PEMBA.
Kampuni ya mwani ya Sea weed cooperation imesema
kUWA itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi wanaoshiriki kulima
zao hilo kwa kuhakikisha changamoto zinazowakabili wakulima hao
zinapatiwa ufumbuzi .
Hayo yameelezwa na Meneja wa Kampuni
hiyo Zanzibar ndUGU Hamil Said sudi alipokua
akizungumza na wakulima wa mwani wakijiji cha shumba mjini KISIWANI
Pemba na kuelezea jinsi Kampuni hiyo ilivojipanga
kuboresha maisha ya wakulima kwa kuwapatia VIFAA ili kuongeza
uzalishaji wa zao hilo na kuboresha maisha yao.
Amesema KUWA kampuni ya sea weed
cooperation lengo lake kubwa la kutoa vifaa vya kutosha kuwapa
wakulima kinyume na makampuni mengine yanavofanya ili kuwawezesha
wakulima kuongeza kipato chao na kumudu kununua vifaa na
mahitaji mengine wanayoyahitaji .
HATA Hivyo MENEJA HUYO amewasihi wananchi kujenga
imani na kampuni hiyo kwa kuwauzia mwani wote wanaolima
kinyume na wanavYofanya hivi sasa ambapo baadhi ya wananchi huwauzia
makampuni mengine ambayo hayawasaidii chochote katika kuimarisha
zao hilo na kuwataka KUheshimu makubaliano licha yaKUTOKUWEPO mikataba ya maandishi.
Amesema KUWA kampuni yake imewahakikishia wananchi
wa shumba mjini kuwa katika kipindi cha miezi sita
ijayo watatoa vifaa vya kutosha kwa wakulima wa kijiji
hicho ikiwa ni pamoja na vihori 40 ,madau 2 , mabanda
ya kuhifadhia mwani , naKUjenga ngazi mbili katika madiko
ambayo wananchi watayachagua wenyewe.
Akizungumza na wananchi hao meneja wa
kampuni hiyo Tawi la Pemba Jabir Salim Shamsham
amesema kwamba jitihada zinazochukuliwa ni kuongeza uzalishaji
utakao wawezesha wananchi kupambana na umaskini na kujenga
mazingira mazuri yatakayowawezesha watoto wa wakulima wa
mwani kupata elimu ya kutosha .
Nao wakulima wa zao hilo wamelalamikia bei
iliyopo hivi sasa ya mwani ya shilingi 500 kwa kilo kuWa ni ndogo Ikilinganisha
na kazi kubwa wanayoiFaNYa wakulima na
kuishauri kampuni hiyo kuongeza bei ya zao hilo licha ya
ukweli uliotolewa na viongozi hao juu ya bei ya zao hilo
katika soko la dunia ,gharama za uendeshaji ndani na nje ya
nchi na udanganyifu unaofanywa na wakulima wa kuuharibu
mwani kutokana na tamaa.
No comments:
Post a Comment