BEIJING.
Waziri wa Mambo ya nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bernard Membe amesema
kuwa, mabinti wa Kitanzania wamekuwa wakifanyishwa biashara ya ukahaba huko
China.
kiongozi huyo ameyasema hayo
alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu wizara yake nchini China
na kubainisha kwamba, watoto wa kike wenye umri wa hadi miaka 14 wamekuwa
wakifanyishwa biashara ya ukahaba China kutokana na kusafirishwa na baadhi ya
Watanzania wasio waaminifu.
Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania
amebainisha kwamba, mwezi uliopita alipata mwaliko nchini humo na kubaini
kuwapo biashara hiyo katika mji wa Guangzhou.
Membe amesema kuwa, kutokana
na taarifa hizo, ameitaarifu Wizara ya Mambo ya Ndani kuunda timu kwenda nchini
humo na pia kubaini wanaoendesha biashara hiyo kuhakikisha inakomeshwa mara
moja.
Amesema imebainika wapo
baadhi ya Watanzania wanakwenda China kwa kutumia hati bandia za kusafiria za
nchi nyingine.
No comments:
Post a Comment