ZANZIBAR.
VIJANA NCHINI WAMESHAURIWA KUTUMIA FURSA ZA KUJIPATIA
TAALUMA KATIKA NYANJA MBALI MBALI KUTOKA KATIKA VYUO NA TAASISI ZA ELIMU HAPA
NCHINI ILI VIWAJENGEE UWEZO WA KUJITEGEMEA WENYEWE KIMAISHA.
USHAURI HUO UMETOLEWA
NA WALIMU WA VYUO NA TAASISI
MBALI MBALI HAPA ZANZIBAR KATIKA KONGAMANO LA VIJANA WENYE TATIZO LA AJIRA
NCHINI HUKO KATIKA UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZAMANI, KIKWAJUNI MJINI
HAPA WAKATI WAKIWASILISHA MAELEZO KUHUSIANA NA KUJIUNGA, TAALUMA WANAZOZITOA,
MAHITAJI YA SOKO YA FANI HUSIKA NDANI NA NJE YA NCHI, ADA INAYOHITAJIKA ILI KUWAJENGEA UWELEWA NA KUCHUKUA HATUA ZA
MAAMUZI SAHIHI YA KUJIKWAMUA KIMAISHA.
WALIMU HAO KUTOKA
TAASISI YA SAYANSI NA TECHNOLOGIA KARUME, CHUO CHA SAYANSI YA AFYA
MBWENI,KITUO CHA UFUNDI MKOKOTONI, CHUO CHA MAENDELEO YA UTALI ZANZIBAR,KUMBU
KUMBU YA MWALIMU NYERERE, UONGOZI WA FEDHA CHWAKA,ZANZIBAR SCHOOL OF HEALTH
(SHAA) MOMBASA PAMOJA NA TAASISI YA BUISSNESS & TECHNOLOGY MWANAKWEREKWE
WAMESEMA KUWA NI LAZIMA VIJANA KULIWEKA SUALA LA ELIMU MBELE ILI WAPATE TAALUMA
HUSIKA KWA MAENDELEO YAO NA TAIFA KWA JUMLA.
VIONGOZI HAO WAMEWAOMBA VIJANA KUJIUNGA NA VYUO NA
TAASISI HIZO KWA GHARAMA NAFUU ILI KUJINUFAISHA HIVI SASA NA HAPO BAADAE.
NAO VIJANA HAO KUTOKA SEHEMU MBALI MBALI NCHINI
WAMEISHUKURU JUMUIYA YA MAENDELEO YA
VIJANA WA MIKUNGUNI (MYDO) KWA KURATIBU KUWEPO KWA KONGAMANO HILO AMBALO
LIMEWAPA FURSA NZURI YA KUPATA UWELEWA
NA KWAMBA SUALA LA ELIMU KWA AJIRA WATALIFANYIA KAZI IPASAVYO KUILINGANA NA
HALI ZAO ZA KIFEDHA.
No comments:
Post a Comment