tangazo

tangazo

Saturday, January 30, 2016

makabidhiano ya bajaji

 naibu katibu mkuu wizara ya ustawi wa jamii jinsia wanawake na watoto msham abdallah khamis akizungumza kabla ya makabidhiano ya bajaji kutoka save the chidren

 naibu katibu mkuu msham akitia saini pembeni yake bi mali
 bi mali kutoka save the children zanzibar akijaribu bajaji


 katibu msham akikabidhiwa funguo
katibu msham akijaribu kuendesha bajaji

jumla ya bajaji mbili zenye thamani ya milioni12 na laki 3 zimetolewa na save the children kwa ajili ya kusaidia kuongeza mapambano katika ufatiliaji wa kesi za udhalilishaji ambapo moja etapelekwa kaskazini na nyengine itatumika mjini katika kitengo cha hifadhi ya mtoto

Friday, January 15, 2016

KMKM WASAINI KINDA, BUSHIR ASEMA HUYU NI ZAIDI YA BAGAWAI WA YANGA




Na Abubakar Khatib (Kisandu)  , Zanzibar.

Timu ya mabaharia ya KMKM inayoshiriki ligi kuu soka visiwani zanzibar , leo hii imethibitisha rasmi kumsajili mlinzi wa kushoto kinda kutoka timu ya Muembe Beni United ambae anaitwa Adam Abdallah na watu wengi humwita BAGAWAI wakimfananisha na mlinzi wa kushoto wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Yanga Mwinyi Haji Ngwali kwa alivofanana uchezaji wake na mlinzi huyo.

 Mtandao huu tumeongea na kocha Ali Bushir wa KMKM na akithibitisha kumsajili kinda huyo katika dirisha hili dogo la usajili la ligi kuu soka zanzibar huku kocha huyo akiamini mtoto huyo mwenye miaka 16 atamshinda MWINYI wa Yanga kwa mafanikio.

“ Ni kweli nimemsajili huyu kijana Adam na kwasasa ni rasmi ni mchezaji wa KMKM, huyu kijana ana kipaji sana na naamini atafika mbali mana yupo kama Mwinyi wa Yanga”. Alisema Bushir.

Hatukuishia hapo tukapiga hodi moja kwa moja mpaka kwenye klabu ya Muembe Beni United inayoshiriki ligi za madaraja ya vijana Wilaya ya Mjini na tukazungumza na kocha wa timu hiyo Suleiman Hamid (Mzee Ole) na kuthibitisha kuwa kweli leo wamemalizana na KMKM kuhusu mchezaji wao ambae ni BAGAWAI two.

“ Ni kweli leo tumemalizana na KMKM kuhusu Adam, naamini huko alipoenda atafanya vizuri mana kocha Bushir anajua kukuza vipaji”. Alisema Mzee Ole.

Tukamtafuta mchezaji mwenyewe huyo Adam Abdallah ambae leo rasmi KMKM wamemsajili huku akifurahi kucheza timu hiyo na amesema kuwa atapambana katika klabu ya KMKM kwenye ligi kuu soka ya zanzibar.

“ Nimefurahi kusajiliwa na KMKM na ntaweza kucheza nikipewa nafasi mana Muharami wa Black Sailors ameweza na mimi ntaweza , Kocha Bushir ameniona kwenye timu yang undo kanisajili, nimefurahi kusajiliwa KMKM pia nawashukuru makocha wangu akiwemo Vigema, Mzee Ole na Kocha THEO mana wote wamenisaidia”. Alisema BAGAWAI TWO.

shaka hamdu shaka kaimu katibu mkuu uvccm taifa akizungumzia juu ya bango liloleta sintofahamu zanzibar


CHIMBENI KHERI AWA MSHAURI WA RAIS MAMBO YA UTAMADUNI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amemwapisha Bwana Chimbeni Heri Chimbeni kuwa Mshauri wa Rais Masuala ya Utamaduni kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana ambapo aliteua pia watendaji wengine wa serikali.

Watendaji wengine walioapishwa leo ni Bwana Juma Hassan Juma Reli kuwa Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, Bwana Mdungi Makame Mdungi kuwa Katibu Kamisheni ya Utumishi wa Umma na Bwana Kai Bashir Mbarouk kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria.

Bwana Reli ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania anachukua nafasi ya Bi Amina Khamis Shaaban ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi wa kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma bwana Mdungi alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba Sheria.

Kwa upande wa Bwana Kai Bashir kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Wizara hiyo.

Hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Said Hassan Said.


Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyihaji Makame, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman, Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdulla Mwinyi na Makatibu na Manaibu Katibu wakuu wa wizara mbalimbali.

Wednesday, January 13, 2016

MKWASA AWAPA DOZI YA SIKU 1 MAKOCHA ZANZIBAR



Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.

Kocha mkuu wa Timu ya soka Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)  Charles Boniface Mkwasa Juzi alitembelea  kwenye darasa wanalokutana makocha mbali mbali wa Soka visiwani Zanzibar  katika skuli ya Sekondari ya Haile Selasies na kuwapiga msasa wa siku moja pamoja na kubadilishana mawazo na makocha hao.

Mkwasa alifurahishwa mno baada ya kupata mualiko kutoka kwa Chama cha Makocha Zanzibar (ZAFCA) kwa kuwatembelea makocha hao ambapo huwa na kawaida ya kukutana mara kwa mara.

“Nimefurahi kupata mualiko kama huu kukutana na makocha wenzangu wa hapa visiwani , na pia nimependa utaratibu wenu wa kukutana mara kwa mara makocha nyote wa hapa visiwani kwa kubadilishana mawazo na kupeyana elimu ya ukocha, na mimi ntawashauri wenzangu kule bara tufanye kama hivi. Alisema Mkwasa.

Mbali na kuwapiga msasa makocha hao mtandao huu ukataka kujua kwa mwalimu huyo kuhusu kombe la Mapinduzi lililohitimishwa leo hii kati ya Mtibwa Sugar na URA ya Uganda huku akikiri  kuwa kweli vipaji vipo visiwani kwenye michuano hiyo pia akiipa tano timu ya JKU.

“ Vipaji vipo vingi sana hapa Zanzibar, kuna vijana nimewaona na ntawaita muda utakapofika, nimewaona kwenye timu zote tatu zilizoshiriki Mapinduzi kutoka Zanzibar, Jamhuri wapo nimewaona, Mafunzo pia nimewaona, na hata JKU wapo wengi wana vipaji”.Alisema Mkwasa.

