ZANZIBAR
RAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEZIKUMBUSHA WIZARA NA IDARA ZA
SERIKALI KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KWA WAKATI NA KURIPOTI KWA MAMLAKA HUSIKA ILI
MATOKEO YAWEZE KUTOLEWA KWA WANANCHI.
AKIHITIMISHA KIKAO CHA KUJADILI UTEKELEZAJI WA MPANGOKAZI WA WIZARA YA
MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO KWA KIPINDI CHA JULAI 2013 HADI MACHI 2014 IKULU
JANA DK. SHEIN ALISISITIZA UMUHIMU KWA WIZARA NA IDARA ZA SERIKALI KUTUMIA
MAMLAKA ZINAZOONGOZA WIZARA NA IDARA ZA SERIKALI KUJADILI MASUALA YAO NA
KUYACHUKULIA HATUA.
DK. SHEIN AMELEZA NA KUSISITIZA MASHAURIANO KATI YA WIZARA NA BODI
ZINAZOSIMAMIA TAASISI ZA SERIKALI KUWA NI LAZIMA YAFANYIKE MARA KWA MARA NA
KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA ZILIZO JUU YAKE.
AIDHA DK.SHEIN AMEBAINISHA KUWA WAJIBU WA BODI HIZO NI KUZISAIDIA WIZARA
KUSIMAMIA TAASISI ZILIZO CHINI YAKE KWA MUJIBU WA SHERIA NA TARATIBU
ZILIZOWEKWA HIVYO MAWASILIANO YA MARA KWA MARA NA WIZARA NI KITU CHA LAZIMA.
AMESEMA NA KUSISITIZA KUWA HUO NDIO UTARATIBU UNAOPASWA KUFUATWA ILI
SHUGHULI ZA SERIKALI ZIWEZE KUFANYIKA KWA WAKATI NA KWA UFANISI.
KATIKA KIKAO HICHO MHE RAIS AMEZIAGIZA WIZARA ZA SERIKALI KUVIPATIA NYENZO
VITENGO VYA UKAGUZI WA NDANI KWA MUJIBU WA MAHITAJI NA UWEZO WA FEDHA ULIOPO
ILI VITENGO HIVYO VIWEZE KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKAMILIFU NA KWA
UHURU.
AWALI AKIWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI MPANGOKAZI WA WIZARA HIYO KATIBU
MKUU DK. JUMA MALIK AKIL ALIELEZA KUWA KATIKA KIPINDI HUSIKA WIZARA YAKE
ILIPANGA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO 14 INAYOJUMUISHA UJENZI WA BARABARA,
MIUNDOMBINU YA VIWANJA VYA NDEGE NA BANDARI PAMOJA NA MRADI WA MAGEUZI YA MFUMO
WA TAASISI.
AMEFAFANUA KUWA MIRADI HIYO IMEZINGATIA UTEKELEZAJI WA MIPANGO MIKUU YA
MAENDELEO YA NCHI IKIWEMO DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2020, MKAKATI WA KUKUZA
UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI-MKUZA II, SERA YA USAFIRI ZANZIBAR, SERA YA
TEHAMA NA MPANGO MKUU WA USAFIRI ZANZIBAR (ZANZIBAR TRANSPORT MASTERPLAN 2009).
KWA UPANDE WA UKUSANYAJI MAPATO, DK AKIL ALIELEZA KUWA HADI MWEZI MACHI
2014 WIZARA YAKE IMEWEZA KUKUSANYA JUMLA YA SHILINGI MILIONI 306 IKIWA NI
ASILIMIA 75 YA LENGO LA WIZARA HIYO LA KUKUSANYA SHILINGI MILIONI 406 KWA MWAKA
WA FEDHA WA 2013/2014.