ZANZIBAR.
CHAMA CHA WANANCHI CUF
KIMEMTAKA RAIS WA ZANZIBAR DR ALI MOHD SHEIN KUFUATILIA MYENENDO YA WATENDAJI
WA SEREKALI ANAYOIONGOZA ILI KUWADHIBITI
VIONGOZI WALIO TAYARI KUHATARISHA AMANI
YA NCHI KWA MASLAHI BINAFSI ILI KUFIKIA LENGO LAKUUNDWA KWA SEREKALI YA UMOJA
WAKITAIFA.
TAARIFA ILIYOTOLEWA KWA
VYOMBO NAKUSAINIWA NA MKURUGENZI WA KHBARI ,UENEZI NA MAWASILIANO YA UMMA WA CUF NDUGU SALIM BIMANI IMEVISHAURI VYOMBO
VYA KHABARI VYA SEREKALI YA MAPINDUZI YA
ZANZIBAR KUACHA USHABIKI WAKISIASA NAKUTOA TAARIFA ZA MATUKIO YOTE KWA MUJIBU
WA TAALUMA YA UANDISHI WA KHABARI .
HATA HIVYO TAARIFA HIYO
YA CUF IMELITAKA JESHI LA POLISI KUTOKUBALI KUTUMIWA KISIASA NA BAADHI YA
VIONGOZI WA SEREKALI.
CHAMA HICHO KIMEELEZEA
KUSKITISHWA KWAKE NA UTARATIBU MPYA WA ULIOIBUKA NDANI YA JESHI LA POLISI
KUZUIA MIKUTANO YA CUF KWA VIGEZO NA SABABU ZAKIINTELIJENSIA ZINAZOTOLEWA AMBAZO HAZIKUBALIKI NA ZINAWEZA KUPELEKEA
KUVUNJIKA KWA AMANI NA UTULIVU WA NCHI KWA MADAI YAKUKIBEBA CHAMA CHA MAPINDUZI.
TAARIFA HIYO YA CUF
IMEWATAKA WANANCHI WA ZANZIBAR KUTOVUNJIKA MOYO NAKUTISHIKA KUTOKANA NA VITIMBI
VYA CCM NAKUTOKUBALI KUTOLEWA KATIKA HARAKATI ZA MAPAMBANO YAO YAKUDAI MAMLAKA
KAMILI ZANZIBAR.
MARA KADHAA CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMEKUWA
KIKILAMIKIA BAADHI YA WATENDAJI KUINGIZA SIASA KATIKA UTENDAJI WAO WA KAZI.
No comments:
Post a Comment