Thursday, January 7, 2016

TUHESHIMU NYAKATI LUQMAN MALOTO



TUHESHIMU NYAKATI
Mbwana Samatta ameitoa kimasomaso Tanzania. Watanzania waliomba na kutarajia na hakika imekuwa kweli. Hongera sana Mbwana kwa kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika kwa wachezaji wa ndani ya Bara la Afrika.
Tuzo ya Mbwana ina maana gani? Neno moja tu linatosha kujibu swali “Nyakati.”
Naam! Mbwana yupo kwenye wakati wake, ilikuwa lazima ashinde kwa sababu huu ni wakati wake, asingeshinda mwaka jana kwa sababu haukuwa wakati wake. Anaweza kushinda tuzo nyingine mwakani na kuendelea kama ni wakati wake.
Mwanamuziki Diamond Platnumz au Nasibu Abdul Juma, anatikisa Afrika kwa sasa akitokea Tanzania, ni kwa sababu huu ni wakati wake. Kila akigusa chupa, inakuwa almasi. Ni wakati wake.
Lazima kuheshimu nyakati. Na mafanikio ya Mbwana na Diamond, yawe fundisho kwa kila mmoja kutambua wakati wake na kuutumia vizuri kufika mbali na kupata mafanikio stahiki.
Wapo wengi hawakutumia vizuri nyakati zao. Alikuwepo fundi Haruna Moshi ‘Boban’, akasajiliwa Gefle IF ya Sweden mwaka 2010. Akatarajiwa kufika mbali. Haikuwa hivyo, alirejea nchini kwa kususa na alipofika Bongo, hakuwa Boban yule tena!
Ni nyakati za Floyd Mayweather! Anapigwaje sasa na wakati yupo kwenye wakati wake? Anatangaza kustaafu kisha anarejea ulingoni na hapigiki. Siku nyakati zake zikitoweka, atapigwa akiwa amelegea kama matembele.
Zilikuwepo zama za Mike Iron Tyson! Ilikuwa kabla hujaingia ulingoni, hakikisha umepima ubongo wako, maana ngumi yake ni kama bomu. Ikiwa ubongo wako haupo imara, akikupiga ngumi ya kichwa unakuwa mwendawazimu. Msome Frank Bruno yaliyomkuta.
Tyson alikuwa anamaliza pambano na kuingiza mpaka dola milioni 50 ndani ya sekunde 27. Aliyejifanya sugu na kusogea naye mpaka raundi 12, alikiona cha mtema kuni. Ila zilifika nyakati Tyson akawa akifika raundi ya sita anapigwa kirahisi kama mlenda. Yupo wapi Muhammad Ali? Zama zake zilishapita!
Unawakumbuka magolikipa tishio ulimwenguni kama Peter Schmeichel na Oliver Kahn? Walikuwa habari nyingine kila mtu katika wakati wake. Ni jambo zuri kuwa kila mmoja aliutendea haki wakati wake.
Ni kama Lionel Messi leo anavyoutendea haki wakati wake, kama ilivyo kwa Cristiano Ronaldo.
Zimepita zama za Ronaldinho Gaucho na Ricardo Kaka. Pamoja na kutikisa dunia lakini ukweli usiopingika ni kuwa hawakuzitendea haki nyakati zao, maana walidumu kwa kitambo kifupi mno kuliko viwango walivyokuwa navyo.
Wapi Zinedine Zidane ‘Zizzou’ na Ronaldo de Lima? Uliza kuhusu Luis Figo, Rivaldo, David Beckham na Thierry Henry? Je, maveterani Pele, Garrincha, Maradona, Romario, Lothar Matthäus, Marco Van Basten, Roberto Baggio na wengine?
Zilipowadia zama za George Weah, alichomoza kutoka Liberia, taifa lililokuwa na machafuko ya kivita, lisilo na rekodi ya soka, lakini alifika mpaka kileleni, akawa Mchezaji Bora wa Dunia, Mchezaji Bora wa Ulaya na Mchezaji Bora wa Afrika. Tuzo tatu kwa mkupuo mwaka 1995. Usichezee na nyakati!
Golini kabla ya Juma Kaseja, walimtangulia akina Mohamed Mwameja, Idd Pazi ‘Father’, Peter Manyika, Juma Pondamali, Athuman Mambosasa, Omar Mahadhi na wengineo. Ni nyakati!
Zama za Edibily Lunyamila, ungesema nini kwenye soka la Tanzania? Kama ilivyokuwa kwa Zamoyoni Mogella. Zilishakuwepo zama za mashuti ya Said Sued ‘Scud’ na Dua Said. Alitisha James Tungaraza mpaka akaitwa Boli Zozo.
Joseph Kaniki yupo jela Ethiopita, akitumia adhabu ya kunaswa na madawa ya kulevya. Ila nyakati zake alikuwa anafunga magoli popote kutokana na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti. Watanzania walimwita Golota.
Na hii ndiyo sababu walishakuwepo akina Sunday Manara ‘Computer’, walipoondoka wakafuata akina Malota Soma, Edward Chumila, Hussein Marsha, na wengine, walipopisha walifuata akina Muso, Mgosi, Tegete, Ngassa na wengine! Ni kupishana kwa nyakati!
Walikuwepo Tupac Shakur na Notorious BIG, wakaimbwa ulimwengu mzima. Hip Hop iliwatazama wao tu! Walifuata akina Nas, Mase, DMX, Ja Rule, Eminem, 50 Cent na wengine! Jay Z anaendelea kucheza na nyakati, watu sasa hawaambiwi kitu kuhusu Kanye West, Lil Wayne, Wiz Khalifa, Kendrick Lamar, Drake na wengine!
Unawezaje kusahau zama za Bow Wow na Lil Romeo, walivyochuana kutengeneza fedha wakiwa watoto? Huwezi bila shaka kusahau vipindi vitamu vya wakubwa, Dre, Snoop Dog, hayati Big Punisher, Fat Joe, Coolio, LL Cool J, Ice Cube, Scarface na wengine.
Huu ni muda wa Justin Bieber, Chris Brown, The Weekend na wengine. Usher Raymond na Timbelake wanarudirudi. Hutasahau kuwa walikuwepo akina Baby Face, Joe Thomas, Lionel Richie na wengine! Yupo wapi Mfalme Michael Jackson?
Kipindi hiki Rihanna akionekana ndiye malkia, unadhani anafikia robo ya makeke ya Jennifer Lopez alipokuwa kwenye kiwango chake? Anafua dafu kwa Britney Spears na Christina Aguilera? Walikuwepo malkia wengine kama Janet Jackson, Whitney Houston, Mariah Carey na wengineo.
Wakati zikijadiliwa stori za nani anaweza sana ‘kuchana’ kati ya Nick Minaj na Iggy Azalea, kabla yao walikuwepo wakali kama Left Eye, Missy Eliot, Da Brat, Lil Kim na wengine.
Adolph Hitler kwa wakati wake alitawala dunia. Saddam Hussein alipokuwa kwenye wakati wake, alishambuliwa na mataifa zaidi ya 10, yakiongozwa na Marekani mwaka 1991 katika Vita ya Ghuba ya Uajemi, lakini hawakumuweza. Mwaka 2003, Marekani na Uingereza peke yake walimng’oa na ikawa sababu ya kukamatwa kisha kunyongwa. Ni kwamba mwaka 2003 hazikuwa zama za Saddam ndiyo maana alipigwa kirahisi.
Zilikuwepo zama za Michael Jordan na Magic Johnson kwenye kikapu, kabla yao walikuwepo akina Larry Bird, Moses Malone na wengine. Baadaye walifuata akina Shaquille O'Neal, Allen Iverson, Tim Duncan, Steve Nash, Kobe Bryant, LeBron James na sasa Stephen Curry ameshavuta kiti na ameketi.
Siasa za nchi kwa sasa zinamtazama Rais John Magufuli lakini kabla yake alikuwepo Jakaya Kikwete, kama alivyotanguliwa na Benjamin Mkapa, Ali Hassan Mwinyi na Baba wa Taifa, Julius Nyerere.
Upinzani leo wanatazamwa Edward Lowassa, Zitto Kabwe, Freeman Mbowe, Tundu Lissu na wengine, kabla yao walitikisa akina Augustino Mrema, Willibroad Slaa, marehemu Christopher Mtikila, Ibrahim Lipumba na wengineo. Ni nyakati!
CHUKUA SOMO
Juhudi huvuta bahati na bahati ndiyo itakufanya ufike kwenye kipindi chako cha mafanikio.
Muongozo ni wewe kujituma na utakapofika kwenye wakati wako, hakikisha unautumia vizuri ili utakapopita, watu waseme “alikuwepo fulani bwana!”
Pambana kwenye eneo lako ili utengeneze wakati wako mzuri. Utakuwa mwenye kupendwa na kuheshimika sana kama utafikia wakati wako na kufanya kile kinachohitajika.
Huu ni wakati wa Mbwana Samatta, kama ilivyo Diamond Platnumz na Ali Kiba. Hongera nyingi kwao.
Ijumaa Kareem.
Ndimi Luqman Maloto

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haruon Ali Suleiman afungua skuli ya zingwezingwe

Na Ali Issa Maelezo –Zanzibar
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haruon Ali Suleiman ameshauri  walimu watakaosomesha Skuli ya Zingwezingwe wawe walimu wanaoishi karibu na  kijiji hicho.
Hayo ameyasema leo huko Zingwezingwe Mkoa wa Kaskazini, Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Unguja, wakati alipokuwa akifungua skuli mpya ya msingi ya kijiji hicho ikiwa ni miongoni mwa  shamra shamra za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar .
Ametaka ushauri huo ufanyiwe kazi  na iwapo watahitajika walimu wapya  kuajiriwa kwa  ajili ya kufundisha katika skuli hiyo  Wizara yake   ambayo ndiyo  inayohusika na  masuala ya ajira   watakuwa tayari  kufanya hivyo.
“Ni vyema kuajiri walimu wakaazi  na wenyeji wa kijiji cha Zingwezingwe  wenye kuyaelewa mazingira ya kijiji hicho na mimi kama Waziri wa Ajira niko tayari   kusaidia hilo,” alisema Waziri Haroun.
Aidha aliwashauri wanafunzi  wanaosoma  katika skuli hiyo  kuitumia  frusa waliyoipata  kusoma kwa juhudi  kwani hiyo ni skuli ya kwanza  kujengwa katika kijiji hicho.
Hata hivyo aliwataka wazazi  na walezi kwa  upande wao kutimiza wajibu wao  wa kufuatilia kikamilifu maendeleo ya Watoto  wao  na kutoa ushirikiano  kwa walimu ili kufanikisha maendeleo ya watoto wao.
Waziri Haroun  aliwataka walimu kusomesha kwa juhudi kwani serikali  tayari imeshatoa maelekezo ya kuwaongezea maslahi yao  mara itakaporudi madarakani baada ya uchaguzi  wa marejeo.
Katika kuongeza ujenzi wa madarasa mengine ya kusomea katika Skuli hiyo, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi na Utawala wa Umma  alichangia matofali 1000 ambapo ujenzi wake utaaza hivi karibuni.
Nae Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Mama Asha Balozi akitoa salamu za Baloz Seif Ali Idd alisema suala la umeme katika skuli hiyo litafanywa na Makamu huyo wa Rais.
 Ujenzi wa skuli hiyo yenye  madarasa  manne na Ofisi ya Mwalimu Mkuu umegharimu shilingi milioni 66 ambazo zimetolewa na  Shirika la Maendeleo la Sweden SIDA, Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B, Mbunge na Mwakilishi na Wazee wa kijii cha Zingwezingwe.

Waziri  wa Fedha Mhe,Omar Yussuf Mzee azindua rasmi jumuiya ya Young Peoneer Veterani Association

Na  Khadija  Khamis  -Maelezo  zanzibar
Waziri  wa Fedha Mhe,Omar Yussuf Mzee amesema kuanzishwa kwa Jumuiya ya vijana wa paunia wa zamani (Young Peoneer Veterani Association )  kutasaidia vijana kujikwamua na umasikini pamoja na kujiepusha  na madawa ya kulevya .
Alisema tunashuhudia vijana wengi wa Zanzibar wanaendelea kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo madawa ya kulevya na kupelekea  mmong’onyoko wa maadili .
Hayo aliyasema leo huko katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo wakati alipokuwa akizindua Jumuiya mpya isiyokuwa  ya  kiserikali Young Peoneer Vererani  Association yenye  lengo la kuwasaidia vijana  wa Zanzibar kimaendeleo.
Waziri  Mzee amekemea  tabia ya vijana kutokuwa na maadili na kujiingiza katika vikundi viovu jambo ambalo linapelekea kuhatarisha maisha na kwenda kinyume na silka na utamaduni wa Zanzibar .
“  Hii inaonesha utofauti mkubwa  uliopo wa malezi heshima na tamaduni  zilizokuwepo awali  zimetoweka  kwa kuvaa nguo zisizostahiki na kupenda maisha ya anasa wakati uwezo wao ni mdogo.”Alisema Waziri  Omari.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa na ushirikiano wa pamoja ili wawe na uwadilivu katika kazi zao waepukane na tamaa.
Sambamba na hayo Waziri Omari alianzisha harambee ya papo kwa papo na kuweza kukusanya fedha ya zaidi ya Tshs millioni 3,834,500 za papo kwa papo na Tshs Millioni 5,850,000 za ahadi  jumla shilling millioni 9,724,500 zilichangiwa Jumuiya hiyo .
Hata hivyo Waziri huyo aliahidi kutoa Komputa mpya moja na Printa mpya moja na pesa taslimu Tshs milioni moja na laki tano pamoja na Tshs milioni moja kwa ajili ya mchango wa mkewe ili kuweza kuisaidia jumuiya hiyo .
Nae Katibu wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii Vijana,Wanawake na Watoto  Asha Ali Abdalla kwa niaba ya Waziri Uwezeshaji ,Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zainabu Omar Muhammed alisema ushirikiano wa jumuiya utaleta mafanikio kwa vijana wa Zanzibar  na  Jumuiya wasisiste kuitumia wizara yake kwa matatizo mbali mbali ambayo  yatayojitokeza.

