ZANZIBAR
BODI YA KUCHUNGUZA AJALI YA MELI YA MV. KILIMANJARO 2 LEO
IMEKABIDHI RASMI RIPOTI YA AJALI HIYO BAADA YA KUMALIZA KAZI HIYO KWA WAZIRI WA
MIUNDO MBINU NA MAWASILIANO RASHID SEIF SULEIMAN OFISINI KWAKE KISAUNI
NJE KIDOGO YA MJI WA ZANZIBAR.
AKIKABIDHI RIPOTI HIYO MWENYEKITI WA BODI HIYO KHAMIS
RAMADHAN ABDALLAH AMESEMA KAZI HIYO WALIYOPEWA WAMEWEZA KUIMALIZA KWA MUJIBU WA
SIKU WALIZOPEWA NA WALIKUWA HURU BILA YA KUINGILIWA NA MKONO WA SERIKALI WALA
TAASISI YOYOTE.
AIDHA ALISEMA BODI ILIFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
LAKINI WALICHUKULIA KAZI HIYO NIYANYUMBANI NA NIWAJIBU WAO KUFANYA KWA MASLAHI
YA WANANCHI WA ZANZIBAR.
HATA HIVYO ALISEMA HAPO AWALI KAZI HIYO WALIPANGIWA
KUIFANYA KWA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA LAKINI KUTOKANA NA UZITO WA KAZI HIYO NA
MAJUKUMU MENGINE WALILAZIMIKA KUOMBA MWEZI MMOJA AMBAPO KAZI HIYO WALITAKIWA
KUIKABIDHI KESHO NA BADALA YAKE WAMEWEZA KUIKABIDHI LEO.
KWA UPANDE WAKE WAZIRI WA MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO
RASHID SEIF SULEIMAN AMEIPONGEZA BODI HIYO KWA KUFANYA KAZI BILA YA UPENDELEO
NA ZAIDI WALIZINGATIA UHALISIA WA KAZI YAO NA SIYO KUBABAISHWA NA MTU.
AIDHA ALISEMA CHOMBO HICHO HAKIKUUNDWA KWA KUTAFUTWA NANI
MBAYA WALA MKOSA WA AJALI HIYO BALI KIMEUNDWA KWA AJILI YA KUANGALIA MAPUNGUFU
YALIYOPO NA KUWEZA KUREKEBISHWA ILI WAZANZIBARI WASIZIDI KUUMIA.
HATA HIVYO ALISEMA DALILI NZURI IPO KATIKA RIPOTI HIYO NA
KAZI ILIYOBAKI NI KUISOMA KWA KINA NA KISHA KUKABIDHI KATIKA MIKONO YA SERIKALI
KUU KWA MUJIBU WA TARATIBU ZILIZOPO.
AIDHA ALIISHUKURU SANA BODI HIYO KWA VILE ILIKUWA HURU NA
KUWEZA KUFANYA KAZI KWA KINA BILA KIZUIZI CHA MTU WALA SERIKALI.
BODI HIYO YA WAJUMBE WATANO AMBAYO ILIYOUNDWA CHINI YA
SHERIA YA USAFIRI WA BAHARINI KIFUNGU NO. 4552 NA 4551 YA MWAKA 2006 IMEUNDWA
KUFUATIA AJALI YA MELI YA MV. KILIMANJARO 2 ILIYOTOKEA MIEZI MIWILI ILIYOPITA
KATIKA MKONDO WA NUNGWI ILIPOKUWA IKITOKEA PEMBA KUJA UNGUJA.
No comments:
Post a Comment