tangazo

tangazo

Saturday, March 21, 2015

VIKUNDI VYA MAZOEZI YA VIUNGO VYAONGEZEKA ZANZIBAR


ZANZIBAR.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amezindua rasmi Kikundi cha Mazoezi ya Viungo cha wanawake kiliopo Mtaa wa Mwera { Mwera Fitness Club }KATIKA Wilaya ya Magharibi.

Uzinduzi huo  UMEFANYIKA katika viwanja vya michezo vya Skuli ya Regeza Mwendo na kushirikisha vikundi kadhaa vya mazoezi vya hapa Unguja wakijumuika pamoja na Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo chini ya Waziri wake Said Ali Mbarouk.

Balozi Seif aliyaongoza maandamano ya wana vikundi mbali mbali katika uzindui huo yaliyoanzia Mtofaani kupita Kituo cha Polisi cha Muembe Mchomeke na kuMALIZIA katika Viwanja vya Skuli ya Regeza Mwendo.

Akizungumza na wanavikundi hao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aMEsema KUWA watu wengi wanaendelea kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa viungo kutokana na kuugua maradhi ambayo yanaweza kuondoka kabisa iwapo jamii itajipangia utaratibu wa kufanya mazoezi.

Balozi Seif aMEsema KUWA ongezeko la wananchi kukimbilia Hospitalini kupata huduma za afya sambamba na Serikali kuu kuagiza dawa zinazogharimu fedha nyingi litapunguwa IWApo watu wengi watafanya mazoezi kila siku.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wananchi kujipangia utaratibu wa kufanya mazoezi ya  kila siku mara wamalizapo ibada yao ya sala ya alfajiri kabla ya kuanza harakati zao za Kimaisha.

AMEfahamisha kwamba michezo inaleta urafiki baina ya vikundi na MIONGOZI MWA WATU ikiwa ni moja ya mafanikio makubwa katika kuimarisha nyanja za michezo na kuondosha maradhi mbali mbali.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kwa juhudi zake za kuhamasisha vikundi MBALI MBALI  nchini kushiriki katika mazoezi ya viungo.

Mapema Mwenyekiti wa zoni D ya Vikundi vya mazoezi Zanzibar Juma Khalid aMEsema KUWA Chama cha Vikundi vya Mazoezi Zanzibar { ZABESA } Kiliamua kuvigawa vikundi vya mazoezi Zanzibar kwa lengo la kupata ufanisi mzuri.

aMEsema KUWA Vikundi vya mazoezi ya viungo lengo lake kuu ni kuhakikisha kwamba sekta ya afya Nchini inapunguza uagizaji  wa dawa ambazo zina gharama kubwa kwa kuhamasisha watu kufanya mazoezi ya viungo.

Mwenyekiti huyo wa Zoni D ya vikundi vya mazoezi ya viungo aliwataka viongozi wa ngazi mbali mbali nchini wafanye mazoezi ili kuweka viwili viwili vyao katika hali ya afya.

Akimkaribisha Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk aMEsema KUWA Wizara hiyo itaendelea kuhakikisha kwamba Jamii yote inashawishika katika kufanya mazoezi.

Uzinduzi huo wa kikundi cha mazoezi cha Mwera Fitness Club uliambatana na mchango wa papo kwa papo kusaidia kuimarisha kikundi hicho kichanga kilichoanzishwa mwaka mmoja uliopita na kukifanya kuweka rikodi ya kufikia vikundi 60 vya mazoezi hapa Zanzibar.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AMEWANASIHI AKINA MAMA NCHINI KUONGEZA KASI YA USHIRIKI WAO KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO


ZANZIBAR.

 

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AMEWANASIHI AKINA MAMA NCHINI  KWAMBA MWAKA HUU NI WA KUPATA WANACHOKIHITAJI KWA KARNE NYINGI ZILIZOPITA KATIKA KUONGEZA KASI YA USHIRIKI WAO KATIKA  UCHAGUZI MKUU UJAO UNAOJENGA MAZINGIRA YAO KATIKA MAMLAKA YA MAAMUZI YA TAIFA HILI.

BALOZI SEIF ALIELEZA HAYO WAKATI AKILIFUNGUA KONGAMANO LA MWANAMKE NA UONGOZI KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA LILILOANDALIWA NA TAASISI YA MWANAHARAKATI SITI BINTI SAAD LILILOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA GRAND PALACE KINU CHA TAA MALINDI MJINI ZANZIBAR.

AMESEMA KUWA WAKIPOTEZA FURSA HIYO MWAKA HUU INAWEZA KUWACHUKUWA MIAKA MINGI IJAYO KUPATIKANA KWAKE KUTOKANA NA WASIOPENDA MAENDELEO YA WANAWAKE KUWEPO HAPA NCHINI.

AMESEMA KUWA MARA NYINGI WANAUME KWA KUPENDELEA KUENDELEZA MFUMO DUME WAKO MSTAWI WA MBELE KUPINGA WANAWAKE KUPATA HAKI ZAO KAMA INAVYOSHUHUDIWA HIVI SASA HAPA NCHINI KATIKA KIPINDI HIKII CHA MPITO KUELEKEA KATIKA KURA YA MAONI.

