RAIS WA ZANZIBAR NA
MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK ALI MOHAMED SHEIN AMEWATAKA WATANZANIA
KUTAMBUA KUWA KUUNDWA KWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NI MATOKEO YA
MAKUBALIANO YA WANANCHI WENYEWE CHINI YA VIONGOZI WAASISI WA MUUNGANO HUO
MAREHEMU MWALIMU JULIUS NYERERE, RAIS WA JAMHURI YA TANGANYIKA NA MAREHEMU MZEE
ABEID AMANI KARUME RAIS WA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR.
KWA HIYO AMESEMA WANANCHI WANA KILA SABABU YA
KUUTETEA, KUULINDA NA KUUNDELEZA NA PIA NI WAJIBU WAO KUJIVUNIA MUUNGANO HUO
KWA MANUFAA YA WATU WOTE.
AKIZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO HUKO
KWENYE UKUMBI WA SALAMA KATIKA HOTELI YA BWAWANI MJINI UNGUJA LEO, DK. SHEIN
AMESEMA MIAKA 50 YA MUUNGANO IMESHUHUDIA MAENDELEO MAKUBWA AMBAYO YAMEMGUSA
KILA MWANANCHI.
AMEBAINISHA KUWA KUDUMU KWA MUUNGANO HUO KUNATOKANA NA
DHAMIRA ZA DHATI ZA UMOJA WALIOKUWANAO WAASISI WAKE, SERA NZURI ZA VYAMA VYA
TANU, AFRO SHIRAZI NA CCM PAMOJA NA JUHUDI ZINAZOENDELEZWA NA VIONGOZI
WALIOFUATIA PAMOJA NA KUUNGWA MKONO NA WANANCHI.
ALIONGEZA KUWA MBALI ZA BUSARA ZA WAASISI WA MUUNGANO
LAKINI KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA ZA UPANDE WA KIJIOLOJIA NA KIJAMII ZINAONESHA
KUWA WATU WA ZANZIBAR NA TANGANYIKA NI WATU WAMOJA HIVYO MUUNGANO WAO SI TUKIO
LILILOKUJA BILA SABABU MAALUM.
DK SHEIN ALIWAKUMBUSHA WANANCHI UHUSIANO USIOTENGANIKA
KATI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MWAKA 1964 NA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA
ZANZIBAR ULIASISIWA TAREHE 26 APRILI MWAKA 1964 NA KUSISITIZA KUWA HIZO NDIZO
NGUZO KUU KWA MUSTAKABALA WA NCHI.
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
ALIWAELEZA WANANCHI WALIOHUDHURIA HAFLA HIYO KUWA MIAKA 50 YA MUUNGANO IMETOA
FURSA KWA WANANCHI WA PANDE ZOTE MBILI KUISHI WAPENDAPO KATIKA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA BILA YA KUBUGHUDHIWA KWA KUWA UHURU HUO UPO NDANI YA
KATIBA ZOTE MBILI.
KWA HIYO AMEWATAKA WATANZANIA KUZINGATIA KAULI MBIU YA
MAADHIMISHO HAYO AMBAYO NI UTANZANIA WETU NI MUUNGANO WETU,TUULINDE,
TUUIMARISHE NA TUUDUMISHE KAULI AMBAYO ALISEMA INATHIBITISHA UMUHIMU WA
UTANZANIA WETU.
ALIKIRI KUWA MUUNGANO UMEKUWA NA CHANGAMOTO ZAKE
LAKINI ALIELEZA PIA JITIHADA MBALI MBALI AMBAZO ZIMEKUWA ZIKICHUKULIWA
KUKABILIANA NA CHANGAMOTO HIZO KWA LENGO LA KUIMARISHA MUUNGANO.
KABLA YA HOTUBA YAKE, DK. SHEIN ALIZINDUA NEMBO YA
MAADHIMISHO YA MIAKA 50 KWA KUPONYEZA KITUFE.
AWALI AKIMKARIBISHA RAIS, MAKAMU WA PILI WA RAIS
BALOZI SEIF ALI IDDI ALIELEZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO YATAAMBATANA
NA SHUGHULI MBALI MBALI ZITAKAZOWASHIRIKISHA WANANCHI KWA NJIA YA MAKANGOMANO,
MICHEZO NA BURUDANI NA KUFIKIA KILELE CHAKE TAREHE 26 APRILI,2014 HUKO KATIKA
KIWANJA CHA UHURU DAR ES SALAAM.
ALIELEZA PIA KUWA KATIKA MIAKA 50 MALENGO YA MUUNGANO
YAMEKUWA YAKITEKELEZWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA NA KUELEZA KUWA WATANZANIA HAWANA
BUDI KUWASHUKURU WAASISI WA MUUNGANO PAMOJA NA VIONGOZI WALIOFUATIA KWA
KUTELEKEZA KWA DHATI AZMA YA MUUNGANO YA KUWALETEA MAENDELEO.
SHEREHE HIZO ZA UZINDUZI ZILIHUDHURIWA PIA NA MAKAMU
WA KWANZA WA RAIS MAALIM SEIF SHARIF HAMAD PAMOJA NA VIONGOZI WENGINE WAKIWEMO
MAWAZIRI WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO NA SERIKALI WA MAPINDUZI YA
ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment