ZANZIBAR.
Kesi inayowakabili viongozi wa jumuiya NA TAASISI
ZAKIISLAM ZANZIBAR imeakhirishwa hadi
julai 3 mwaka huu AMBAPO IMEWEKEWA pingamizi na Mkurugenzi wa mashtaka
KUHUSU dhamana ILIYOTOLEWA KWA WASHTAKIWA
HAO.
Mapema muendesha mashitaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa
mashitaka DPP Raya Mselem aliwasilisha pingamizi ya kupinga UAMUZI WA Mahkama
kuu kusikiliza ombi la dhamana ya watuhumiwa hao.
LICHA YA MAHAKAMA KUU KUTOA DHAMANA KWA WATUHUMIWA BADO
UPANDE WA MASHTAKA UNAPINGA SUALA HILO NA UMEAMUA KUKATA RUFAA ILI WASHTAKIWA
WAREJESHWE TENA RUMANDE BAADA YAKUKAA NDANI MWAKA MMOJA NA MIEZI MINNE.
Hata hivyo wakili wa upande wa utetezi Abdalla Juma
aMEIomba mahkama hiyo kuakhirisha shauri hilo hadi mahAkAma ya rufaa
itakapokaa na kusikiliza RUFAA HIYO.
HATA HIVYO Jaji ISACK Sepetu hakupingana na hoja hiyo.
Watuhumiwa WALIOFIKA MAHAKAMANI LEO ni PAMOJA NA AMIRI
MKUU WA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH Farid Hadi Ahmed,AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA
UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR FADHILATU SHEIKH Mselem BIN AlY, NAIBU AMIRI WA JUMUIYA YA UAMSHO NA
MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR ZANZIBAR AL-USTADH Azan Khalid Hamdan.
WENGINE NI KATIBU
WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR AL-USTADH Abdalla Saidi,
MAUSTADH MusSa Juma Mussa, SUleiman Juma Sleiman, Khamis Ali Sleiman, hasSan
Bakari Sleiman, Gharibu Ahmada Juma, na Majaliwa Fikirini Majaliwa.
Mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu
mali, Uchochezi,Ushawishi , kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula
njama ya kufanya kosa
Kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne AL-USTADH
Azan Khalid ambae anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi
vitendo VINAWEZA v kusababisha uvunjifu wa amani.
Vitendo hivyo vinadaiwa kufanyika kati ya
Oktoba 17,18 na 19 mwaka ,2012 katika maeneo tofauti katika manispaa yaa mji wa
Zanziba ambapo washitakiwa hao wote waMEkana makosa yote hayo.
viongozi hao walipewa dhamana na mahakama kuu ya zanzibar
tarehe 27 mwezi wa pili mwaka huu baada yakutekeleza masharti yaliyowekwa.
No comments:
Post a Comment