MAPEMA MWENYEKITI WA TAASISI YA MWANAHARAKATI SITI BINTI SAAD BIBI NASRA MOH’D HILAL ALIWAKUMBUSHA AKINA MAMA WENZAKE KWAMBA HUU NI WAKATI MZURI KWAO KUITUMIA NAFASI ILIYOKUWEMO NDANI YA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA KATIKA KUJIIMARISHA KIUONGOZI.

BIBI NASRA AMESEMA KUWA NJIA PEKEE KATIKA KUHAKIKISHA WANA WAKE HAO WANAITUMIA FURSA HIYO NI KUJITOKEZA KWA WINGI KUSHIRIKI KATIKA KUPIGA KURA YA MAONI SAMBAMBA NA USHIRIKI WA UCHAGUZI MKUU WA MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.

MNAENDELEA KUSKILIZA TAARIFA HII YA KHABARI KUTOKA RADIO ADHANA  FM MASJID JUMUIYA RAHALEO ZANZIBAR .

WIZARA YA UWEZESHAJI ,USTAWI WA JAMII, VIJANA , WANAWAKE NA WATOTO IMESHAURIWA KUENDELEA NA MPANGO WAKE WA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE


ZANZIBAR.

WIZARA YA  UWEZESHAJI ,USTAWI WA JAMII, VIJANA , WANAWAKE NA WATOTO IMESHAURIWA KUENDELEA NA MPANGO WAKE WA  KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE KIUCHUMI, KISIASA NA MASUALA YA UONGOZI KWA LENGO LA KUWAFANYA KUWA WATENDAJI BORA KATIKA SHUGHULI ZAO. 

 

USHAURI HUO UMETOLEWA NA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WANAWAKE NCHINI WAKATI WAKITOA SHUKRANI ZAO KWA WIZARA HIYO PAMOJA NA MWEZESHAJI WA MAFUNZO HAYO YANAYOENDELEA KWENYE UKUMBI WA KITENGO CHA KUPAMBANA NA MALARIA, MWANAKWEREKWE. 

 

WAMESEMA KUWA WIZARA IMEFANYA JAMBO ZURI LA KUWAPATIA MAFUNZO KWA WAKATI HUU KUTOKANA NA  WANAWAKE WENGI KUONGOZA TAASISI MBALI MBALI HAPA NCHINI. 

 

WASHIRIKI HAO WAMESEMA WAMEWEZA KUJIFUNZA MAMBO MENGI AMBAYO YAMEWAAMSHA NA KUWA NA ARI YA KUBADILIKA KWA KUFANYA KAZI KWA KUJIAMINI NA KUWA WABUNIFU KATIKA TAASISI ZAO ILI KULETA UFANISI KAZINI. 

 

WAMEAHIDI KUYATUMIA MAFUNZO HAYO IPASAVYO ILI KULETA MABADILIKO KATIKA SEKTA ZAO NA KUHAKIKISHA MAZINGIRA YA SEKTA HIZO YANABADILIKA SAMBAMBA NA KUBORESHA HALI ZA WAFANYAKAZI. 

 

NAE MHADHIRI MWANDAMIZI KUTOKA CHUO KIKUU CHA MZUMBE, MOROGORO AMBAE NI MKUFUNZI WA MAFUNZO HAYO DR, ANDREW SULLE AMEWASISITIZA VIONGOZI HAO KUFANYA KAZI VIZURI ILI WANANCHI WAONE NA WAWEZE KUFAIDIKA NA UTUMISHI WAO. 

 

AIDHA AMESEMA KUWA VIONGOZI WANAHITAJIKA KUELEWA MPANGO MKAKATI,DIRA NA MWELEKEO WA TAASISI ZAO KWA KUFANYA HIVYO WATAWEZA KUJUA NAMNA YA SHUGHULI ZANAVYOENDESHWA KATIKA TAASISI ZAO. 

 

PIA DR. ANDREW AMEWATAKA KUACHA KUJIFUNGIA NDANI BADALA YAKE KUFIKIRIA KUBADILISHA MAMBO KIMAENDELEO KATIKA TAASISI ZAO NA KUTUMIA FURSA YA KUANGALIA UFANISI WA SEKTA NYENGINE ZILIZOFAULU. 

CUF HAITALIPIZA KISASI


ZANZIBAR.

CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMESEMA KUWA IWAPO KITAINGIA IKULU YA ZANZIBAR MWEZI OKTOBA MWAKA HUU HAKITOLIPIZA KISASI KWA CCM  NA BADALA YAKE KITATOA FURSA KWA WANANCHI KUFANYA SHUGHULI ZAO BILA YA KUBAGULIWA NAKUPEWA USUMBUFU WOWOTE.

 

HAYO YAMEELEZWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO MAALIM SEIF HAMAH ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA CHAMA HICHO KUTOKA WILAYA SITA ZA UNGUJA HUKO HOTELI YA BWAWANI ZANZIBAR, AMBAPO PIA MWENYEKITI WA KAMATI YA MARIDHIANO, MZEE HASSAN NASSOR MOYO WA CCM ALIHUDHURIA.

 

MAALIM SEIF AMBAYE PIA NI MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR AMESEMA  KUWA BINAFSI NENO ‘KISASI’ AMELIFUTA KABISA, NA AMEWATAKA WANA CUF WENYE MAWAZO KWAMBA CHAMA HICHO KIKIINGIA IKULU ITAKUWA ZAMU YAO YA KUTESA KUSAHAU HILO.

 

AMEONGEZA KUWA CUF KITAANGALIA MBELE NA WALA HAKITAFUKUA MAKABURI, KITASIMAMIA USAWA HAKUTAKUWA NA UBAGUZI KATIKA AJIRA KWA MISINGI YOYOTE ILE, NA KILA MMOJA ATATEMBEA KIFUA MBELE ILI AJIONE NI MZANZIBARI SAWA NA MWENGINE.

 

AMESEMA KUWA  NI JUKUMU LA WAZEE WA CHAMA HICHO KUWAONGOZA VIJANA KATIKA KUHAKIKISHA CUF INAPATA USHINDI MKUBWA USIOPUNGUA  ASILIMIA 75 KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO, KUTOKANA NA CHAMA HICHO KUWA TEGEMEO LA WAZANZIBARI KATIKA KUWALETEA UKOMBOZI.

 

KATIBU MKUU HUYO AMESEMA KUWA MWAKA 2015 NI MWAKA WA UAMUZI KWA WAZANZIBARI KUHUSU MUSATAKABALI WA NCHI YAO, HIVYO AMEWATAKA WANANCHI KUJIPANGA KUKIPA USHINDI  WA KIHISTORIA CHAMA HICHO ILI KIWEZE KUSHIKA DOLA BILA YA KIKWAZO CHOCHOTE NA KISIMAMIE MATARAJIO YAO.

 

AMESEMA KUWA DALILI ZA USHINDI WA KIHISTORIA KWA CUF 2015 ZINAONEKANA WAZI KWA NAMNA WAZANZIBARI WANAVYOKIKUBALI CHAMA HICHO SIKU HADI SIKU, BAADA YA KUJIDHIHIRISHA NDICHO PEKEE CHENYE NGUVU NA UWEZO WA KUPIGANIA MASLAHI YA WAZANZIBARI NA NCHI YAO.

 

WAKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO WAASISI WA CHAMA HICHO, MZEE ALI HAJI PANDU NA MZEE MACHANO KHAMIS ALI WAMETOA WITO KWA WANANCHI WA ZANZIBAR KUMPA NGUVU NA KUZIDI KUMUUNGA MKONO KATIBU WA CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KATIKA KUTETEA HADHI NA HESHIMA YA ZANZIBAR.

 

KWA UPANDE WAKE, MZEE HASSAN NASSOR MOYO AMESEMA KUWA MAALIM SEIF NI KIONGOZI JASIRI MWENYE AZMA YA DHATI ISIYOTETEREKA KATIKA KUHAKIKISHA ZANZIBAR INABAKI KATIKA UTULIVU NA WANANCHI WAKE WANAKUWA WAMOJA.

Monday, March 16, 2015

hospitali za Zanzibar hazifanyi biashara ya vipimo vya aina yoyote katika maabara zake


ZANZIBAR.

 

Waziri wa  Afya Zanzibar  Mahmoud Thabiti Kombo amesema KUWA hospitali za Zanzibar hazifanyi biashara ya vipimo vya aina yoyote katika maabara zake bali huwataka  wananchi kuchangia kwa baadhi ya vipimo hivyo na kupewa risiti mara baada ya kuchangia huduma hiyo.

 

Hayo ameyaeleza wakati akijibu  la mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani Wilaya ya Magharibi Unguja.

 

AmeELEZEA  haja kwa wananchi kudai risiti ya malipo wakati wanapochangia huduma hiyo ili iwe ndio uthibitisho wa malipo hayo na IWAPO ikitokea kwa mwananchi yoyote kutopewa risti hiyo kwa ajili  ya huduma aliyochangia  anatakiwa  kutoa taarifa kwa uongozi wa hospitali aliyolipia au kutoa taarifa kwa watendaji wa wizara hiyo.

 

Aidha  amesema kuwa uongozi wa Wizara hiyo hauna taarifa juu ya kuwepo kwa wizi wa baadhi ya vifaa vya matibabu na kuuzwa kwa wananchi kutoka kwa watendaji wa wizara hiyo hivyo amesema Wizara yake italifanyia kazi tatizo hilo ipasavyo ili kulipatia ufumbuzi unaofaa na kuwataka wananchi kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa IWAPO waTabaini kuwepo kwa tatizo hilo kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

KAMPUNI YA SEA WEED COOPERATION YAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANANNCHI


PEMBA.

 

Kampuni ya mwani  ya Sea weed cooperation  imesema kUWA  itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi  wanaoshiriki kulima zao hilo kwa kuhakikisha  changamoto zinazowakabili wakulima  hao   zinapatiwa ufumbuzi .

 

Hayo yameelezwa   na  Meneja  wa Kampuni  hiyo  Zanzibar  ndUGU Hamil  Said  sudi    alipokua akizungumza  na wakulima wa mwani  wakijiji cha shumba mjini KISIWANI Pemba  na kuelezea  jinsi Kampuni  hiyo ilivojipanga  kuboresha maisha  ya wakulima  kwa kuwapatia VIFAA  ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kuboresha maisha yao.

 

Amesema   KUWA kampuni ya sea weed cooperation  lengo lake kubwa  la kutoa vifaa vya kutosha kuwapa wakulima  kinyume na makampuni mengine yanavofanya  ili kuwawezesha wakulima  kuongeza kipato chao  na kumudu kununua  vifaa na mahitaji mengine wanayoyahitaji .

