tangazo

tangazo

Thursday, March 5, 2015

JUMLA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 31 ZIMETUMIKA KUTENGENEZA STUDIO MPYA ZA KISASA ZA AZAM TV,


DAR-ES-SALAAM.

 

JUMLA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 31 ZIMETUMIKA KUTENGENEZA STUDIO MPYA ZA KISASA ZA AZAM TV, ZILIZOPO ENEO LA TABATA RELINI, DAR ES SALAAM.

HAYO YAMESEMWA NA NAIBU MTENDAJI MKUU WA AZAM MEDIA LIMITED, TIDO MHANDO WAMILIKI WA AZAM TV LEO MCHANA KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI, TABATA, DAR ES SALAAM. 

MHANDO MWENYE UZOEFU WA KUONGOZA KAMPUNI KUBWA ZA VYOMBO VYA HABARI ZIKIWEMO IDHAA YA KISWAHILI BBC, SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TAIFA (TBC) NA MWANANCHI COMMUNICATION LIMITED (MCL), AMESEMA KUWA STUDIO HIZO ZINA UBORA KULIKO NYINGINE ZOTE NCHINI.

TIDO AMESEMA KUWA BAADA YA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA STUDIO HIZO, ZOEZI LA UZINDUZI WAKE RASMI LITAFANYIKA KABLA YAKUKAMILIKA WIKI HII.

MHANDO AMBAYE ALIKUWA MTANGAZAJI MAARUFU WA MPIRA WA MIGUU ENZI ZAKE NCHINI KUPITIA REDIO TANZANIA DAR ES SALAAM (RTD), ALISEMA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI HUO ANATARAJIWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE.

No comments:

Post a Comment