WAZIRI WA NCHI TAWALA ZA MIKOA NA IDARA MAALUM ZA SMZ AFUNGUA MRADI WA MAJI MAKUNDUCHI MKOA WA KUSINI UNGUJA.

 Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Muh. Haji Omar Kheri akifungua mtambo wa maji
 Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Muh. Haji Omar Kheri akifungua pazia pamoja na kufungua Maji kuashiria ufunguzi rasmin wa Mradi wa Maji safi katika Kijiji cha Makunduchi Mkoa kusini Unguja, ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Muh. Haji Omar Kheri akisalimiana na wafanyakazi wa Mamla ya Maji Zanzibar (ZAWA) mara baada ya kufika Kijiji cha Makunduchi kufungua mradi wa Miji ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Baadhi ya wageni walikwa waliohudhuria katika ufunguzi wa Mradi wa Maji safi uliozinduliwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Tenki jipya la kuhifadhia Maji lililopo Makunduchi.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Ali halili Mirza akitoa taarifa ya kitalamu wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Maji safi uliozinduliwa Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na Idara Maalum Muh. Haji Omar Kheri akizungumza na wananchi wa Makunduchi katika ufunguzi wa mradi wa Maji safi, ikiwa ni shamrashamra za kuazimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amewataka wananchi wa kijiji hicho kushirikana na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) ili kuendeleza miundo mbinu hiyo na pia amewata kuchangia kiasi cha pesa kwa wale watakao pata Maji. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

MAALIM SEIF AWATAKA WANANCHI WAWE WATULIVU

ZANZIBAR                                            
Na: Hassan Hamad (OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema juhudi za kuutafutia ufumbuzi mkwamo wa kisiasa Zanzibar zinaendelea, na kuwataka wananchi waendelee kuwa watulivu.
Amesema katika kipindi hiki cha mazungumzo maneno mengi ya kuwavunja moyo wananchi hasa kutoka vyama vya upinzani yatasemwa, lakini amesema ufumbuzi wa tatizo hilo utapatikana kwa kuheshimu misingi ya katiba na sheria za nchi.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar katika salamu zake za kuwakaribisha waumini wa dini ya kiislamu waliohudhuria Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW).
Amesema katika kuutafutia ufumbuzi mzozo huo, atahakikisha kuwa maamuzi ya wananchi waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015 kwa kuchagua viongozi wanaowataka yanaheshimiwa.
Ameeleza kuwa amefanya Maulid hayo ya kila mwaka huku nchi ikigubikwa na mkwamo wa kisiasa, na kusisitiza kuwa ufumbuzi wake utapatikana kwa kuzingatia matakwa ya kikatiba na sheria.
Maalim Seif ambaye ni mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), ametoa kauli hiyo siku moja tu baada ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kutamka hadharani kuwa yeye ni Rais halali wa Zanzibar kwa mujibu wa katiba, na kuwataka wasioridhika waende mahakamani.
Amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi hatika hafla hiyo ya Maulid, na kuwataka waendeleze umoja na mshikamano wao, sambamba na kudumisha amani na utulivu.
“Najua kuwa yatasemwa mengi katika kipindi hiki, lakini narejea wito wangu kwa wananchi kuwa musichokozeke”, alisistiza Maalim Seif.
Hafla hiyo ya Maulid iliyoishirikisha Madrasat Nuur Islamiyya ya Ukutani Zanzibar, imehudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Rais mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Haruna Lipumba pamoja na Mzee Hassan Nassor Moyo.

Tuesday, January 5, 2016

MUAMUZI YOYOTE ATAKAEBORONGA MAPINDUZI CUP ATAPIGWA KITANZI,  ALIYEKATAA BAO LA MTIBWA VS AZAM AMESHAKUWA MFANO


Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.

Kamati inayosimamia kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar imetoa angalizo kwa mara nyengine kwa waamuzi wote wanaosimamia michuano hiyo.

Akizungumza nasi kwa msisitizo mkubwa Hashim Salum ambae ni mjumbe wa kamati ya kombe hilo alisema hawatomuangalia muamuzi usoni.

“Awali kabla ya michuano hii tuliwaita waamuzi wote na tukawaeleza hali halisi ya michuano ukubwa wake na hadhi yake kwa kuwaambia lazima wafate sheria 17 za mpira , sasa atakaeboronga hasa kwa makusudi kwa maslahi yake binafsi, lazima tumfute kwenye mashindano yetu”. Alisema Hashim.

Jana kamati hiyo ilimfuta kwenye mashindano hayo Mwamuzi wa pembeni Dalila Jaffar Mtwana aliyechezesha mechi kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar kufuatia kulikataa bao la Mtibwa Sugar kwenye mchezo uliochezwa siku ya Jumapili January 3, 2016.

Mwamuzi huyo alilikataa bao halali lililofungwa na Kichuya wa Mtibwa Sugar kipindi cha pili cha mchezo huo ambalo lingeipa ushindi timu ya Mtibwa Sugar kwenye mcheo huo ambao ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kukataliwa kwa bao hilo kulizua tafrani kati ya waamuzi waliochezesha mchezo huo dhidi ya wachezaji wa Mtibwa na bechi zima la ufundi hali iliyolazimu jeshi la polisi kuwatoa waamuzi hao uwanjani wakiwa chini ya ulinzi mkali.

MECHI YA YANGA NA AZAM YAVUNJA RIKODI UWANJA WA AMAAN




Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar

Mchezo ulopigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Amaan katika kombe la mapinduzi kati ya Yanga na Azam umeingiza mashabiki wengi kuliko hata fainali ya mwaka jana kati ya Simba na Mtibwa Sugar.

Mbali ya rikodi hiyo pia mchezo huo umevunja rikodi ya kuingiza watu wengi kuliko michezo yote iliochezwa hadi sasa kwenye michuano hiyo.

Katika mchezo huo ambapo Azam na Yanga wametoka sare ya kufungana 1-1 umeingiza mashabiki mpaka wengine wamekosa pa kukaa jambo ambalo likapelekea kukaa kwenye Tatan za uwanja huo.

Mchezo mwengine unaotarajiwa kuingiza mashabiki wengi utakaochezwa kesho saa 2:15 usiku kati ya Yanga na Mtibwa Sugar ambapo Yanga anahitaji sare tu ili isonge nusu fainali wakati Mtibwa Sugar watalazimika washinde ndipo asonge mbele hasa ikiwa Azam ataifunga Mafunzo katika mchezo unaotangulia kuchezwa mapema kesho.

Kwasasa mechi wanapokutana Yanga na Azam huwa ya ushindani zaidi na hata kufikia hatua ya wachezaji kutaka kurushiana masumbwi jambo ambalo huwenda ikapelekea kuwa ndio mechi kubwa zaidi Tanzania kuliko hata watakapokutana wapinzani wa Jadi Simba na Yanga.

Uwanja wa Amaan unachukua jumla ya Watazamaji  15,000 ambapo pia ndo uwanja mkuu wa michezo Zanzibar , ukiwemo mpira wa miguu kama ada yake lakini hata riadha  na mambo mengine zikiwemo sherehe hasa za Mapinduzi januari 12 kila mwaka.

BEKI WA YANGA AFURAHIA KUCHEZA MAPINDUZI CUP KWA MIAKA3 MFULULIZO



Na: Abubakar Khatib (Kisandu), Zanzibar.

Mlinzi wa kushoto wa timu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania  Mwinyi Haji Ngwali (Bagawai) anajivunia kucheza kombe la mapinduzi kwa miaka mitatu mfululizo kwa timu tatu tofauti.

“ Ukweli ni jambo zuri kwenye maisha ya Soka kucheza kombe kama hili miaka mitatu mfululizo kwa timu tatu tofauti, najivunia na pia ninafuraha sana, kwanza nipo nyumbani Zanzibar, pili kombe hili naliheshimu kwani limenipa umaarufu mkubwa mimi binafsi, na pia nimejisikia furaha sana nilipoiyona familia yangu wamekuja hapa Amaan kuniangalia Babaangu mzazi na Kaka Makame umewaona wamekuja kunipa sapoti, ukweli nina furaha KISANDU mpaka sina tena cha kusema”. Alisema Mwinyi.

Mwinyi Haji alianza kucheza kombe hilo mwaka 2014 (Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ) akiichezea timu ya Chuoni na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mashindano hayo, lakini mwaka 2015 akaitumikia timu ya Mabaharia ya KMKM na mwaka huu anatoa huduma yake katika timu yake mpya ya Yanga pia ameweka rikodi ya kucheza kombe hilo mara tatu mfululizo akihudumu timu tatu tofauti kila mwaka.

WANANCHI WATAKIWA KUTOA MASHIRIKIANO MAPAMBANO DAWA ZA KULEVYA.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika sasa katika kuona Wananchi wanalazimika ipasavyo kutoa mashirikiano ili kufanikisha ile azma ya Serikali Kuu ya kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya Nchini.
Amesema kukosekana ushirikiano katika kutoa ushahidi Mahakamani dhidi ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya ambako kunawahusu zaidi Wananchi wanaokuwa karibu na wahusika hao inapelekea kufutwa kwa kesi na hivyo kudumaza juhudi za Serikali katika vita dhidi ya matumizi ya dawa hizo.
Balozi Seif Ali Iddi almesema hayo baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za kulevya hapo Kidimni Wilaya ya Kati ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari  1964.
Alisema suala la Dawa za kulevya hivi sasa limekuwa janga la Dunia kwa vile ni  la muda mrefu na kuathiri watu wengi hasa Vijana. Hivyo udhibiti wa matumizi yake unahitaji maamuzi magumu ya Serikali pamoja na ushirikiano wa Kitaifa Kikanda na Dunia kwa ujumla.
Balozi Seif alisema licha ya changamoto zilizopo za utekelezaji wa sheria na kanuni za udhibiti wa dawa za kulevya katika kukabiliana na wimbi la uingizaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya Nchini, lakini Serikali kupitia vyombo vyake vya dola imefanikiwa kuwakamata wahusika wa biashara hiyo katika kipindi cha mwaka 2015.
Balozi Seif alifahamisha kwamba suala la rushwa limekuwa likipewa nafasi kubwa kuwa ni miongoni mwa vikwazo vya kupata mafanikio dhidi ya vita vya dawa za kulevya licha ya juhudi kubwa inayochukuliwa na Serikali katika kupambana dhambi hiyo ya rushwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwanasihi walioanzisha nyumba hizo pamoja na Vijana wanaoishi kwenye nyumba hizo kujitahidi kutoshawishika kurudi nyuma kwa kujiingiza tena katika janga la matumizi ya dawa za kulevya.
Mapema  akitoa Taarifa ya ujenzi wa Kituo hicho Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dr.Omar Dadi Shajak alisema ujenzi wa kituo hicho unagharimiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa zaidi ya Shilingi Bilioni  Nne na Milioni Mia Mbili { 4,200,000,000/- } hadi kukamilika kwake.
Dr. Shajak alisema Kituo hicho cha aina yake ndani ya ukanda wa Mwambao wa Afrika Mashariki kitakuwa na uwezo wa kuhudumia Vijana wapato 200 wake kwa waume kwa wakati mmoja ambapo pamoja na mambo mengine kutakuwa na mafunzo ya kazi za amali, michezo na huduma nyengine za kurekebisha tabia.
Dr. Omar Dadi Shajak alifahamisha kwamba  Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika kukabiliana na wimbi la uingizaji, uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya tayari imeshaandaa zawadi kwa Mtu au Kikundi kitakachojitolea kutoa Taarifa ya kukamatwa kwa wahusika wa dawa za kulevya.
Ujenzi wa Kituo cha Tiba na marekebisho ya Tabia kwa Vijana wanaoacha Dawa za kulevya hapo Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja chenye eneo la ukubwa wa Eka  Tatu kinajengwa na Kampuni ya Kizalendo ya Al – Hilal General Trading Cooperation Limited chini ya Mkandarasi Mbwana Bakari Juma kutoka Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati Zanzibar.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Monday, January 4, 2016

TUNAMPONGEZA JOHN POMBE MAGUFULI

Tunampongeza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Kwa ajili ya mapumziko ya jamii kama watanzania ni watu basi watu hao wana haki nyingi za kibinaadamu kama hii aloiona Mh John Pombe Magufuli nayo ni hii ya kupata mapunziko ya kupunga upepo kwenye mandhari nzuri tena tulivu yenye upepo wa bahari nayo ni sehemuu ya asilia ya tangu zamani ni ile ya coco beach ambayo ipo kwa miaka mingi kwa kupata mandhari mazuri kwa watanzania kwa vile katika kutojali jamii ya watusehemu hiyo iliuzwa kwa mpango ule ule wa uvamizi wa maeneo ya ufukwe kwa kujenga mahoteli lakini kwa kuliona hilo Raisi wetu  mpendwa alirudishe kwa wananchi eneo hilo kama eneo la wazi la beach kwa ajili ya watu mbalimbali ili kurudisha uhalisia wake kwa watu kama zamani kwenda kupunzika na kupata hewa mwanana kama tunavyojua mtu ni afya na afya bora vile  mtu kupata wasa wa kupunzika hususan siku za mapunziko kujipatia maeneo kama hayo kupumzika na familia zao kupunga upepo na kubadilishana mawazo baada ya kazi kama kauli mbiu yetu inavosema hapa kazi tu kuonekana ule msemo kazi na dawa au kazi na mapunziko hata ule mfumo wa kazi wa kimataifa kazi na mapunziko na mapunziko katika sehemu kama hizo ndio mpango mzima wa maisha ya ulimwengu kwa hivo tunakushukuru kwa kulirejesha eneo hilo Mh Raisi umejali haki za binaadamu kwa mujibu wa sheria bado Tanzania tunapenda kuongozwa na anaejali wananchi wako na sio kila pahala panauzwa tu na kufikia wananchi kukosa haki zao za msingi lakini hili ni fundisho hata kwa Zanzibar inoendelea kutoa maeneo yote ya ufukwe na kutokujali wananchi watapata wapi kupunzika katuika jamii hii ya kizanzibar ni lazima viongozi hawa wa Zanzibar walione hilo kwa misingi ile ile ya mtu ni afya mtu anahitaji kupata mandhari ya bahari kama mzanzibar alozungukwa na bahari ndio faida ya kisiwa kwa hivo iko haja ya kuweka eneo la wazi kwa ajili ya wananchi ili kuona na sisi tumo ndani ya ulimwengu wa visiwa na kuendana na sheria za kimataifa mataifa mingi ulimwenguni hutenga maeneo kwa ajili ya mapunziko mbalimbali ya wananchi wake mbalimbali wakiwemo walemavu watoto, vijana, wazee, kina mama wote hawa wamo katika jamii na ni miongoni mwa wananchi. Maeneo ya wazi ni lazima kwa misingi ya haki za binaadamu kwa mujibu wa sheria  


Chama cha TADEA
RASHID YUSSUF MCHENGA
Mwanasiasa mkongwe/Mwanaharakati
na Katibu mwenezi taifa Tadea

0773560243 / 0715560243

MIPANGO MIZURI ITALETA MAENDELEO

Iko haja ya kua na mipango mizuri ya kiuchumi ili kuipandisha nchi kiuchumi ili kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kama yalivo malengo makuu ya taifa.

Kwa misingi ileile ya matarajio ya kupanda kwa kiuchumi na sio kushuka kiuchumi kwa sababu taifa lolote lile linaposhuka kiuchumi linakua mzigo ulimwenguni kwa sababu lengo la mataifa yasonge mbele kiuchumi wewe unashuka utakua unarudisha nyuma na jitihada za mataifa na ndio unakua mzigo

Na ndio maana mataifa yote yamejipangia na malengo ya kupanda kiuchumi na ndio kuna sekta nyeti na ndio roho ya taifa kama vile mipango uchumi fedha ukiachana na hizo na zikifanya kazi vizuri yaani kitaalamu huna sababu ya kushuka kiuchumi kwa maana nchi ni mipango mizuri inotokelezea kwa ufanisi zaidi na ndio maana kuna wataalamu wa mipango na nchi zote duniani  zilizopata maendeleo makubwa ya kiuchumi walikuwa na wataalamu wa mipango wa ndani na nje kwa kumaanisha  kama wataalamu wako wa ndani wepesi basi unaweza kuchukua wataalamu wanje na wa kimataifa waka tengeneza mpango mizuri ya nchi ilimradi upande kiuchumi li uwe mzigo katika ulimwengu wa kiuchumi kwa hivo wataalamu wan je na ndani wanaweza kushirikiana na kuinua uchumi na ndio sera ya kiuchumi mataifa ya duniani nchi nyingi ulimwenguni zimepanda kiuchumi na hata kufikia kuitwa 8 na wengine kuonekana wafalme wa kiuchumi na wengine kufikia uchumi wa kati wote hawa walifata sera ya uchumi wa kitaifa na kimataifa kwa kua na wataalamu wa mipango fedha na uchumi na kufikia malengo makuu walojipangia katika mataifa yao kwa kujua ni maendeleo na maendeleo ni mipamgo mizuri inoendana na wakati kwa mfano ulimwenguni kwa sasa kuna nchi kama Brazil,Africa ya Kaskazini na Uturuki uchumi wao unakwenda kwa kasi na ulimwengu unaliona na unalifahamu hilo na kwa hivo hata Tanzania na Zanzibar watakapokua wamefikia uchumi wa kati ulimwengu utasema kua sasa Tanzania ikiwemo na Zanzibar tunayo kila sababu ya kupanda kiuchumi kwa kutumia rasilimli watu na tulionazo ndani na kutumia wataalamu wa ndani na nje kwa hivo tutafikia malengo makuu ya kufikia uchumi wa kati na kati ifikapo 2025 kwa kutambua amani na utulivu sambamba na uzalendo kua  ni misingi mikuu ya kuleta  maendeleo na kulinda maendele kwa kuelewa maendeleo ingekua bustani basi maji yake ni amani na utulivu bila ya amani hakuna maendeleo

Kwa hivo watanzania uzalendo mbele na amani na utulivu iwe sera yetu iwe tunu ya taifa letu ili viongozi wetu hawa tuwadai maendeleo ya kiuchumi na kisiasa. Na kama tutadumisha suala la amani hilo la kuleta maendeleo lina wezekana kwa sababu Dr John Pombe Magufuli imeonesha nia ya dhati ya kutaka kuleta maendeleo ya kweli na ulimwengu unalifahamu hilo na sisi mashuhuda kwajitihada zote viongozi wetu hawa kama majuzi Raisi wa Zanzibar ilikagua eneo la bandari huru ya mpiga duru Zanziabr alisema wazi sasa tufanye kazi na hatuta muonea haya mtu yoyote mzembe fisadi na mbadilfu wa mali za serekali na sasa tunafungu ukurasa mpya tutapambana nao na kwa hili alilosema Dr Shein Rais wa Zanzibar mwenyekiti wa baraza la mapinduzi limeleta matumaini mapya visiwani

Kwa hivo tunaziomba serekali zote mbili kuleta maendeleo ya kweli ya kiuchumi ili kufikia uchumi wa kati kwa wakati tulojipangia suala vipi tutafikia malengo ni lazima yote na yote lazima tuwe na wataalamu wanje na wandani wataalamu wa fedha uchumi mipango kwa kufahamu nchi ni mipango mizuri ya uhakika ndio pekee inaweza kuinua nchi kiuchumi na kupata maendeleo ya kiuchumi na kisiasa, kijamii, kimataifa na hata mtu kwa mtu yaani kuondosha kaya masikini.

