RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA
MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEIHAKIKISHIA SERIKALI YA UHOLANZI KUWA
SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR INA DHAMIRA YA KWELI YA KUENDELEZA NA KUIMARISHA
USHIRIKIANO WAKE NA UHOLANZI.
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA
MAPINDUZI ALITOA KAULI HIYO JANA WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAZIRI WA
BIASHARA ZA NJE WA NCHI HIYO BIBI LILIANNE PLOUMEN ALIYEMTEMBELEA IKULU.
“NINGEPENDA KUREJEA TENA DHAMIRA YETU YA
KUENDELEZA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA UHOLANZI KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA
MAENDELEO KWA FAIDA ZA NCHI ZETU NA WATU WAKE” DK. SHEIN ALIMUELEZA BIBI
PLOUMEN.
ALIONGEZA KUWA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR
WANASUBIRI KWA HAMU KUANZA UJENZI WA WODI MPYA YA KINAMA WAJAWAZITO NA WATOTO
KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA AMBAYO ITAJENGWA KWA UFADHILI WA SERIKALI YA
NCHI HIYO KUPITIA MPANGO WA ORIO.
DK. SHEIN ALIUELEZA MSAADA WA NCHI HIYO KATIKA
SEKTA YA AFYA KUWA MUHIMU SANA KWA USTAWI WA WANANCHI WA ZANZIBAR NA HIYO
INAONESHA JINSI ZANZIBAR NA UHOLANZI ZILIVYO MARAFIKI.
ALIMUELEZA WAZIRI HUYO KUWA AMEPATA FARAJA
KUSIKIA KUWA SERIKALI YA UHOLANZI TAYARI IMELETA TIMU YA WATAALAMU HUMU NCHINI
KUFANYA UTAFITI WA UWEZEKANO WA UJENZI WA BANDARI ZANZIBAR.
“TUNAHITAJI BANDARI YA KISASA HIVI SASA IWE KWA
AJILI YA SHUGHUILI ZA ABIRIA NA MIZIGO AU HATA BANDARI YA MAFUTA NA GESI ZOTE
NI MUHIMU KWA MAZINGIRA YA UCHUMI WA ZANZIBAR HIVI SASA” ALISISITIZA DK. SHEIN.
HALIKADHALIKA DK. SHEIN ALIMUELEZA BIBI PLOUMEN
KUWA SERIKALI YA ZANZIBAR IMEFURAHISHWA NA TAARIFA KUWA UHOLANZI IMETENGA FEDHA
MAALUM KWA AJILI YA KUIJENGEA UWEZO ZANZIBAR KATIKA KUENDELEZA RASILIMALI ZAKE
IKIWEMO MAFUTA NA GESI.
KWA HIVYO ALIISHUKURU SERIKALI NA WANANCHI WA
UHOLANZI KWA MISAADA YAKE HIYO NA MENGINE AMBAYO IMEKUWA IKICHANGIA NA
KUHARAKISHA UFANIKISHAJI WA MALENGO MBALIMBALI YA MAENDELEO NCHINI.
DK. SHEIN ALIMSHUKURU WAZIRI HUYO KWA KUTEMBELEA
ZANZIBAR KUFUATIA MAZUNGUMZO YAKE WALIYOFANYA AKIWA NCHINI UHOLANZI MWENZI
AGOSTI MWAKA JANA WAKATI ALIPOFANYA ZIARA RASMI NCHINI HUMO.
“NILIFURAHI KUSIKIA UTAFANYA ZIARA NCHINI NA LEO
NIMERAFIJIKA ZAIDI KUONA UJIO WAKO UMEAMBATANA NA UJUMBE MZITO WA MAKAMPUNI
KUTOKA NCHINI UHOLANZI ”ALIELEZA DK. SHEIN NA KUONGEZA KUWA HATUA HIYO
INAFUNGUA UKURASA MPYA WA MATUMAINI NA USHIRIKIANO WA MIAKA MINGI IJAYO KATI YA
SERIKALI NA SEKTA BINAFSI.
WAKATI HUO HUO WAZIRI WA BIASHARA ZA NJE WA
UHOLANZI BIBI LILIANNE PLOUMEN ALISEMA KUWA SERIKALI YA NCHI YAKE IMEAINISHA
MAENEO YA USHIRIKIANO NA ZANZIBAR KUFUATIA ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR NA
MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALIYOIFANYA NCHINI UHOLANZI MWEZI AGOSTI
MWAKA JANA.
“TANGU ULIPOFANYA ZIARA YAKO NCHINI KWETU
SERIKALI YETU IMEKUWA IKIANGALIA NAMNA BORA YA KUISAIDIA ZANZIBAR KATIKA
KUENDELEZA RASILIMALI ZAKE IKIWEMO MAFUTA, GESI PAMOJA NA MIUNDOMBINU YA
USAFARI WA BAHARINI IKIWEMO UJENZI WA BANDARI”ALIELEZA BIBI PLOUMEN.
KATIKA KUFANYA HIVYO ALIELEZA KUWA SERIKALI YA
NCHI YAKE IMETENGA FEDHA MAALUM KWA AJILI YA MAFUNZO YA KUIJENGEA UWEZO
ZANZIBAR KUENDELEZA RASILIMALI ZAKE IKIWEMO SEKTA YA MAFUTA NA GESI.
“TUMEBAINI (SERIKALI YA UHOLANZI)MAENEO YA
KUSHIRIKIANA NA MAKAMPUNI UTAKAYOONANA NA LEO(JANA) YANA WELEDI MKUBWA KATIKA
MAENEO HAYO AMBAYO NI PAMOJA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA USAFIRI WA BAHARINI,
UJENZI WA BANDARI, MAFUTA NA GESI, MAPATO NA KODI KATIKA RASILIMALI NA TAASISI
YA MAFUNZO”ALIFAFANUA BIBI PLOUMEN.
ALIELEZA KUWA UJIO WA MAKAMPUNI HAYO KUTOKA
NCHINI KWAKE NI SEHEMU YA JITIHADA ZA SERIKALI YA NCHI YAKE NA ZANZIBAR YA
KUIMARISHA UHUSIANO BAINA YA SERIKALI ZAO NA USHIRIKIANO BAINA YA SEKTA BINAFSI
ZA NCHI MBILI HIZO.
MAZUNGUMZO HAYO YALIHUDHURIA PIA NA BAADHI YA
MAWAZIRI NA MKATIBU WAKUU PAMOJA NA KATIBU MKUU KIONGOZI DK. ABDULHAMID YAHYA
MZEE.
No comments:
Post a Comment