVYO WAO AFRIKA NDIO KWAO NA WANAJIVUNIA KUJITAMBUA HIVYO NA KUSISITIZA KUWA HUO NI UKWELI WA KIHISTORIA .