ZANZIBAR.
TUME YA
UCHAGUZI ZANZIBAR IMESEMA KUWA
IMESHAKAMILISHA KUTUNGA SERA YA JINSIA NA USHIRIKISHWAJI WA MAKUNDI
MAALUMU ILI KUTOA FURSA KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKI
KATIKA UCHAGUZI.
HAYO
YAMEELEZWA NA MKUU WA DIVISHENI YA UCHAGUZI WA TUME YA UCHAGUZI YA
ZANZIBAR IDRISA HAJI JECHA, KATIKA
SEMINA YA SIKU MOJA KWA WAANDISHI WA HABARI, WAKATI AKITOA MADA KUHUSU
MATAYARISHO YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2015, ILIOYOFANYIKA KATIKA HOTELI YA
ZANZIBAR BEACH RESORT ZANZIBAR.
AMESEMA
KUWA MCHAKATO WA SERA HIYO UMEFANYWA KWA PAMOJA NA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA
LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA WANAWAKE (UNMWOMEN).
AMEONGEZA KUWA SERA HIYO INA LENGO LA KUHAKIKISHA
WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WANASHIRIKISHWA KIKAMILIFU KATIKA
MASUALA YOTE KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI.
ALIFAHAMISHA
KWAMBA TAYARI MAELEKEZO WASHAPATA NA ITAKUWA NA DIRA NZURI HASA KATIKA KIPINDI
HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.
SAMBAMBA
NA HILO ALISEMA KUWA KATIKA MATAYARISHO HAYO TUME HIYO INATARAJIA KUTOA MATOKEO
YA MAPITIO YA MAJIMBO YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR MWISHONI MWA MWEZI
HUU .
AMEONGEZA
KUWA ZEC INATAKIWA KUFANYA MAPITIO YA MAJIMBO YA UCHAGUZI KATIKA KIPINDI CHA
KILA BAADA YA MIAKA MINANE HADI MIAKA 10 NA KUCHUNGUZA IDADI YA MIPAKA NA
MAJINA YA MAJIMBO HAYO AMBAPO KAZI HIYO IMEANZA MWEZI JUNI 2014.
AMESEMA KUWA KAZI HIYO TAYARI IMESHAFANYIKA VIZURI KWA USHIRIKIANO MKUBWA WA WADAU WA UCHAGUZI KWA UNGUJA NA PEMBA NAMNA YA MIPAKA YA MAJIMBO.
AMESEMA KUWA KAZI HIYO TAYARI IMESHAFANYIKA VIZURI KWA USHIRIKIANO MKUBWA WA WADAU WA UCHAGUZI KWA UNGUJA NA PEMBA NAMNA YA MIPAKA YA MAJIMBO.
No comments:
Post a Comment