ZANZIBAR.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI
AMESEMA KUWA WAANDISHI WA KHABARI NCHINI WANA NAFASI KUBWA YA KUITUMIA TAALUMA
YAO KATIKA KUSAIDIA WANANCHI KUFANIKISHA VYEMA KURA YA MAONI
INAYOTARAJIWA KUFANYIKA MWEZI WA APRILI PAMOJA NA UCHAGUZI MKUU WA MWEZI OKTOBA
MWAKA HUU.
BALOZI SEIF
AMEELEZA HAYO KATIKA MAHAFALI YA SITA YA KUWATUNUKU VYETI NA STASHAHADA
WAHITIMU 105 WA CHUO CHA UANDISHI WA KHABARI ZANZIBAR YALIYOFANYIKA KATIKA
VIWANJA VYA WIZARA YA KHABARI, UTAMADUNI, UTALII NA MICHEZO KIKWAJUNI MJINI
ZANZIBAR.
AMESEMA KUWA WANAHABARI WATAPOJIKITA VIZURI KUFANYA KAZI
ZAO KWA KUZINGATIA MAADILI YA TAALUMA YAO NA UZALENDO NI DHAHIRI KWAMBA
WATAISAIDIA JAMII KATIKA KULINDA AMANI ILIYOPO NA KULIFANYA TAIFA KUPIGA HATUA
KUBWA YA MAENDELEO.
AMEELEZEA FARAJA YAKE KUTOKANA NA MAENDELEO MAKUBWA
YALIYOPATIKANA TOKEA KUANZISHWA KWA CHUO CHA HABARI ZANZIBAR AMBAPO JUMLA YA
WANACHUO MIA 628 WAMEHITIMU NGAZI MBALI MBALI TOKEA MWAKA 2010.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ALISEMA SERIKALI YA
MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAELEWA CHANGAMOTO KUBWA ZINAZOKIKABILI CHUO CHA HABARI
ZANZIBAR LIKIWEMO ENEO LA UJENZI WA MAJENGO MAPYA YA KUDUMU AMBAPO TAYARI
IMESHATENGA ENEO LA UKUBWA WA MITA 180 KWA 150 LITAKALOJENGWA MAJENGO HAYO.
AMESEMA KUWA SERIKALI ITATENGA FUNGU MAALUM LA FEDHA
MWAKA HUU WA 2015/2016 KWA AJILI YA KUENDELEZA MRADI WA UJENZI WA MAJENGO
MAPYA LIKIWEMO LA GHOROFA MBILI PAMOJA NA KUYAFANYIA MATENGENEZO MAKUBWA
MAJENGO MAWILI YATAKAYOTUMIKA KAMA OFISI ZA CHUO.
AKISOMA RISALA YA WAHITIMU HAO CHUO CHA WAANDISHI WA
HABARI MUHITIMU ABOUBAKAR HARITH BAKARI AMESEMA KUWA WAHITIMU HAO
WAMEAHIDI KUTUMIA VIZURI KALAMU ZAO ILI LENGO LA TAALUMA WALIYOIPATA LIWEZE
KUFANIKIWA.
AMESEMA KUWA YAPO MAFANIKIO YANAYOJICHOMOZA KWA WANAFUNZI
WA CHUO HICHO WAKATI WANAPOKUWA KWENYE MAZOEZI YA VITENDO AMBAPO BAADHI YA
VITUO VYA HABARI HUONYESHA ISHARA YA KUTAKA KUWAAJIRI KUENDELEA NA KAZI KWENYE
VITUO HIVYO.
MAPEMA MKUU WA CHUO CHA HABARI ZANZIBAR DR. ABOUBAKAR
SHEIKH RAJAB ALISEMA JUHUDI ZA UONGOZI WA CHUO HICHO ZIMEPELEKEA KUONGEZEKA KWA
IDADI YA WANAFUNZI WANAODAHILIWA KILA MWAKA.
No comments:
Post a Comment