Kwa hivo inawezekana tukiondosha uzembe, ufisadi, rushwa, ubadhirifu  wa mali za serekali, ujangili nk tutafikia malengo makuu ya taifa na kufikia uchumi wakati na kupunguza kaya masikini
Chama cha TADEA
RASHID YUSSUF MCHENGA
Mwanasiasa mkongwe/Mwanaharakati
na Katibu mwenezi taifa Tadea
0773560243 / 071556024

Tudumisheni upendo wa Tanzania

MASHAMBA YA MIWA MAHONDA YATIWA MOTO.


 Baadhi ya Miwa iliyoteketea kwa moto kutokana na hujuma iliyofanywa  na Watu wasiojuilikana huko kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa Pole Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda  Bwana Tushar Mehta kufuatia watu wasiojuilikana kutia tena moto mashamba ya Miwa Mahonda.
 Balozi Seif kati kati  akifuatana na Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda akikagua baadhi ya sehemu ya shamba la Miwa la Eka 50 lililotiwa moto jana jioni na watu wasiojuilikana.

Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa.

Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda  Bwana Tushar Mehta akimueleza Balozi Seif hasara iliyopatikana kutokana na hujuma ya moto kwenye mashamba ya Miwa Mahonda.
Balozi Seif akielezea masikitiko yake kutokana na baadhi ya watu kufanya hujuma za makusudi kujaribu kuvuruga juhudi za Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda za kuimarisha  Sekta ya Viwanda.

Tishio la ajira za Wafanyakazi 350 wa Kiwanda cha Sukari Mahonda zinaendelea kuwa hatarini kufuatia hujuma zinazofanywa kwa makusudi na baadhi ya watu kuendelea kutia moto mashamba ya miwa huko Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kitendo hicho cha hujuma kinaweza kuusababisha Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda  kuwa na mawazo ya kufikiria kuzuia ajira mpya 450 za Wafanyakazi wa Kiwanda hicho katika malengo yake baada ya kukamilika kwa matengenezo makubwa na kuanza tena uzalishaji wa sukari.
Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda  Bwana Tushar Mehta alisema hayo wakati akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kuangalia hasara iliyosababishwa na moto uliotiwa kwa mara nyengine tena na Watu wasiojuilikana  ndani ya shamba la Miwa katika kipindi cha siku Tano baada ya tukio kama hilo la Tarehe 30 mwezi uliopita.
Bwana Tushar alisema moto huo umetiwa kati kati ya shamba la Miwa  jana jioni na wahalifu wenye  dhamira ya makusudi ya kutoa usumbufu na kizuizi kwa wananchi na vikosi vya Ulinzi katika harakati za kukabiliana na moto huo. .
Alisema Eka zipatazo 50 za Miwa iliyopevuka imeteketea kwa moto hali ambayo imeisababishia Kiwanda hicho hasara ya Tani 200 za Sukari na Lita 2,300 za Spititi zilizokuwa zizalishwe kutokana na miwa hiyo ikiwa na hasara  ya jumla ya dola za Kimarekani Laki 228,758.56 sawa na zaidi ya shilingi Milioni 494 za Kitanzania.
Meneja huyo wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda  alifahamisha kwamba hadi sasa Eka zipatazo 200 zimeteketea  kwa moto kwenye  matukio yote mawili     katika kipindi cha siku Tano zilizopita na kusababisha hasara ya jumla ya Dola za Kimarekani  Milioni 1,176,234.28  sawa na shilingi za Kitanzania  Bilioni 2,326,818,500/-.
Akiupa pole Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kutokana na hasara  ya Mashamba  iliyosababishwa na moto  huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hujuma hiyo ya makusudi haiitakii neema Zanzibar katika harakati zake za kustawisha uchumi wake.
Balozi Seif aliwanasihi watu wenye tabia hiyo kuachana nayo kwani mbali ya kujibebesha dhambi lakini pia inawavunja moyo wawekezaji walioamua kuja kuwekeza miradi yao ya kiuchumi  Nchini kwa lengo la kuisaidia Serikali pamoja na Wananachi hapa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba juhudi za makusudi za Serikali kuu katika kukifufua tena Kiwanda cha Sukari  na Manukato Mahonda baada ya kusita kwa miaka kadhaa zililenga kuimarisha  Uchumi kupitia sekta ya viwanda sambamba na kupanua  soko la ajira kwa Vijana.
Alisema tabia ya baadhi ya watu kufikiria kwamba hujuma hiyo itatoa fursa kwao kutumia maeneo ya mashamba ya Miwa kuendeleza Kilimo na Mifugo inafaa kuachwa mara moja kwa vile mashamba hayo yataendelea kuwa katika mipango ya  Serikali ya kuhudumia  Sekta ya Viwanda.
“ Haya ni Mashamba ya Serikali yaliyotengwa maalum kwa shughuli za harakati za Viwanda. Hivyo ndoto za baadhi ya Watu kufikiria kwamba  hujuma zao zitazaa matunda kwa kufanya wanavyotaka zinapaswa ziachwe mara moja ”. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliufahaisha Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kwamba Serikali Kuu inaangalia mpango utakaowezesha Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusaidia ulinzi kwenye Mashamba hayo ili kulinda hujuma zinazoonekana kushamiri siku hadi siku.
Hilo ni tukio la sita la hujuma za moto kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda  tokea kianze tena uzalishaji wa sukari na Spiriti mapema mwaka uliopita wa 2015.


Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

wana ccm watakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa marejeo

Ally Ndota, Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai amewataka wanachama wa Chama hicho kujiandaa na hatimaye kujitokeza kwa wingi katika Uchaguzi  wa marudio, ili kukiletea ushindi wa kishindo chama hicho.
Aidha, amesisitiza haja kwa wanachama wote popote walipo kujitokeza kwa wingi katika kufanikisha maadhimisho ya sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika Januari 12, mwaka huu, Mjini Unguja.
Ndugu Vuai ameyasema hayo leo hapo Afisi Kuu ya CCM alipokuwa akizungumza katika kikao maalum na Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar kilichojumuisha pia na Makatibu wa CCM wa Mikoa ya Unguja.
Amesema Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kinawataka viongozi, wanachama wa CCM na Jumuiya zake kujipanga kikamilifu na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio na kuwachagua kuanzania Rais, Wajumbe wa baraza la Wawakilishi na Madiwani wakati utakapowadia.
Ametoa wito kwa wana CCM na wananchi wapenda amani na utulivu kuachana na propaganda potofu zinazoenezwa mitaani siku hadi siku na wapinzani zenye lengo la kuwagombanisha viongozi na wafuasi wa CCM na badala yake hawana budi kujishughulisha na mambo ya msingi kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla.
Ameyataja mambo hayo ya msingi kuwa kwanza ni kujiandaa na hatimaye kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa marudio mara baada ya kupangwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na pili kushiriki katika maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964.
Chama Cha Mapinduzi ni Chama imara, chenye heshima na kinachotambulika na kuheshimika ndani na nje ya Tanzania, hivyo wanachama wake katu hawatakubali kupokea propaganda potofu zinazopandikizwa na wapinzania kwa ajili ya kutaka kudhoofisha nguvu ya Chama hicho.

Akizungumzia kuhusu suala la CUF kutoshiriki katika sherehe za mwaka Mapinduzi  za mwaka huu kama ilivyodaiwa na Chama hicho hivi karibuni, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar alisema kitendo hicho si jambo la ajabu miongoni mwa Jamii  ya Wazanzibari, kwani kwa vipindi tofauti  kadhaa huko nyuma  wamekuwa wakisusia sherehe hizo.

“Miaka  mingi huko nyuma kabla ya kuundwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa (SUK) Viongozi na wafuasi wa Chama hicho (CUF) walikuwa na kawaida sio tu ya kutoshiriki katika sherehe hizo, bali pia waliweza kususia hata vikao halali vya Baraza la Wawakilishi”. Alidai Naibu Katibu Mkuu huyo.

Amesema CUF kwa muda wote tangu kuasisiwa kwake, kimekuwa na kigugumizi kikubwa katika kuyatambua na kuyathamini Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoleta ukombozi wa kweli kwa wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba hali inayowafanya kuishi wakiwa watu huru ndani ya Taifa lao huru na kufaidika na matunda yatokanayo na Mapinduzi hayo.

Mara kadhaa wana CUF hasa viongozi waliomo ndani ya Serikali walidiriki kuwasilisha mawazo yao ya kutaka neno SMZ liondoshwe na lisitumike kabisa katika Serikali ya Zanzibar  mawazo ambayo yaligonga mwamba, hali inayodhihirisha kuwa CUF haitambui sembese kuthamini sherehe hizo na kinachofanyika sasa ni visingizio tu.

Jambo la msingi kwa jamii ya Wazanzibari ni vyema wakaelewa kwamba ndani ya mioyo ya Wana CUF hawayatambui kabisa Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 na mara kadhaa Viongozi wake wamekuwa wakisisika hadharani kupitia majukwaa ya kisiasa wakitaka Zanzibar iwe na Kumbukumbu za Uhuru bandia wa mwaka 1963.