 

HATA Hivyo MENEJA HUYO amewasihi wananchi  kujenga imani na kampuni hiyo  kwa kuwauzia  mwani wote  wanaolima  kinyume na wanavYofanya hivi sasa ambapo baadhi ya wananchi  huwauzia makampuni mengine  ambayo hayawasaidii chochote  katika kuimarisha  zao hilo  na kuwataka  KUheshimu makubaliano licha yaKUTOKUWEPO  mikataba ya maandishi.

 

Amesema  KUWA kampuni yake  imewahakikishia wananchi wa shumba mjini  kuwa  katika kipindi cha miezi sita  ijayo  watatoa vifaa vya kutosha   kwa wakulima  wa kijiji hicho  ikiwa ni pamoja  na vihori  40 ,madau 2  , mabanda ya kuhifadhia mwani , naKUjenga  ngazi mbili  katika madiko  ambayo wananchi watayachagua wenyewe.

 

Akizungumza  na wananchi hao  meneja  wa kampuni hiyo Tawi la Pemba   Jabir  Salim Shamsham   amesema kwamba  jitihada zinazochukuliwa  ni kuongeza uzalishaji  utakao wawezesha  wananchi kupambana na umaskini   na kujenga mazingira mazuri  yatakayowawezesha  watoto wa wakulima wa mwani  kupata elimu ya kutosha .

 

Nao wakulima wa zao hilo  wamelalamikia  bei iliyopo hivi sasa ya mwani ya shilingi 500 kwa kilo kuWa ni ndogo Ikilinganisha  na kazi  kubwa    wanayoiFaNYa wakulima  na kuishauri  kampuni hiyo kuongeza  bei ya zao hilo  licha ya ukweli  uliotolewa na viongozi hao  juu ya bei ya zao hilo  katika soko la dunia ,gharama  za uendeshaji  ndani na nje ya nchi  na udanganyifu unaofanywa na wakulima   wa kuuharibu mwani  kutokana na tamaa.

UONGOZI WA KAMISHENI YA WAKFU NA MALI YA AMANA PEMBA YAONYWA


PEMBA.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuonya Uongozi wa Kamisheni ya Wakfu na Mali Amana Kisiwani Pemba kusitisha zoezi la uwekaji wa Mabango  ya kuzuia ujenzi wa Nyumba katika eneo la ardhi lenye mzozo liliopo Kifoi – Limbani Wete pamoja na la Junguni Gando Kisiwani Pemba.

Balozi Seif aMEtoa onyo hilo alipofanya ziara fupi kukagua eneo hilo ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya Kamisheni ya Wakfu na wananchi waliopewa viwanja na mamlaka husika kujenga nyumba za kuishi.

Amesema KUWA  iwapo Uongozi huo wa Wakfu na Mali ya Amana ulikuwa ukitekeleza agizo uliLopewa na Kiongozi yeyote  suala hilo litajadiliwa katika Vikao vya Baraza la Mapinduzi Zanzibar hapo baadaye.

AMEsemaKUWA  eneo hilo la Kifoi Limbani Wete Pemba ni miongoni mwa Maeneo ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyagawa kwa Wananchi eka tatu tatu mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ili waendeleze shughuli za Kilimo.

AMEfahamisha kwamba Hati zote zilizotolewa na kutumika kuhusu umiliki wa matumizi ya Ardhi katika Visiwa vya Zanzibar kabla ya mwaka 1964 hazitumiki tena na kwa sasa ni batili.

Balozi Seif alisisitiza kwamba ardhi yote ya Visiwa vya Zanzibar ni mali ya Serikali, Hivyo mipango yoyote itakayoamuliwa na Serikali katika matumizi ya ardhi hiyo popote pale ndani ya Zanzibar ni lazima iheshimiwe na Wananchi pamoja na Taasisi za umma na binafsi.

Akitoa ufafanuzi  Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Pemba Ndugu Said Iddi Hamad alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wizara hiyo kupitia Idara ya Ardhi na Mipango Miji ilikata viwanja na kugaWa KWA Wananchi kwa lengo la kujenga nyumba za Kuishi.

NdUGU  Said aMEsema KUWA  hatua hiyo imekuja baada ya eneo hilo kuanza kuvamiwa na kuanzishwa ujenzi holela jambo ambalo Taasisi ya Ardhi  ikalazimika kuchukuwa hatua za kitaalamu za kulipima eneo hilo katika mfumo unazingatia mipango miji.

RAIS WA ZANZIBAR ATAKIWA KUFATILIA MIENENDO YA WATENDAJI WA SERIKALI


ZANZIBAR.

 

CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMEMTAKA RAIS WA ZANZIBAR DR ALI MOHD SHEIN KUFUATILIA MYENENDO YA WATENDAJI WA SEREKALI ANAYOIONGOZA  ILI KUWADHIBITI VIONGOZI  WALIO TAYARI KUHATARISHA AMANI YA NCHI KWA MASLAHI BINAFSI ILI KUFIKIA LENGO LAKUUNDWA KWA SEREKALI YA UMOJA WAKITAIFA.

