ZANZIBAR.
CHAMA CHA WANANCHI CUF KIMESEMA KUWA IWAPO KITAINGIA IKULU YA ZANZIBAR
MWEZI OKTOBA MWAKA HUU HAKITOLIPIZA KISASI KWA CCM NA BADALA YAKE KITATOA FURSA KWA WANANCHI
KUFANYA SHUGHULI ZAO BILA YA KUBAGULIWA NAKUPEWA USUMBUFU WOWOTE.
HAYO YAMEELEZWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO MAALIM SEIF HAMAH ALIPOKUWA
AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA CHAMA HICHO KUTOKA WILAYA SITA ZA UNGUJA HUKO HOTELI YA
BWAWANI ZANZIBAR, AMBAPO PIA MWENYEKITI WA KAMATI YA MARIDHIANO, MZEE HASSAN
NASSOR MOYO WA CCM ALIHUDHURIA.
MAALIM SEIF AMBAYE PIA NI MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR AMESEMA KUWA BINAFSI NENO ‘KISASI’ AMELIFUTA KABISA,
NA AMEWATAKA WANA CUF WENYE MAWAZO KWAMBA CHAMA HICHO KIKIINGIA IKULU ITAKUWA
ZAMU YAO YA KUTESA KUSAHAU HILO.
AMEONGEZA KUWA CUF KITAANGALIA MBELE NA WALA HAKITAFUKUA MAKABURI,
KITASIMAMIA USAWA HAKUTAKUWA NA UBAGUZI KATIKA AJIRA KWA MISINGI YOYOTE ILE, NA
KILA MMOJA ATATEMBEA KIFUA MBELE ILI AJIONE NI MZANZIBARI SAWA NA MWENGINE.
AMESEMA KUWA NI JUKUMU LA WAZEE WA
CHAMA HICHO KUWAONGOZA VIJANA KATIKA KUHAKIKISHA CUF INAPATA USHINDI MKUBWA
USIOPUNGUA ASILIMIA 75 KATIKA UCHAGUZI
MKUU UJAO, KUTOKANA NA CHAMA HICHO KUWA TEGEMEO LA WAZANZIBARI KATIKA KUWALETEA
UKOMBOZI.
KATIBU MKUU HUYO AMESEMA KUWA MWAKA 2015 NI MWAKA WA UAMUZI KWA WAZANZIBARI
KUHUSU MUSATAKABALI WA NCHI YAO, HIVYO AMEWATAKA WANANCHI KUJIPANGA KUKIPA
USHINDI WA KIHISTORIA CHAMA HICHO ILI
KIWEZE KUSHIKA DOLA BILA YA KIKWAZO CHOCHOTE NA KISIMAMIE MATARAJIO YAO.
AMESEMA KUWA DALILI ZA USHINDI WA KIHISTORIA KWA CUF 2015 ZINAONEKANA WAZI
KWA NAMNA WAZANZIBARI WANAVYOKIKUBALI CHAMA HICHO SIKU HADI SIKU, BAADA YA
KUJIDHIHIRISHA NDICHO PEKEE CHENYE NGUVU NA UWEZO WA KUPIGANIA MASLAHI YA
WAZANZIBARI NA NCHI YAO.
WAKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO WAASISI WA CHAMA HICHO, MZEE ALI HAJI PANDU
NA MZEE MACHANO KHAMIS ALI WAMETOA WITO KWA WANANCHI WA ZANZIBAR KUMPA NGUVU NA
KUZIDI KUMUUNGA MKONO KATIBU WA CUF MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KATIKA KUTETEA
HADHI NA HESHIMA YA ZANZIBAR.
KWA UPANDE WAKE, MZEE HASSAN NASSOR MOYO AMESEMA KUWA MAALIM SEIF NI
KIONGOZI JASIRI MWENYE AZMA YA DHATI ISIYOTETEREKA KATIKA KUHAKIKISHA ZANZIBAR
INABAKI KATIKA UTULIVU NA WANANCHI WAKE WANAKUWA WAMOJA.
No comments:
Post a Comment