Kwa mantiki hiyo basi, CCM kinawaomba wana CCM na wale wote ambao ni waumini wa kweli wa Mapinduzi ya Januari 12, 1964 popote walipo nchini, wajitokeze kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika sherehe za maadhimisho ya kutimia miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar huku wakiwaambia  wana CUF kwamba “wasitafute visingizio kwani hawana chembe ya Imani na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya 1964 na kwamba kushiriki ama kutoshiriki kwao hakuathiri chochote sherehe hizo”.

Sunday, January 3, 2016

Makatibu wakuu wapya wakatende kama walivyoapa

Rais Magufuli, wiki iliyopita alifanya uteuzi wa Makatibu Wakuu wa Wizara za serikali ya awamu ya tano na akawaapisha na pia kuwasainisha Hati ya Maadili na Utumishi wa Umma, nao wakaahidi kwenda katika wizara walizopangiwa na kufanya kazi kulingana na kasi ya Serikali mpya.

Hafla ya kuapishwa makatibu wakuu 26 iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikulu jijini Dar es Salaam, ilikuwa ya aina yake kutokana na kuapa mara mbili, huku Rais Magufuli akiwaeleza kuwa asiyeweza kazi aseme waziwazi ili asiape, akae kando.

Walikula kiapo cha kwanza mbele ya Rais Magufuli na kiapo cha pili cha maadili ya viongozi wa umma kiliwahusisha makatibu wakuu pamoja na naibu makatibu wakuu 24, na kufanya idadi ya walioteuliwa na Rais Desemba 30 mwaka jana kuwa 50.

Kiapo cha pili walisaini hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, inayotolewa na ofisi ya Rais, Sekretariet ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kiapo hicho ni cha kuahidi kutofanya mambo mbalimbali kama kutotumia cheo kwa maslahi binafsi, kulinda rasilimali za nchi, kutotoa wala kupokea rushwa, kutotoa siri za serikali na kuwa wazalendo.

Makatibu Wakuu ndio watendaji wakuu wa wizara, wamepewa madaraka makubwa ya kuhakikisha kuwa sera za wizara husika zinatekelezwa kwa ufanisi chini ya usimamizi wao, na ndio maana wakati wanaapa kiapo cha pili, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliwataka viongozi watendaji wakuu hao wafanye kazi zao kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu kwa maslahi ya nchi.

Tunaamini kuwa Makatibu Wakuu hao, wanajua namna kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano ilivyo, wanafahamu pia Serikali ina mifumo ya karibu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango iliyotolewa, ni dhahiri kuwa wao watakuwa chachu ya kusukuma uwajibikaji kwa wote walio chini ya mamlaka yao.

Kero kubwa za wananchi zimekuwa kukithiri kwa rushwa hasa katika sekta za umma, ambako sehemu kubwa ya huduma ilikuwa ikinunuliwa, watendaji wengi waliamini kuwa bila rushwa kutolewa, huduma ilikuwa ngumu kupatikana, na hasa katika sekta za mahakama, polisi, afya nk.

Baada ya kuapishwa kwa Makatibu Wakuu, WAziri Mkuu aliwaasa na kusema "Serikali imeamua kudhibiti utendaji katika sekta mbalimbali, utendaji unaotakiwa ni ule wa wazi, uadilifu, uaminifu ambao utatoa matokeo tarajiwa kwa wananchi".

Ni kweli kuwa wananchi wengi wameonyesha kuwa na imani na Serikali hii ya Rais Magufuli, na dhamira ya Rais  ni kuweka uongozi unaowajibika, uwe karibu zaidi kwa wananchi, ili huduma muhimu ambao zimekuwa tatizo kwao kwa muda mrefu zipatikane bila urasimu.

Baadhi ya Makatibu Wakuu waliovuta hisia za wanataaluma, walikuwa Meja Jenerali Gaudence Milanzi aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, yeye aliahidi kupambana kwa nguvu zote na tatizo la ujangiri wa wanyama pori nchini, pia Jaji Meja Jenerali Rwegasira wa Wizara ya Mambo ya Ndani aliahidi kupambana na mtandao wa dawa za kulevya nchini ambao alisema kwa muda mrefu umekuwa tishio.

Tunaamini Makatibu Wakuu wote watatekeleza majukumu yao kama walivyoapa, ni wazi kwamba Rais amewateua kwa kuzingatia viwango vya uwajibikaji wao, na kwa hakika atakuwa amejiridhisha kwa ufanisi unaotarajiwa kutoka kwao.

Ni wakati muafaka sasa kwa Serikali kutekeleza yale ambayo yanahusu nafasi za Makatibu Wakuu, kwani hao ndio kiungo kikubwa kwa wananchi, tunaamini sehemu kubwa ya kero ambazo zimewakwaza wananchi kwa kipindi kirefu sasa zitapata ufumbuzi unaostahiki.
chanzo nipashe

dokta shein ahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye sherehe za mapinduzi


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa wananchi wa Unguja na Pemba kujitokeza kwa wingi kusherehekea maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi yanayoanza jana.

Dk. Shein amesema wananchi wana kila sababu za kushiriki maadhimisho hayo kwa kuwa Mapinduzi ya tarehe 12 Januari, 1964 ndiyo yaliyoleta Uhuru kwa wananchi wa Unguja na Pemba kutoka kwa wakoloni.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki zoezi la kufanya usafi katika soko la matunda la Mombasa mjini Unguja leo, Dk. Shein alisema wananchi wanaelewa vyema historia ya Mapinduzi ya Zanzibar na kwamba wanajua wajibu wao katika kuyalinda na kuyadumisha.

Dk Shein alisisitiza kuwa “Kila mtu ana haki na wajibu wa kuyaenzi na kuyaendeleza Mapinduzi ya mwaka 1964” kwa kuwa ni dhahiri hakuna mwananchi asiethamini uhuru wake.

Rais wa Zanzibar aliwaeleza waandishi wa habari na wananchi waliohudhuria zoezi hilo kuwa Mapinduzi ya mwaka 1964 yameleta maendeleo kwa kila mwananchi na kwamba hakuna mwananchi asiyefaidika na matunda ya Mapinduzi.

Dk. Shein alisema Mapinduzi ya mwaka 1964 yalifanyika kwa malengo maalum ya kuwakomboa wananchi Zanzibar kwa kuwa mazingira yaliyokuwepo wakati huo kitendo cha kufanya Mapinduzi kilikuwa hakiwezi kuepukika.

Alibainisha kuwa wapo wanaoyakumbuka kwa furaha na wengine wamenuna lakini Mapinduzi yalikuwa ni lazima na ndivyo ilivyofanyika na sasa Zanzibar iko huru.

Aliwataka wananchi kushiriki katika ratiba mbalimbali za maadhimisho hayo yakiwemo mashindano ya mpira wa miguu ya Kombe la Mapinduzi yanayoanza leo katika uwanja wa Amaan Zanzibar.

JUMUIYA YA KUKUSANYA ZAKA NA SADAKA ZANZIBAR (JUZASA) YAFANYA MKUTANO MKUU WAKE.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) akitoa maelezo ya Jumuiya na kumkaribisha mgeni rasmi (kushoto) Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla Talib kufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanziba
 Baadhi ya wanachama wa Jumuiya na wageni walikwa wakisikiliza nasaha za Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) hayupo pichani wakati wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo.
 Mgeni rasmin Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla Talib akifungua Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar uliofanyika katika ukumbi Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.
 Shekh. Ahmad Haydar Jabir akikumbusha juu ya kutoa Zaka na Sadaka, na kutofautisha baina Sadaka na Zaka, amewataka waumini kusama kuyajua hayo.
 Mmoja wawalikwa Shekh Said Khalid Said akichangia katika Mkutano huo.
Mjumbe wa Bodi ya Jumuiya hiyo Dkt. Muh'd Hafidh akitoa neno la shukrani mara baada ya kumaliza kwa Mkutano. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Taasisi za kiislamu nchini zimeshauriwa kushawishi kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa Zaka na Sadaka ili ziweze kuleta tija katika kundi kubwa la jamii ya Kislam.
Katibu mtendaji wa kamisheni ya mufti namali ya amana Zanzibar sheikh abdalla talib amesema Lengo la mfumo huo uliwekwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu ni kusadia na kupunguza umasikini katika jamii lakini kwa sasa wengi wanaotaoa sadka hizo hazifikii lengo hilo kwa vile kumekosekana mfumo bora  unaowafikia watu wengi na kuleta mabadiliko makubwa.
Akifungua mkutano wa jumuiya ya zaka na sadaka Zanzibar ZASA ametolea mfano wan chi ya denmar amabyo ina waislamu kwa asilimi 3 tu imekuw ana utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa sadka na zaka  hali iliyofanikisha kupatikana  misaada mingi iliyosaidia  katika nchi hiyo na hata nchi nyengine.
Amefahamisha kuwa  kwa kuwa  Zanzibar asilimia kubwa ya wanananchi wake ni waislamu ina nafasi ya kufikia malengo hayo kama pia itatoa elimu kwa wananchi hasa wenye uwezo  ili kufahamu  umuhimu wa Ibada hiyo pamoja na njia bora za kutoa zaka na sadaka katika jamii.
Nae mwenyekii wa jumuiy hiyo sheikh said masoud  amesema kwa sasa umekuwa na mwamko mdogo hasa kwa wafanyabiashara kutoa zaka na sadaka  kulingana na taratibu zinazotakiwa  kidini.
Nae katibu wa jumuiya hiyo ya jusaza omar abubakar Mohamed amesema jumuiya hiyo  imeshatoa zaka kwa watu 46 zikiwemo za fedha taslim, charahani, friza na wengine kujengewa nyumba.