 

TAARIFA ILIYOTOLEWA KWA VYOMBO NAKUSAINIWA NA MKURUGENZI WA KHBARI ,UENEZI NA MAWASILIANO YA UMMA  WA CUF NDUGU SALIM BIMANI IMEVISHAURI VYOMBO VYA KHABARI  VYA SEREKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUACHA USHABIKI WAKISIASA NAKUTOA TAARIFA ZA MATUKIO YOTE KWA MUJIBU WA TAALUMA YA UANDISHI WA KHABARI .

 

HATA HIVYO TAARIFA HIYO YA CUF IMELITAKA JESHI LA POLISI KUTOKUBALI KUTUMIWA KISIASA NA BAADHI YA VIONGOZI WA SEREKALI.

 

CHAMA HICHO KIMEELEZEA KUSKITISHWA KWAKE NA UTARATIBU MPYA WA ULIOIBUKA NDANI YA JESHI LA POLISI KUZUIA MIKUTANO YA CUF KWA VIGEZO NA SABABU ZAKIINTELIJENSIA ZINAZOTOLEWA  AMBAZO HAZIKUBALIKI NA ZINAWEZA KUPELEKEA KUVUNJIKA KWA AMANI NA UTULIVU WA NCHI KWA MADAI  YAKUKIBEBA CHAMA CHA MAPINDUZI.

 

TAARIFA HIYO YA CUF IMEWATAKA WANANCHI WA ZANZIBAR KUTOVUNJIKA MOYO NAKUTISHIKA KUTOKANA NA VITIMBI VYA CCM NAKUTOKUBALI KUTOLEWA KATIKA HARAKATI ZA MAPAMBANO YAO YAKUDAI MAMLAKA KAMILI ZANZIBAR.

 

MARA KADHAA CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMEKUWA KIKILAMIKIA BAADHI YA WATENDAJI KUINGIZA SIASA KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI.

Thursday, March 5, 2015

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR YAKAMILISHA KUTUNGA SERA YA JINSIA


ZANZIBAR.

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR  IMESEMA KUWA  IMESHAKAMILISHA KUTUNGA SERA YA JINSIA NA USHIRIKISHWAJI WA MAKUNDI MAALUMU ILI KUTOA FURSA KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI.

  

HAYO YAMEELEZWA NA MKUU WA DIVISHENI YA UCHAGUZI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR  IDRISA HAJI JECHA, KATIKA SEMINA YA SIKU MOJA KWA WAANDISHI WA HABARI, WAKATI AKITOA MADA KUHUSU MATAYARISHO YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015, ILIOYOFANYIKA KATIKA HOTELI YA ZANZIBAR BEACH RESORT  ZANZIBAR.

  

AMESEMA KUWA MCHAKATO WA SERA HIYO UMEFANYWA KWA PAMOJA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA WANAWAKE (UNMWOMEN).

 

 AMEONGEZA  KUWA SERA HIYO INA LENGO LA KUHAKIKISHA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WANASHIRIKISHWA KIKAMILIFU KATIKA MASUALA YOTE KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI.

  

ALIFAHAMISHA KWAMBA TAYARI MAELEKEZO WASHAPATA NA ITAKUWA NA DIRA NZURI HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.

  

SAMBAMBA NA HILO ALISEMA KUWA KATIKA MATAYARISHO HAYO TUME HIYO INATARAJIA KUTOA MATOKEO YA MAPITIO YA MAJIMBO  YA UCHAGUZI YA  ZANZIBAR MWISHONI MWA MWEZI HUU .

AMEONGEZA KUWA ZEC INATAKIWA KUFANYA MAPITIO YA MAJIMBO YA UCHAGUZI KATIKA KIPINDI CHA KILA BAADA YA MIAKA MINANE HADI MIAKA 10 NA KUCHUNGUZA IDADI YA MIPAKA NA MAJINA YA MAJIMBO HAYO AMBAPO KAZI HIYO IMEANZA MWEZI JUNI 2014.

AMESEMA KUWA KAZI HIYO TAYARI IMESHAFANYIKA VIZURI KWA USHIRIKIANO MKUBWA WA WADAU WA UCHAGUZI KWA UNGUJA NA PEMBA NAMNA YA MIPAKA YA MAJIMBO.

 
KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA WA KITI CHA URAIS WA ZANZIBAR, ALISEMA WAGOMBEA WA BARAZA LA WAWAKILISHI NA UGOMBEA UDIWANI KATIKA SERIKALI ZA MITAA UTAFANYIKA SEPTEMBAR 7 MWAHA HUU.

JUMLA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 31 ZIMETUMIKA KUTENGENEZA STUDIO MPYA ZA KISASA ZA AZAM TV,


DAR-ES-SALAAM.

 

JUMLA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 31 ZIMETUMIKA KUTENGENEZA STUDIO MPYA ZA KISASA ZA AZAM TV, ZILIZOPO ENEO LA TABATA RELINI, DAR ES SALAAM.

HAYO YAMESEMWA NA NAIBU MTENDAJI MKUU WA AZAM MEDIA LIMITED, TIDO MHANDO WAMILIKI WA AZAM TV LEO MCHANA KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI, TABATA, DAR ES SALAAM. 

MHANDO MWENYE UZOEFU WA KUONGOZA KAMPUNI KUBWA ZA VYOMBO VYA HABARI ZIKIWEMO IDHAA YA KISWAHILI BBC, SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TAIFA (TBC) NA MWANANCHI COMMUNICATION LIMITED (MCL), AMESEMA KUWA STUDIO HIZO ZINA UBORA KULIKO NYINGINE ZOTE NCHINI.

