Iko haja ya kua
na mipango mizuri ya kiuchumi ili kuipandisha nchi kiuchumi ili kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025 kama yalivo malengo makuu ya taifa.
Kwa misingi
ileile ya matarajio ya kupanda kwa kiuchumi na sio kushuka kiuchumi kwa sababu
taifa lolote lile linaposhuka kiuchumi linakua mzigo ulimwenguni kwa sababu lengo
la mataifa yasonge mbele kiuchumi wewe unashuka utakua unarudisha nyuma na
jitihada za mataifa na ndio unakua mzigo
Na ndio maana
mataifa yote yamejipangia na malengo ya kupanda kiuchumi na ndio kuna sekta
nyeti na ndio roho ya taifa kama vile mipango uchumi fedha ukiachana na hizo na
zikifanya kazi vizuri yaani kitaalamu huna sababu ya kushuka kiuchumi kwa maana
nchi ni mipango mizuri inotokelezea kwa ufanisi zaidi na ndio maana kuna
wataalamu wa mipango na nchi zote duniani
zilizopata maendeleo makubwa ya kiuchumi walikuwa na wataalamu wa
mipango wa ndani na nje kwa kumaanisha
kama wataalamu wako wa ndani wepesi basi unaweza kuchukua wataalamu wanje
na wa kimataifa waka tengeneza mpango mizuri ya nchi ilimradi upande kiuchumi
li uwe mzigo katika ulimwengu wa kiuchumi kwa hivo wataalamu wan je na ndani
wanaweza kushirikiana na kuinua uchumi na ndio sera ya kiuchumi mataifa ya duniani
nchi nyingi ulimwenguni zimepanda kiuchumi na hata kufikia kuitwa 8 na wengine
kuonekana wafalme wa kiuchumi na wengine kufikia uchumi wa kati wote hawa
walifata sera ya uchumi wa kitaifa na kimataifa kwa kua na wataalamu wa mipango
fedha na uchumi na kufikia malengo makuu walojipangia katika mataifa yao kwa
kujua ni maendeleo na maendeleo ni mipamgo mizuri inoendana na wakati kwa mfano
ulimwenguni kwa sasa kuna nchi kama Brazil,Africa ya Kaskazini na Uturuki
uchumi wao unakwenda kwa kasi na ulimwengu unaliona na unalifahamu hilo na kwa
hivo hata Tanzania na Zanzibar watakapokua wamefikia uchumi wa kati ulimwengu
utasema kua sasa Tanzania ikiwemo na Zanzibar tunayo kila sababu ya kupanda
kiuchumi kwa kutumia rasilimli watu na tulionazo ndani na kutumia wataalamu wa
ndani na nje kwa hivo tutafikia malengo makuu ya kufikia uchumi wa kati na kati
ifikapo 2025 kwa kutambua amani na utulivu sambamba na uzalendo kua ni misingi mikuu ya kuleta maendeleo na kulinda maendele kwa kuelewa
maendeleo ingekua bustani basi maji yake ni amani na utulivu bila ya amani
hakuna maendeleo
Kwa hivo
watanzania uzalendo mbele na amani na utulivu iwe sera yetu iwe tunu ya taifa
letu ili viongozi wetu hawa tuwadai maendeleo ya kiuchumi na kisiasa. Na kama
tutadumisha suala la amani hilo la kuleta maendeleo lina wezekana kwa sababu Dr
John Pombe Magufuli imeonesha nia ya dhati ya kutaka kuleta maendeleo ya kweli
na ulimwengu unalifahamu hilo na sisi mashuhuda kwajitihada zote viongozi wetu
hawa kama majuzi Raisi wa Zanzibar ilikagua eneo la bandari huru ya mpiga duru
Zanziabr alisema wazi sasa tufanye kazi na hatuta muonea haya mtu yoyote mzembe
fisadi na mbadilfu wa mali za serekali na sasa tunafungu ukurasa mpya
tutapambana nao na kwa hili alilosema Dr Shein Rais wa Zanzibar mwenyekiti wa
baraza la mapinduzi limeleta matumaini mapya visiwani
Kwa hivo
tunaziomba serekali zote mbili kuleta maendeleo ya kweli ya kiuchumi ili
kufikia uchumi wa kati kwa wakati tulojipangia suala vipi tutafikia malengo ni
lazima yote na yote lazima tuwe na wataalamu wanje na wandani wataalamu wa
fedha uchumi mipango kwa kufahamu nchi ni mipango mizuri ya uhakika ndio pekee
inaweza kuinua nchi kiuchumi na kupata maendeleo ya kiuchumi na kisiasa,
kijamii, kimataifa na hata mtu kwa mtu yaani kuondosha kaya masikini.
Kwa hivo
inawezekana tukiondosha uzembe, ufisadi, rushwa, ubadhirifu wa mali za serekali, ujangili nk
tutafikia malengo makuu ya taifa na kufikia uchumi wakati na kupunguza kaya
masikini
Chama cha TADEA
RASHID YUSSUF MCHENGA
Mwanasiasa mkongwe/Mwanaharakati
na Katibu mwenezi taifa Tadea
0773560243 / 071556024
Tudumisheni upendo wa Tanzania
No comments:
Post a Comment