Saturday, January 2, 2016

SHEREHE ZA MAPINDUZI ZIPO KAMA KAWAIDA ASEMA MAKAMU WA PILI WA RAIS

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Maadhimisho ya Sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964  yatafanyika kama kawaida na kupangwa kuanza rasmi jumapili ya Tarehe 3 Januri 2016.
Alisema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba katika muda wote wa maandamisho hayo kunakuwa na hali ya utulivu na usalama mkubwa katika maeneo yote ya Visiwa vya vya Unguja na Pemba.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar alisema hayo wakati akitoa Taarifa rasmi ya ratiba ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar mbele ya Wana Habari hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema suala la upande wa Upinzani kuzisusia sherehe za Mapinduzi   kwa kisingizio cha Rais aliyepo madarakani si halali ni muendelezo wa kuwapotosha Wananchi walio wengi nchini.
Balozi Seif alifafanua kuwa Rais wa sasa Dr. Ali Mohammed Shein ataendelea kuwa rais hadi yule atakayechaguliwa rasmi na kihalali na Wananchi ale kiapo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar  ya mwaka 1984 kama ilivyokwishatolewa ufafanuzi na wanasheria walio wengi.
Alisema tukio hili la maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52 ni jambo la kujivunia kwa kila Mwananchi  wa Visiwa vya Unguja na Pemba mpenda maendeleo na anayeifahamu vyema Historia ya Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi.
Alieleza kwamba ipo miradi mingi na tofauti ya Wananchi ambayo Viongozi na hata baadhi ya  wanachama wa upande wa upinzani walishiriki kuibuni sasa inakuaje miradi hiyo waiachie wakati tayari imeshalengwa kuinufaisha jamii iliyowazunguuka.
“ Tuna kila sababu na ni haki yetu kusherehekea siku hii adhimu katika Maisha yetu. Hivyo tuambizane, tushajiishane na tushiriki katika matukio mbali mbali ya maadhimisho ya sherehe hizi kuanzia mwanzo hadi mwisho “. Alisema Balozi Seif.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  alieleza kwamba Miradi yote ya Maendeleo ipatayo 24 ambapo 16 ikiwa imekamilika na Minane inatarajiwa kuwekwa mawe ya msingi imehusishwa katika maadhimisho hayo itakayoanza Jumatatu ijayo.
Alisema madhimisho hayo yataanza rasmi kesho Jumapili  ikiwa ni siku maalum kwa kazi za usafishaji wa masingira katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba ukilenga zaidi katika sehemu za kutolea huduma za kijamii kama Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na  masoko.
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar alifahamisha kwamba ingawa zoezi hilo hufanyika kila zinaponza sherehe za Mapinduzi lakini mwaka huu juhudi malum zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa katika hali ya usafi muda wote.
Alikumbusha kuwa hivi sasa Taifa linakabiliwa na tatizo la kuwepo kwa maradhi ya Kipindupindu, hivyo jamii  ina wajibu wa kutumia fursa hizi za maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi kwa kuchukuwa hatua za kujikinga na kupambana na maradhi hayo ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na mazingira machafu ya sehemu zinazotumika na jamii katika shughuli za kila siku.
Alisema kwa vile suala la usafi wa mazingira ni la lazima Viongozi Wakuu wa Kitaifa watahakikisha  wanaungana na Wananchi katika zoezi hilo kwenye maeneo watakayopangiwa.
Alieleza kwamba utaratibu maalum umeshaandaliwa kwa kila mamlaka za Mikoa, Wilaya, Baraza la Manispaa, Mabaraza ya Miji na Halmashauri za Wilaya katika kuratibu mfumo mzima wa kufanikisha zoezi hilo la usafi wa mazingira.  
Akigusia suala la hatma ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar  ambalo limekuwa agenda kubwa kwa baadhi ya watu wakiwemo hata wanasiasa nchini wakiendelea kupotosha Wananchi  Balozi Seif alisema Taarifa rasmi ya vikao vinavyowakutanisha Viongozi wa juu kulijadili suala hilo itatolewa rasmi mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo.
Hata hivyo Balozi Seif alitanabahisha kwamba  Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar         {  ZEC } kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar  ya mwaka 1984 ndio yenye mamlaka ya kuendesha na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Alisema kwa vile tume hiyo kupitia Mwenyekiti wake  haikuridhika na mazingira yaliyojichomoza wakati wa zoezi la kupiga kura na kulazimika kufuta Uchaguzi pamoja na matokeo yake yote Taasisi hiyo hiyo ndio yenye uwezo wa kuitisha uchaguzi mwengine kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.
Akijibu baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari Balozi Seif alisema katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 iko wazi na kutoa mamlaka kwa tume ya uchaguzi ya Zanzibar kupanga uchaguzi mwengine kufuatia kufutwa kwa ule wa mwezi oktoba mwaka 2015.
“ Kinachosubiriwa kwa sasa ni Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kutangaza Tarehe ya uchaguzi mwengine ambapo kujumu la kugharamia uchaguzi huo limo ndani ya mamlaka ya Serikali Kuu yenyewe “. Alisema Balozi Seif.
Kuhusu Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambao baadhi ya watu wamekuwa wakitoa tafsiri potofu, Balozi Seif aliwajibu wanahabari hao kwamba  Baraza la Wawakilishi lilivunjwa lakini Rais wa Zanzibar  bado anayo Mamlaka  ya kuliitisha iwapo kuna suala muhimu la Kitaifa.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Friday, January 1, 2016