TIDO AMESEMA KUWA BAADA YA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA STUDIO HIZO, ZOEZI LA UZINDUZI WAKE RASMI LITAFANYIKA KABLA YAKUKAMILIKA WIKI HII.

MHANDO AMBAYE ALIKUWA MTANGAZAJI MAARUFU WA MPIRA WA MIGUU ENZI ZAKE NCHINI KUPITIA REDIO TANZANIA DAR ES SALAAM (RTD), ALISEMA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI HUO ANATARAJIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE.

WAZIRI WA AFYA WA ZANZIBAR RASHID SEIF SULEIMAN AMESEMA SIKIO, MDOMO NA MACHO NI SEHEMU MUHIMU SANA


ZANZIBAR.

 

WAZIRI WA AFYA WA ZANZIBAR  RASHID SEIF SULEIMAN AMESEMA SIKIO,  MDOMO  NA MACHO NI SEHEMU MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YA  BINAADAMU HIVYO UNAPOKUWA NA WATAALAMU WA  KUSHUGHULIKIA VIUNGO HIVYO NI NEEMA KUBWA INAYOPASWA KUENZIWA.

WAZIRI HUYO  AMEELEZWA  HAYO KTIKA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA MJINI ZANZIBAR WAKATI WA UZINDUZI  WA KUWAPIMA USIKIVU WATOTO WACHANGA MARA  BAADAYA KUZALIWA ILI KUJUA MATATIZO YAO.

AMESEMAKUWA  UCHUNGUZI  WA WATOTO WACHANGA KUJUA USIKIVU WAO  MAPEMA NI MPANGO MZURI  AMBAO UTALISAIDIA TAIFA KUWA NA   WATOTO WENYE USIKIVU  MZURI NA NJIA RAHISI  YA KUWAPATIA MATIBABU KWA WATAKAOGUNDULIKA NA MATATIZO HAYO.

AMESEMA  MARADHI YA USIKIVU  YAMEKUWA YAKIWASUMBUA WATOTO WENGI ZANZIBAR NA IWAPO KILA MZAZI ATATIMIZA WAJIBU WAKE WA KUMPELEKA  MTOTO WAKE  KUPATA VIPIMO YATAWEZA KUPUNGUA.

WAZIRI WA AFYA ALIWATAKA WAZAZI  KUWA NA UTAMADUNI WA KUZALIA HOSPITALI  ILI KUPATA HUDUMA HIYO KWA URAHISI NA WATAKAOZALIA MAJUMBANI  KUWAPELEKA WATOTO WAO KUCHUNGUZWA USIKIVU MARA BAADA YA KUZAA.

AIDHA WAZIRI HUYO ALIWATAKA MADAKTARI  WALIOPATIWA MAFUNZO YA KUTOA HUDUMA HIYO KUWA WAADILIFU KATIKA KUTEKELEZA KAZI ZAO KWANI HUDUMA ZA WATOTO WACHANGA  NA WAZAZI ZINAHITAJI UVUMILIVU.

WAZIRI ALISEMA TATIZO LA USKIVU HUAZIA  MTOTO  ANAPOCHELEWA KULIA MARA BAADA YA KUZALIWA AMA WANAPOPATA HOMA YA MANJANO, KUTOPATIWA CHANJO, MZAZI KUCHELEWA KUZAA BAADA YA UCHUNGU WA MUDA  MREFU NA KUZALIWA MTOTO BILA YA YA KUFIKA MUDA WA KUZALIWA.

NAO MADAKTARI WALIO PATIWA MAFUNZO HAYO WAMESEMA KUWA WANA UWEZO MZURI WA KUWAPIMA USIKIVU WATOTO  NA KUBAINI MATATIZO YAO  NA KUISHAURI SERIKALI KUANDAA UTARATIBU MZURI WA KUWAFIKIA WATOTO WATAKAOZALIWA VIJIJINI.

MRADI HUO WA KUPIMA WATOTO USIKIVU ULIPOKEA MSADA WA VIFAA VYA KISASA VYA UCHUNGUZI KUTOKA JUMUIYA YA MADAKTARI WANOTOA HUDUMA ZA MATIBABU VIJIJINI ( ZOP) AMBAVYO VINA THAMANI VYA DOLA ELFU 50 ZA KIMAREKANI. 

Sunday, March 1, 2015

MARUFUKU YA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI KATIKA MAENEO YA SKULI KWA WANAFUNZI INAENDELEA


WILAYA YA KATI.

 

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR IMESEMA KUWA MARUFUKU YA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI KATIKA MAENEO YA SKULI KWA WANAFUNZI INAENDELEA.

 

HAYO YAMEELEZWA LEO NA AFISA WA ELIMU WILAYA YA KATI UNGUJA MAALIM MAKAME HAJJI SRANLEY WAKATI AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA UMOJA WA SEREKALI ZA WANAFUNZI ZANZIBAR USEWAZA KILICHOFANYIKA KATIKA VIUNGA VYA SKULI YA DUNGA.

 

AMESEMA KUWA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI KWA WANAFUNZI YANACHANGIA KUPUNGUA KWA KIWANGO CHA UFAULU NAKUPELEKEA KUONGEZEKA KWA VIJANA WASIO NA TAALUMA.

