Na Khadija Khamis -Maelezo zanzibar
Waziri wa Fedha Mhe,Omar Yussuf Mzee amesema kuanzishwa kwa Jumuiya ya vijana wa paunia wa zamani (Young Peoneer Veterani Association ) kutasaidia vijana kujikwamua na umasikini pamoja na kujiepusha na madawa ya kulevya .
Alisema tunashuhudia vijana wengi wa Zanzibar wanaendelea kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo madawa ya kulevya na kupelekea mmong’onyoko wa maadili .
Hayo aliyasema leo huko katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo wakati alipokuwa akizindua Jumuiya mpya isiyokuwa ya kiserikali Young Peoneer Vererani Association yenye lengo la kuwasaidia vijana wa Zanzibar kimaendeleo.
Waziri Mzee amekemea tabia ya vijana kutokuwa na maadili na kujiingiza katika vikundi viovu jambo ambalo linapelekea kuhatarisha maisha na kwenda kinyume na silka na utamaduni wa Zanzibar .
“ Hii inaonesha utofauti mkubwa uliopo wa malezi heshima na tamaduni zilizokuwepo awali zimetoweka kwa kuvaa nguo zisizostahiki na kupenda maisha ya anasa wakati uwezo wao ni mdogo.”Alisema Waziri Omari.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa Jumuiya hiyo kuwa na ushirikiano wa pamoja ili wawe na uwadilivu katika kazi zao waepukane na tamaa.
Sambamba na hayo Waziri Omari alianzisha harambee ya papo kwa papo na kuweza kukusanya fedha ya zaidi ya Tshs millioni 3,834,500 za papo kwa papo na Tshs Millioni 5,850,000 za ahadi jumla shilling millioni 9,724,500 zilichangiwa Jumuiya hiyo .
Hata hivyo Waziri huyo aliahidi kutoa Komputa mpya moja na Printa mpya moja na pesa taslimu Tshs milioni moja na laki tano pamoja na Tshs milioni moja kwa ajili ya mchango wa mkewe ili kuweza kuisaidia jumuiya hiyo .
Nae Katibu wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii Vijana,Wanawake na Watoto Asha Ali Abdalla kwa niaba ya Waziri Uwezeshaji ,Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Zainabu Omar Muhammed alisema ushirikiano wa jumuiya utaleta mafanikio kwa vijana wa Zanzibar na Jumuiya wasisiste kuitumia wizara yake kwa matatizo mbali mbali ambayo yatayojitokeza.
No comments:
Post a Comment