MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU TANZANIA BW. LUDOVICK UTOUH, AMEKUTANA
NA UONGOZI WA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) KUJADILIANA JUU YA MASUALA YA FEDHA YA
CHAMA HICHO KWA KIPINDI CHA MIAKA MITATU, KUANZIA MWAKA 2010 HADI MWAKA 2012.
AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO KILICHOFANYIKA OFISI KUU ZA CUF BUGURUNI,
BW. LUDOVICK AMESEMA NI JAMBO LA FARAJA KUONA CHAMA HICHO KIMEONESHA NJIA KWA
VYAMA VYENGINE, KIKIWA CHA MWANZO KUKAGULIWA NA CHOMBO HICHO.
BW. LUDOVICK AMBAYE ALIONGOZA UJUMBE WA OFISI YA MDHIBITI NA MKUGUZI MKUU
WA HESABU, AMEELEZEA KURIDHISHWA NA MUENDELEZO WA MASUALA YA FEDHA NDANI YA
CHAMA HICHO, NA KUAHIDI KUTOA RIPOTI KAMILI KATIKA KIPINDI CHA SIKU 21.
KIKAO HICHO PIA KILIMUHUSISHA KATIBU MKUU WA CUF AMBAYE PIA NI MAKAMU WA
KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.
WAKATI HUO HUO MAALIM SEIF AMEFANYA MAHOJIANO NA KAMPUNI YA GLOBAL
PUBLISHERS LIMITED YA DAR ES SALAAM, INAYOCHAPISHA MAGAZETI YA UWAZI, CHAMPION,
RISASI, IJUMAA NA AMANI.
PAMOJA NA MAMBO MENGINE KAMPUNI HIYO ILITAKA KUJUA JUU MAENDELEO YA CHAMA
HICHO, PAMOJA NA MAFANIKIO, CHANGAMOTO NA UTENDAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA
KITAIFA.
KUHUSU MAENDELEO YA CHAMA HICHO MAALIM SEIF AMESEMA CHAMA HICHO HAKIJAFIFIA
KAMA INAVYODAIWA NA BAADHI YA WATU, NA BADALA YAKE KIMEZIDI KUIMARIKA KATIKA
MIKOA MBALI MBALI YA TANZANIA.
AMESEMA LENGO KUU LA CHAMA CHA SIASA NI KUSHIKA HATAMU ZA DOLA, NA KWAMBA
TAYARI CHAMA HICHO KIMEKUWA SEHEMU YA SERIKALI KATIKA SERIKALI YA UMOJA WA
KITAIFA ZANZIBAR.
AKIPOULIZWA KUHUSU MADAI YA KUKIDHOOFISHA CHAMA HICHO KUTOKANA NA KUSHIKILIA
WADHIFA WA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR AKIWA PIA NI KATIBU MKUU WA
CUF, MAALIM SEIF ALISEMA KAZI KUBWA YA KATIBU MKUU NI KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA
MAJUKUMU YA CHAMA AMBAYO HUFANYWA NA WASADIZI WAKE WAKIWEZO NAIBU MAKATIBU
WAKUU PAMOJA NA WAGURUGENZI.
HIVYO AMESEMA NAFASI HIYO HAIATHIRI UFANISI WA CHAMA HICHO, NA KAMWE
HAIWEZI KUWA SABABU YA KUZOROTESHA MAENDELEO YA CHAMA, NA KUTOA MIFANO KWA RAIS
JAKAYA KIKWETE AMBAYE NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NA DKT. ALI MOHD
SHEIN AMBAYE NI MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR.
MAALIM SEIF PIA ALIZUNGUMZIA JUU YA SUALA LA DAWA ZA KULEVYA AMBAPO ALISEMA
OFISI YAKE IKIWA IMEPEWA JUKUMU HILO, IMEKUWA IKIPANGA MIKAKATI YA KILA AINA
KUONA KUWA TATIZO HILO LINADHIBITIWA.
HATA HIVYO AMEKIRI KUWEPO UGUMU WA KUKABILIANA NA TATIZO HILO KUTOKANA NA
JIOGRAFIA YA ZANZIBAR AMBAYO IMEKUWA NA NJIA NYINGI ZISIZO RASMI,
ZINAZOFIKIRIWA KUINGIZWA DAWA HIZO UKITOA VIWANJA VYA NDEGE NA BANDARI
ZINAZOTAMBULIKA.
AMESISITIZA HAJA KWA WATENDAJI WA MAMLAKA ZA VIWANJA VYA NDEGE NA BANDARI
KUWA WAADILIFU, NA KUEPUKANA NA VISHAWISHI VINAVYOWEZA KUPELEKEA UINGIZAJI WA
DAWA ZA KULEVYA KATIKA MAENEO HAYO.
AIDHA AMESEMA KWA SASA WAMEKUWA WAKIWEKA UDHIBITI KATIKA MAENEO HAYO YALIYO
RASMI, PAMOJA NA KUSAMBAZA ELIMU KWA VIJANA WAKIWEMO WANAFUNZI, JUU YA ATHARI
YA DAWA HIZO.
AMEHIMIZA MASHIRIKIANO BAINA YA VYOMBO VYA DOLA NA WANANCHI KATIKA
KUKABILIANA NA TATIZO HILO AMBALO LIMEKUWA LIKIWAATHIRI ZAIDI VIJANA AMBAO NDIO
NGUVU KAZI YA TAIFA.
“TATIZO HILI HALITOMUATHIRI MTOTO WA FULANI TU BALI TUJUE KUWA VIJANA WENGI
HATA WATOTO WA VIONGOZI NA MATAJIRI WANAATHIRIKA, KWA HIVYO KITU CHA MSINGI NI
MASHIRIKIANO BAINA YA VYOMBO VYETU VYA DOLA NA WANANCHI”, ALISISITIZA MAALIM
SEIF.
No comments:
Post a Comment