ZANZIBAR.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AMEWANASIHI AKINA
MAMA NCHINI KWAMBA MWAKA HUU NI WA KUPATA WANACHOKIHITAJI KWA KARNE
NYINGI ZILIZOPITA KATIKA KUONGEZA KASI YA USHIRIKI WAO KATIKA UCHAGUZI
MKUU UJAO UNAOJENGA MAZINGIRA YAO KATIKA MAMLAKA YA MAAMUZI YA TAIFA HILI.
BALOZI SEIF ALIELEZA HAYO WAKATI AKILIFUNGUA KONGAMANO LA MWANAMKE NA
UONGOZI KATIKA KATIBA INAYOPENDEKEZWA LILILOANDALIWA NA TAASISI YA
MWANAHARAKATI SITI BINTI SAAD LILILOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA GRAND
PALACE KINU CHA TAA MALINDI MJINI ZANZIBAR.
AMESEMA KUWA WAKIPOTEZA FURSA HIYO MWAKA HUU INAWEZA KUWACHUKUWA MIAKA
MINGI IJAYO KUPATIKANA KWAKE KUTOKANA NA WASIOPENDA MAENDELEO YA WANAWAKE
KUWEPO HAPA NCHINI.
AMESEMA KUWA MARA NYINGI WANAUME KWA KUPENDELEA KUENDELEZA MFUMO DUME WAKO
MSTAWI WA MBELE KUPINGA WANAWAKE KUPATA HAKI ZAO KAMA INAVYOSHUHUDIWA HIVI SASA
HAPA NCHINI KATIKA KIPINDI HIKII CHA MPITO KUELEKEA KATIKA KURA YA MAONI.
MAPEMA MWENYEKITI WA TAASISI YA MWANAHARAKATI SITI BINTI SAAD BIBI NASRA
MOH’D HILAL ALIWAKUMBUSHA AKINA MAMA WENZAKE KWAMBA HUU NI WAKATI MZURI KWAO
KUITUMIA NAFASI ILIYOKUWEMO NDANI YA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA KATIKA KUJIIMARISHA
KIUONGOZI.
BIBI NASRA AMESEMA KUWA NJIA PEKEE KATIKA KUHAKIKISHA WANA WAKE HAO
WANAITUMIA FURSA HIYO NI KUJITOKEZA KWA WINGI KUSHIRIKI KATIKA KUPIGA KURA YA
MAONI SAMBAMBA NA USHIRIKI WA UCHAGUZI MKUU WA MWEZI OKTOBA MWAKA HUU.
MNAENDELEA
KUSKILIZA TAARIFA HII YA KHABARI KUTOKA RADIO ADHANA FM MASJID JUMUIYA RAHALEO ZANZIBAR .
No comments:
Post a Comment