ZANZIBAR.
Waziri wa Afya
Zanzibar Mahmoud Thabiti Kombo amesema
KUWA hospitali za Zanzibar hazifanyi biashara ya vipimo vya aina yoyote katika
maabara zake bali huwataka wananchi
kuchangia kwa baadhi ya vipimo hivyo na kupewa risiti mara baada ya kuchangia
huduma hiyo.
Hayo ameyaeleza wakati akijibu la mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim
Ayoub katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani Wilaya ya Magharibi
Unguja.
AmeELEZEA haja
kwa wananchi kudai risiti ya malipo wakati wanapochangia huduma hiyo ili iwe
ndio uthibitisho wa malipo hayo na IWAPO ikitokea kwa mwananchi yoyote kutopewa
risti hiyo kwa ajili ya huduma
aliyochangia anatakiwa kutoa taarifa kwa uongozi wa hospitali
aliyolipia au kutoa taarifa kwa watendaji wa wizara hiyo.
Aidha amesema
kuwa uongozi wa Wizara hiyo hauna taarifa juu ya kuwepo kwa wizi wa baadhi ya
vifaa vya matibabu na kuuzwa kwa wananchi kutoka kwa watendaji wa wizara hiyo
hivyo amesema Wizara yake italifanyia kazi tatizo hilo ipasavyo ili kulipatia
ufumbuzi unaofaa na kuwataka wananchi kushirikiana na Serikali kwa kutoa
taarifa IWAPO waTabaini kuwepo kwa tatizo hilo kwa maslahi yao na Taifa kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment