tangazo

tangazo

Tuesday, March 4, 2014

RAIS SHEIN NA WAMAREKANI


RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR WANAJIVUNIA UHUSIANO MZURI ULIOPO KATI YAO NA SERIKALI NA WANANCHI WA MAREKANI.

AKIZUNGUMZA NA UJUMBE KUTOKA JIJI LAVELLEJO KATIKA JIMBO LA CALIFONIA NCHINI MAREKANI ULIOONGOZWA NA MEYA WA JIJI HILO MSTAHIKI OSBY DAVIS, IKULU DK. SHEIN ALIELEZA PIA KUWA ZANZIBAR INARIDHISHWA NA UHUSIANO HUO AMBAO UMEJENGWA NA HISTORIA INAYOWAUNGANISHA WATU WA ZANZIBAR NA WA MAREKANI KWA KARNE NYINGI.

ALIBAINISHA KUWA UHUSIANO KATI YA ZANZIBAR NA MAREKANI ULIANZA KATIKA KARNE YA 19 KATIKA NGAZI YA UKONSELI NA HADI NCHI MBILI HIZO ZIMEJENGA HISTORIA YA URAFIKI WA KWELI KATI YA SERIKALI ZETU NA WATU WAKE NA NDIO MAANA HADI LEO UHUSIANO HUO UMEKUWA MZURI HUKU PANDE ZOTE ZIKIWA NA ARI YA KUUIMARISHA.

ALIIELEZEA ZIARA YA UJUMBE HUO KUTOKA JIJI LA VALLEJO KUWA SIO TU NI MUHIMU KATIKA KUWAUNGANISHA WANANCHI WA MAREKANI NA WENZAO WA ZANZIBAR BALI NI UTHIBITISHO WA URAFIKI ULIOPO KATI YA ZANZIBAR NA MAREKANI.

ALIONGEZA KUWA WATU WA NCHI HIZO WAMEKUWA WAKITEMBELEANA NA KUSAIDIANA KWA MIONGO MINGI NA VIJANA WENGI WA ZANZIBAR WAMEKARIBISHWA NCHINI MAREKANI NA WENGINE WAMEPATA FURSA ZA MASOMO NA KUISHI HUKO BILA VIKWAZO.

KWA HIYO ALISDEMA NDIO MAANA ZANZIBAR INGEPENDA KUONA KILA SIKU UHUSIANO WAKE NA MAREKENI UNAIMARIKA.

ALIBAINISHA KUWA KUTOKANA NA UHUSIANO MZURI HUO ZANZIBAR AMBAYO NI SEHEMU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMEKUWA IKIPOKEA MISAADA MBALIMBALI AMBAYO IMEKUWA CHACHU KATIKA KUIMARISHA MAENDELEO HUMU NCHINI.

MIONGONI MWA MISAADA HIYO ALIUELEZA UJUMBE HUO NI UJENZI WA BARABARA HUKO MKOA WA KASKAZINI PEMBA AMBAZO ZIMEJENGWA KWA MSAADA WA WATU WA MAREKANI KUPITIA MFUKO WA CHANGAMOTO ZA MILENIA NA ZINATARAJIWA KUZINDULIWA HIVI KARIBUNI

ALIONGEZA KUWA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR WAMEFURAHISHWA NA UAMUZI WA SERIKALI NA WATU WA MAREKANI KWA KUWAJUMUISHA TENA KATIKA AWAMU YA PILI NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MFUKO WA CHANGAMOTO ZA MILENIA UAMUZI AMBAO UNAONESHA KUWA MAREKANI NA ZANZIBAR NI MARAFIKI WA KWELI.

KWA HIYO DK. SHEIN ALIUTHIBITISHIA UJUMBE HUO DHAMIRA YA KWELI YA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR YA KUENDELEZA NA KUUENZI UHUSIANO WAKE NA MAREKANI.

DK. SHEIN ALISISITIZA KUWA ZANZIBAR NA MAREKANI WANA MALENGO YANAYOFANANA NA DHAMIRA MOJA HIVYO KUIMARISHA UHUSIANO KATI YAO NDIO NIA NA NI WAJIBU WA KILA UPANDE.

ALIUTAKA UJUMBE HUO AMBAO UTAFANYA MAZUNGUMZO NA WADAU MBALIMBALI KATIKA SEKTA BINAFSI HUSUSAN SEKTA YA UTALII KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR KATIKA KUENDELEZA UTALII KATI YA ZANZIBAR NA JIMBO LA CALIFONIA NA MAREKANI KWA UJUMLA.

KWA HIYO ALIMUELEZA MSTAHIKI MEYA HUYO KUWA ZIARA HIYO IMEFUNGUA UKURASA MPYA KATIKA KUENDELEZA NA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATI YA WATU WA ZANZIBAR NA WATU WA JIMBO LA CALIFONIA NA MREKANI KWA UJUMLA.

KWA UPANDE WAKE MSTAHIKI MEYA WA VALLEJO BWANA OSBY DAVIS ALISEMA KUFIKA KWAO ZANZIBAR WANAJIONA WAMEFIKA NYUMBANI NA KUMSHUKURU MHESHIMIWA RAIS KWA KUMPA FURSA YEYE NA UJUMBE WAKE KUONANA NAYE.

ALIELEZA KUWA KUWA NI FAHARI NA HESHIMA KUBWA KWAOU KUPATA FURSA YA KUONANA NA MHE RAIS WA ZANZIBAR, NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE KIKWETE NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WAKE.

AMESEMA KUWA ZIARA YAKE HIYO NDIO NI MWANZO WA ZIARA NYINGI KAMA HIZO KUTEMBELEA ZANZIBAR NA TANZANIA KWA JUMLA.

ALIBAINISHA KUWA WANANCHI WA MAREKANI WENYE ASILI YA AFRIKA WANAJIVUNIA KUTAMBUA ASILI YAO NA NDIO MAANA WAMEANZISHA JUHUDI ZA KUIMARISHA UHUSIANO NA ASILI YAO.

MSTAHIKI MEYA DAVIS ALIFAFANUA KUWA KUSEMA HIVYO SIO KWAMBA WAO SI WA MAREKANI LAKINI NI UKWELI KUWA WATU WA MAREKANI WANA ASILI ZAO WENGINE WANATOKA JAPAN, WENGINE UJERUMANI, WENGINE WA CHINA NA KADHALIKA HIVYO WAO AFRIKA NDIO KWAO NA WANAJIVUNIA KUJITAMBUA HIVYO NA KUSISITIZA KUWA HUO NI UKWELI WA KIHISTORIA .

No comments:

Post a Comment