MFAHAMU HILMY MTOTO MWENYE ULEMAVU ALOANZISHA TAASISI YA KUSAIDIA WALEMAVU WENZAKE


Na Hafidh Hussein, Zanzibar.
                MAISHA ya Mwanadamu yeyote katika sayari hii ya Dunia yametawaliwa na mambo mengi ambayo kimantiki uonekana kama furaha ama uzuni, ambayo yote hayo katika falsafa za kiimani uitwa mitihani inayotokana na majaaliwa ya Mola kwa wanadamu na viumbe vingine.
Kilichonisukuma kuandika makala haya ni kutokana na kuguswa na maisha halisi aliyepitia kijana mmoja mwenye historia ya kusisimua anayeitwa  Hilmy Faria Shawali tangu anazaliwa mpaka sasa kwa ufupi naweza kueleza kuwa kimtizamo ni masahibu na mitihani.
Lakini pia naweza kunasibisha msemo maarufu unaotumiwa na wazee wetu ama watu wazima wakati wanapokuwa wakitoa usia kwa vijana wao kwamba “Kama hujafa ujaumbika” msemo huu umekuwa na maana pana sana juu ya maisha ya mwanadamu ya kila siku kwani kila mmoja Mwenyezi mungu anampa mtihani wake katika hii dunia.
Kijana huyo ambaye ni Hilmy Faria Shawali ni mtoto wa kwanza katika Familia ya mzee Faria Shawali amezaliwa Septemba 29, mwaka wa 1996 katika hospitali ya  Chelsie Westminister katikati ya mji wa London nchini Uingereza.
Hilmy katika kipindi cha miaka 19 aliyonayo amepitia masahibu mengi mpaka kufikia alipo sasa na laiti kama sio ujasiri wa baba yake mzazi leo nisingeandika Makala hii.
Kama ilivyo kawaida ya nchi za wenzetu hasa za Magharibi zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kufuatilia makuzi ya mtoto toka akiwa tumboni kwa mama yake, kutokana na ukuwaji wa Teknolojia ya sayansi na vifaa vya kisasa katika Hospitali zao, hivyo wakati wa ujauzito wa miezi minne tayari Hilmy alishajulikana atakuwa ni mtoto wa namna gani.
Kutokana na maumbile yake Jopo la wataalamu wakiwemo wakunga na Matatibu wakashauri familia ya mimba ya Hilmy itolewe maana mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye ulemavu wa viungo.
Ushauri wa kutolewa mimba hiyo ni kutokana na Imani na tamaduni za wazungu walioamini kuwa motto huyo akizaliwa  anakuja kuwatesa na kuwasumbua wazazi wake lakini kutokana na Imani ya dini aliyokuwa nayo Baba yake Hilmy,  alikataa  ushauri huo na kutaka mtoto huyo azaliwe licha ya madaktari kumsihi mara kwa mara afuate ushauri wao.
Mzee Faria alianza kutawaliwa na  hofu kutokana na  Madaktari kumsumbua mara kwa mara akubali kutoa  mimba ya mkewe, hali iliyopelekea kwenda mara kwa mara katika hospitali aliyopangiwa mkewe Klinic licha ya kuwa mbali na sehemu aliyokuwa akiishi, lakini ilimlazimu kutumia usafiri wa (Public Transport).
Kutokana na Mzee huyo kuwa ni mgeni katika nchi hiyo ilibidi kuacha kazi kwa ajili ya kufuatilia kwa ukaribu hali ya mke wake ndipo baba yake akakutana na daktari mmoja kutoka kenya akamwambia kuwa yeye ni muislamu hawezi kukubali mimba ya mke wake itolewe.
“ Wewe unajua mimi ni muislam sitoweka kukubali mimba itolewe kwa misingi ya dini yangu, na isitoshe eti kutokana na kuwa kiumbe kilichokuwa ndani ya tumbo la mke wangu kina ulemavu”, alisisitiza Faria na kuendelea kuweka wazi msimamo wake huo kuwa ni lazima mtoto huyo azaliwe hali iliyopelekea Madaktari kumuunga mkono huku wakimwambia kuwa mtoto huyo akizaliwa kupona ni bahati.
Wakati wa kujifungua ulifika na ikabidi Mama yake Hilmy awe china ya uangalizi wa madaktari kwa lengo na kukabiliana na lolote linaloweza kutokea.
Jopo la Madaktari walifanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya Mama na mtoto kutoka lipozaliwa usiku wake alifanyiwa upasuaji (Operesheni) kubwa ambayo hata madaktari hawakutegemea kupona kwa mtoto huyo.
Upasuaji huo kitaalamu unaitwa  Spinali Bifida na kulazimika kukaa, Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU) kwa muda wa wiki mbili mara baada ya upasuaji  huo, alilazimika kufanyiwa upasuaji nyingine mkubwa wa kichwa ambayo ulijulikana kama Unshunt nayo madaktari walikuwa na nusu kwa nusu kunusuru maisha ya Hilmy, lakini kwa uwezo wa mola madaktari walipatwa na mshangao maana Hilmi alipona.
Akiendelea na matibabu yake Hilmy alikuwa akiishi katika maisha ya kufanyiwa matibabu kwa njia ya upasuaji ambapo mpaka sasa inasadikika tayari ameshafanyiwa upasuaji  50, kati ya hizo 13 zilikuwa za za kawaida, licha ya huzuni na majonzi kwa upande wa Mama yake Hilmy  lakini Baba mzazi wa kijana huyo, alisimama  kidete kwa kumliwaza na kumfariji mkewe kwa kuamini hiyo yote ni mipango ya mwenyezi mungu.
Maisha ya Hilmy yaliendelea chini ya uangalifu na umakinifu  wa wazazi wake na kujitahidi kumkuza mtoto wao katika hali ya kumfariji ili ajihisi yeye ni sawa na watoto wengine alipofikisha umri wa kwenda shule naye alipelekwa shule na wazazi wake ili kujiunga na watoto wenzake.
Hilmy alisoma katika shule za kawaida shule ya John Chilton walimu wa shule aliyosoma hawakumuacha mkono Hilmy  walimpa uangalizi wa hali ya juu kutokana na hali yake ya ulemavu aliyonayo na alisoma hapo mpaka alipo maliza kidato cha sita na mwaka huu wa 2015 Hilmy yupo Chuo Kikuu anasomea uandishi wa Habari za Michezo (Sport Journalism) .
Katika kusoma kwake Kijana huyo elimu ya Chuo kikuu anakabiliwa na changamoto kubwa ya umbali wa kutoka anapoishi mpaka kufika chuo maana anakaa Mji wa London Middlesex kitongoji cha Han Well anasoma katika university ya Hendon Middlesex.
Kama ilivyo kawaida kwa raia wa Zanzibar waishio nje ya nchi yao hutenga muda maalum kwa watoto wao aidha kila mwisho wa mwaka shule zinapofungwa au kila baada ya muda Fulani kuwaleta watoto wao katika nchi zao za asili walizozaliwa ili kujifunza lugha zao za asili yaani lugha mama au kuja kuzijulia hali familia zao kwa lengo la watoto kufahamu familia za wazazi wao.
Baada ya kutembelea familia zao zilizopo Zanzibar Hilmy aligundua  kitu cha ziada ambacho hata madaktari waliokuwa wakimuhudumia mama yake kipindi cha ujauzito wake walishindwa kugundua kitu gani kilifichikana katika mimba ile na vipi kitaleta faraja kwa walemavu wote wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Mnamo mwaka 2013 akitokea katika jiji la London  kuja Zanzibar katika safari za kawaida kutembelea nchi ya wazazi wake hapo Hilmy akiwa na miaka kumi na saba alipofika alipata fursa ya kutembelea maeneo tofauti ya mji wa Unguja katika pita pita zake zake alikutana na watu tofauti bila ya mtu yeyote kujua nini Hilmy anafikiria na athari gani anaipata akiwa katika kigari chake cha kutembelea (Will Chair).
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Hilmy alipokuwa akitembea katika maeneo mbali mbali, alikutana na Watu wenye maumbile kama yake yaani watu wenye ulemavu wanaohitaji misaada maalum kutokana na uhalisia wa maumbile yao.
Watu hao walimgusa kwa kiasi kikubwa kijana Halmy na muda wake mwingi kuzingatia ni kwa kiasi gani anaweza kuwasaidia ni watu wenye hali kama yake ambao ni walemavu maana aliguswa na hali zao na jinsi wanavyokosa mahitaji muhimu wengine wanasota hata nyenzo za kutumia kutoka sehemu moja au nyingine hawana.
Baada ya muda wa likizo kuisha na kurudi uingereza ndipo alipomwita Baba yake mzazi na kumuelezea dhamira na lengo lake la kuanzisha Jumuiya ambayo itamuwezesha kuwasadia watu wenye ulemavu wanaoishi Zanzibar.
Baada ya kijana huyo kuzungumza yaliyokuwepo moyoni na kueleza kinaga ubaga hali halisi ya watu wenye ulemavu wanaoishi Zanzibar, Baba yake alipoteza ujasiri na kuenda kukaa pembeni na kuanza kutokwa na machozi kwa kuona mwanawe amafikiria jambo kubwa ambalo hata yeye hakuwahi kulifikiria licha ya mara kwa mara alikuwa anakuja nyumbani kwao Zanzibar.
Baba Mzazi wa kijana huyo alifikria mengi na hata kuwaza kuwa alipokuwa anakuja Zanzibar alikuwa akikutana na Watu wenye ulemavu ambapo aliweza kumsaidia mtu mmoja mmoja na kwa vitu ambavyo haviwezi kukidhi mahitaji yao yote ya msingi lakini hakuwahi kuwaza kuanzisha jumiya (charity).
Malengo ya Hilmy juu ya Watu wenye ulemavu wa Zanzibar ni mengi jambo ambalo mwandishi wa Makala hii alipopata fursa ya kukaa na Hilmy na kuzungumzia masuala mbali mbali alimwambia mambo mengi anayopanga kuyafanya juu ya maendeleo ya watu wenye ulemavu.

Miongoni mwa mambo ya msingi aliyoyapa kipaumbele katika mipango yake ni kuwa anatamani siku moja awe na uwezo wa kuwafikia watu wote wenye ulemavu ili aweze kuwapa mahitaji yao ya msingi ili waishi kama watu wengine.
“ Natamani siku moja niwe na uwezo wa kuwafikia watu wenye ulemavu wote wa Zanzibar ili niweze kuwapatia mahitaji yao yote ya msingi”
Bado nina imani kuwa Mwenyezi mungu atanijaalia kufikia malengo yangu, kwani nakuwa naumia sana ninapoona mtu mwenye ulemavu kama mimi anaishi katika hali ya kukata tama kutokana na kukosa huduma za msingi hata za kumuezesha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa usalama”,. alisema Hilmy huku akiwa na hisia za huruma na kuonyesha nia ya dhati ya kuwajali wao hao.
Katika juhudi za awali  kijana huyo amefanikiwa kuanzisha Taasisi yake kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye ulemavu Zanzibar inayojulikana kama “Hilmy Charity” ambayo ni jumuiya isiyokuwa ya kiserikali inayotambuliwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jumuiya hiyo imesajiliwa mwaka ………na kuanza kufanya kazi zake rasmi mwaka…. Ambayo ipo  chini ya mwamvuli wa jumuiya zisizo za kiserikali Zanzibar (Angoza) inayofanywa kazi za kuwasaidia watu wenye ulemavu nchini.
Hilmy Charity tayari wametoa msaada wa vigari( Will Chear) vya watu wenye ulemavu  220, ambavyo tayari vimetolewa katika maeneo mbali mbali ya mikoa ya Zanzibar, kwa upande wa Unguja 150 pamoja na Pemba vigari 70.
Licha ya ulemavu wa Hilmy anauthibitishia ulimwengu kuwa ulemavu sio kikwazo cha kufikia malengo ambapo mpaka sasa  anashiriki mashindano ya mbio za vigari ya mita 200 na 400 ya watu wenye ulemavu na tayari ameshiriki katika mashindano mbali mbali ikiwemo London youth ,Middlesex, Bedford na mengineyo mengi na ameshinda katika baadhi ya mashindano na kuchukua medani sita za dhahabu na mategemeo yake ni ifikapo mwaka 2020 kushiriki mashindano ya Olimpic ya Tokyo.
Kijana huyo Hilmy Faria Shawal ni  mtoto wa mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu katika timu ya Small Simba Zanzibar ambayeni ni Faria Shawal, pamoja na ulemavu wake haukumfanya wazazi wake wamfungie ndani na kumuona ni mkosi kwao bali walimpa fursa za kuishi kama watu wengine.
Kutokana na historia halisi ya Maisha ya Hlmy unaweza kuwa na maswali mengi ya kujiuliza ikiwemo kuwa je kama Baba yake angekubali Madaktari watoe mimba yake nyota yake ingeweza kung’ara kwa watu wengine, na je baada ya kuzaliwa laiti wazazi wake wangemfungia ndani na kumkosesha fursa ya kupata elimu angeweza kuwa msaada na mfano wa kuigwa kwa watu wengine, hivyo majawabu ya maswali hayo yapo vichwani mwa wasomaji wa makala hii huku tukikubaliana kuwa ulemavu kwa binadamu sio mkosi ama usumbufu kwa watu wengine bali ni majaaliwa ya mola.
Bado kijana huyo mwenye ulemavu anaishi kwa kujiamini na kutekeleza malengo yake kwa ufanisi, hivyo jamii ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuendelea kuunga mkono juhudi za kijana huyo kwa lengo la kujenga jamii shirikishi ya watu wenye ulemavu ili waweze kuishi kwa amani na utulivu kama walivyo watu wengine.
Jamii ni vyema kuanzia sasa kila mmoja akajihesabu kuwa ni Mtu mwenye ulemavu wa kesho hata kama leo anajihesabu kakamilika kwani sababu za ulemavu kwa asilimia kubwa zinatokana na asili ya maisha yetu ya kila siku zikiwemo ajali, maradhi ama kuzaliwa na ulemavu mambo ambayo kwa kiasi kikubwa hayana kinga ya moja kwa moja hivyo kila mmoja anaweza kuwa katika hali hiyo, hivyo tuungane kwa pamoja kulaani vikali vitendo vya udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu na kuwa mabalozi wema wa kuunga mkono juhudi za maendeleo za watu hao.

Katika mfululizo wa Makala za Maisha na Vipaji vya watu wenye ulemavu pia tukae tayari kupokea Makala nyingine  hivi karibuni  yenye kuelimisha na kusisimua ya Binti ambaye anaishi na ulemavu wa viungo vya macho aliyemaliza shahada yake ya sharia na kuwa msaada mkubwa kwa watu wenye ulemavu  Zanzibar.