Kwa ajili ya mapumziko ya jamii kama
watanzania ni watu basi watu hao wana haki nyingi za kibinaadamu kama hii
aloiona Mh John Pombe Magufuli nayo ni hii ya kupata mapunziko ya kupunga upepo
kwenye mandhari nzuri tena tulivu yenye upepo wa bahari nayo ni sehemuu ya
asilia ya tangu zamani ni ile ya coco beach ambayo ipo kwa miaka mingi kwa
kupata mandhari mazuri kwa watanzania kwa vile katika kutojali jamii ya watusehemu
hiyo iliuzwa kwa mpango ule ule wa uvamizi wa maeneo ya ufukwe kwa kujenga
mahoteli lakini kwa kuliona hilo Raisi wetu
mpendwa alirudishe kwa wananchi eneo hilo kama eneo la wazi la beach kwa
ajili ya watu mbalimbali ili kurudisha uhalisia wake kwa watu kama zamani
kwenda kupunzika na kupata hewa mwanana kama tunavyojua mtu ni afya na afya
bora vile mtu kupata wasa wa kupunzika
hususan siku za mapunziko kujipatia maeneo kama hayo kupumzika na familia zao
kupunga upepo na kubadilishana mawazo baada ya kazi kama kauli mbiu yetu
inavosema hapa kazi tu kuonekana ule msemo kazi na dawa au kazi na mapunziko
hata ule mfumo wa kazi wa kimataifa kazi na mapunziko na mapunziko katika
sehemu kama hizo ndio mpango mzima wa maisha ya ulimwengu kwa hivo tunakushukuru
kwa kulirejesha eneo hilo Mh Raisi umejali haki za binaadamu kwa mujibu wa
sheria bado Tanzania tunapenda kuongozwa na anaejali wananchi wako na sio kila
pahala panauzwa tu na kufikia wananchi kukosa haki zao za msingi lakini hili ni
fundisho hata kwa Zanzibar inoendelea kutoa maeneo yote ya ufukwe na kutokujali
wananchi watapata wapi kupunzika katuika jamii hii ya kizanzibar ni lazima
viongozi hawa wa Zanzibar walione hilo kwa misingi ile ile ya mtu ni afya mtu
anahitaji kupata mandhari ya bahari kama mzanzibar alozungukwa na bahari ndio
faida ya kisiwa kwa hivo iko haja ya kuweka eneo la wazi kwa ajili ya wananchi
ili kuona na sisi tumo ndani ya ulimwengu wa visiwa na kuendana na sheria za
kimataifa mataifa mingi ulimwenguni hutenga maeneo kwa ajili ya mapunziko
mbalimbali ya wananchi wake mbalimbali wakiwemo walemavu watoto, vijana, wazee,
kina mama wote hawa wamo katika jamii na ni miongoni mwa wananchi. Maeneo ya
wazi ni lazima kwa misingi ya haki za binaadamu kwa mujibu wa sheria
Chama cha TADEA
RASHID YUSSUF MCHENGA
Mwanasiasa mkongwe/Mwanaharakati
na Katibu mwenezi taifa Tadea
0773560243 / 0715560243
No comments:
Post a Comment