 

AIDHA AFISA HUYO AMEBAINISHA KUWA TATIZO LA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI LINACHANGIA NA BAADHI YA WAZAZI KUTOHUDHURIA VIKAO VINAVYOITISHWA NA WALIMU MASKULINI KWA LENGO LAKUJADILI NAKUTATUA KERO ZA WANAFUNZI.

 

KWA UPANDE WAKE KATIBU WA UMOJA WA SEREKALI ZA WANAFUNZI ZANZIBAR USEWAZA NDUGU SALIM HUMOUD SALIM AMESEMA KUWA KWA MUJIBU WA SHERIA YA MWAKA 1982 KIFUNGU NO 06 NI MARUFUKU KWA MWANAFUNZI KUTUMIA SIMU AKIWA KATIKA MAZINGIRA YA SKULI AMBAPO BAADHI YA WANAFUNZI WANAKWENDA KINYUME NA SHERIA HIYO.

 

HATA HIVYO KATIBU HUYO AMEFAFANUA KUWA WAZAZI WANA NAFASI KUBWA YAKUTOA USHIRIKIANO KATIKA KAMATI ZA SKULI KWA LENGO LAKUTATUA TATIZO HILO.

 

NAO WANAFUNZI WALIOHUDHURIA KATIKA KIKAO HICHO WAMEIOMBA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR KUPANGA MIKAKATI YAKUDHIBITI VITAMBULISHO VYAKE ILI VISITUMIKE KATIKA USAJILI WA SIMU KWA WANAFUNZI.

MKUU WA WILAYA YA WETE HASSAN KHATIB HASSAN AMELITAKA JESHI LA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KUTOWAVUNJA MOYO WAATHIRIWA WA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KINJISIA


WILAYA YA WETE.

 

MKUU WA WILAYA YA WETE HASSAN KHATIB HASSAN AMELITAKA JESHI LA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KUTOWAVUNJA MOYO WAATHIRIWA WA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KINJISIA WANAPOFIKA KATIKA VITUO VYA POLISI.

KIONGOZI HUYO AMETOA WITO HUO KATIKA UKUMBI WA JAMHURI WETE ALIPOKUWA AKIFUNGA MAFUNZO YA SIKU TANO KWA ASKARI POLISI WA DAWATI LA JINSIA LA WANAWAKE NA WATOTO WA MKOA WA KASKAZINI, AMBAO NDIO WANAOJISHUGHULISHA NA UFUATILIAJI PAMOJA NA UPELELEZI WA KESI ZINAZOHUSIANA NA VITENDO VYA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.

AMESEMA KUWA KUWAVUNJA MOYO WAATHITRIWA KUNAJENGA MATUMAINI MABOVU KATI YA JAMII NA JESHI LA POLISI , HIVYO AMEWATAKA ASKARI HAO WAWE WAPIGANAJI NAMBA MOJA KATIKA KUONDOA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.

AMEONGEZA KUWA  KUWAVUNJA MOYO WAATHIRIWA WA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA, KUNAWAATHIRI KISAIKOLOJIA WANAWAKE , WATOTO ,FAMILIA NA JAMII NZIMA.

 

KWA UPANDE WAKE MRATIBU WA MAFUNZO HAYO, AMBAE PIA NI MRATIBU WA DAWATI LA JINSIA LA WANAWAKE NA WATOTO KUTOKA MAKAO MAKUU YA POLISI ZANZIBAR, MAUA SALEH JUMA AMESEMA KUWA  MIONGONI MWA MALENGO YA MAFUNZO HAYO NI KUWAJENGEA UFAHAMU  WASHIRIKI KUBADILISHANA UZOEFU PAMOJA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KATIKA KUSHUGHULIKIA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA.

 

AMESEMA KUWA POLISI WANAOSHUGHULIKIA MADAWATI NDIO MLANGO PEKEE WA KUELEKEA KUYAMALIZA MATENDO HAYO NDANI YA JAMII.

NAE BI ZAINAB ABDALLA ALI AMBAE NI MSHIRIKI WA MAFUNZO HAYO, AMESEMA KUWA  MAFUNZO HAYO YATAWAPA FURSA YA KUFANYA KAZI ZAO KWA UHAKIKA NA UBORA KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA USTAWI WA JAMII WA WILAYA NA MKOA.

AKIMKARIBISHA MGENI RASMI, MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOA WA KASKAZINI PEMBA MRAKIBU WA POLISI KHEIR MUSSA, AMESEMA KUWA MAFUNZO HAYO YATASAIDIA UHARAKISHAJI WA UPELELEZI NA KUTOKUWEPOUCHELEWESHAJI KWA KESI ZINAZOHUSIANA NA UNYANYASAJI NA UKATILI WA KIJINSIA .

MAFUNZO HAYO YAMEANDALIWA KWA USHIRIKIANO KATI  YA JESHI LA POLISI NA SHIRIKA LAKUHUDUMIA  WATOTO LA UMOJA WA MATAIFA UNICEF.

WAANDISHI WA KHABARI NCHINI WANA NAFASI KUBWA YA KUITUMIA TAALUMA YAO KATIKA KUSAIDIA WANANCHI KUFANIKISHA VYEMA KURA YA MAONI


ZANZIBAR.

 

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AMESEMA KUWA WAANDISHI WA KHABARI NCHINI WANA NAFASI KUBWA YA KUITUMIA TAALUMA YAO KATIKA KUSAIDIA WANANCHI KUFANIKISHA VYEMA  KURA YA MAONI INAYOTARAJIWA KUFANYIKA MWEZI WA APRILI PAMOJA NA UCHAGUZI MKUU WA MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.

BALOZI SEIF  AMEELEZA HAYO KATIKA MAHAFALI YA SITA YA KUWATUNUKU VYETI NA STASHAHADA WAHITIMU 105 WA CHUO CHA UANDISHI WA KHABARI ZANZIBAR YALIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA WIZARA YA KHABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO KIKWAJUNI MJINI ZANZIBAR.

AMESEMA KUWA WANAHABARI WATAPOJIKITA VIZURI KUFANYA KAZI ZAO KWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YAO NA UZALENDO NI DHAHIRI KWAMBA WATAISAIDIA JAMII KATIKA KULINDA AMANI ILIYOPO NA KULIFANYA TAIFA KUPIGA HATUA KUBWA YA MAENDELEO.

AMEELEZEA FARAJA YAKE KUTOKANA NA MAENDELEO MAKUBWA YALIYOPATIKANA TOKEA KUANZISHWA KWA CHUO CHA HABARI ZANZIBAR AMBAPO JUMLA YA WANACHUO MIA 628 WAMEHITIMU NGAZI MBALI MBALI TOKEA MWAKA 2010.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ALISEMA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAELEWA CHANGAMOTO KUBWA ZINAZOKIKABILI CHUO CHA HABARI ZANZIBAR LIKIWEMO ENEO LA UJENZI WA MAJENGO MAPYA YA KUDUMU AMBAPO TAYARI IMESHATENGA ENEO LA UKUBWA WA MITA 180 KWA 150 LITAKALOJENGWA MAJENGO HAYO.

AMESEMA KUWA SERIKALI ITATENGA FUNGU MAALUM LA FEDHA MWAKA HUU WA 2015/2016 KWA AJILI YA KUENDELEZA MRADI WA UJENZI WA MAJENGO MAPYA  LIKIWEMO LA GHOROFA MBILI PAMOJA NA KUYAFANYIA MATENGENEZO MAKUBWA MAJENGO MAWILI YATAKAYOTUMIKA KAMA OFISI ZA CHUO.

AKISOMA RISALA YA WAHITIMU HAO CHUO CHA WAANDISHI WA HABARI  MUHITIMU ABOUBAKAR HARITH BAKARI AMESEMA KUWA WAHITIMU HAO WAMEAHIDI KUTUMIA VIZURI KALAMU ZAO ILI LENGO LA TAALUMA WALIYOIPATA LIWEZE KUFANIKIWA.

AMESEMA KUWA YAPO MAFANIKIO YANAYOJICHOMOZA KWA WANAFUNZI WA CHUO HICHO WAKATI WANAPOKUWA KWENYE MAZOEZI YA VITENDO AMBAPO BAADHI YA VITUO VYA HABARI HUONYESHA ISHARA YA KUTAKA KUWAAJIRI KUENDELEA NA KAZI KWENYE VITUO HIVYO.

MAPEMA MKUU WA CHUO CHA HABARI ZANZIBAR DR. ABOUBAKAR SHEIKH RAJAB ALISEMA JUHUDI ZA UONGOZI WA CHUO HICHO ZIMEPELEKEA KUONGEZEKA KWA IDADI YA WANAFUNZI WANAODAHILIWA KILA MWAKA.

MAOMBI YAENDELEA KWA SALMIN AWADHI


ZANZIBAR.

 

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK. ALI MOHAMED SHEIN  AMEUNGANA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA DINI, VYAMA NA SERIKALI PAMOJA NA WANANCHI KUTOKA MAENEO MBALI MBALI YA ZANZIBAR KATIKA HITMA YA KUMUOMBEA MAREHEMU SALMIN AWADH SALMIN ALIYEKUWA MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI .

 

HITMA HIYO ILIYOTAYARISHWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM )ZANZIBAR, ILISOMWA KATIKA MASJID MUSHAWAR, MWEMBESHAURI MJINI ZANZIBAR NA KUTANGULIWA NA  QUR-AN TUKUFU ILIYOSOMWA NA SHEIKH SHARIF ABDULRAHMAN.

 

VIONGOZI WA DINI NAO WALIPATA FURSA YA KUTOA MAWAIDHA KWA MNASABA WA TUKIO HILO AMBAPO KATIBU MKUU WA MUFTI SHEIKH FADHIL SORAGA ALITOA MAWAIDHA KUHUSU MADA YA MAUTI PAMOJA NA HAJA YA KUMUOMBEA DUA MAITI.

 

MIONGONI MWA VIONGOZI WALIOHUDHURIA NI KADHI MKUU WA ZANZIBAR SHEIKH KHAMIS HAJI, NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR VUAI ALI VUAI, MAWAZIRI, WABUNGE,WAWAKILISHI NA VIONGOZI WENGINE WA SERIKALI, DINI NA VYAMA VYA SIASA PAMOJA NA WANANCHI KUTOKA MIKOA YA UNGUJA KICHAMA NA KISERIKALI.