ZANZIBAR.
WIZARA YA UWEZESHAJI ,USTAWI WA JAMII, VIJANA
, WANAWAKE NA WATOTO IMESHAURIWA KUENDELEA NA MPANGO WAKE WA KUWAJENGEA
UWEZO WANAWAKE KIUCHUMI, KISIASA NA MASUALA YA UONGOZI KWA LENGO LA KUWAFANYA
KUWA WATENDAJI BORA KATIKA SHUGHULI ZAO.
USHAURI HUO UMETOLEWA NA WASHIRIKI WA MAFUNZO YA
KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WANAWAKE NCHINI WAKATI WAKITOA SHUKRANI ZAO KWA
WIZARA HIYO PAMOJA NA MWEZESHAJI WA MAFUNZO HAYO YANAYOENDELEA KWENYE UKUMBI WA
KITENGO CHA KUPAMBANA NA MALARIA, MWANAKWEREKWE.
WAMESEMA KUWA WIZARA IMEFANYA JAMBO ZURI LA
KUWAPATIA MAFUNZO KWA WAKATI HUU KUTOKANA NA
WANAWAKE WENGI KUONGOZA TAASISI MBALI MBALI HAPA NCHINI.
WASHIRIKI HAO WAMESEMA WAMEWEZA KUJIFUNZA MAMBO
MENGI AMBAYO YAMEWAAMSHA NA KUWA NA ARI YA KUBADILIKA KWA KUFANYA KAZI KWA
KUJIAMINI NA KUWA WABUNIFU KATIKA TAASISI ZAO ILI KULETA UFANISI KAZINI.
WAMEAHIDI KUYATUMIA MAFUNZO HAYO IPASAVYO ILI KULETA
MABADILIKO KATIKA SEKTA ZAO NA KUHAKIKISHA MAZINGIRA YA SEKTA HIZO YANABADILIKA
SAMBAMBA NA KUBORESHA HALI ZA WAFANYAKAZI.
NAE MHADHIRI MWANDAMIZI KUTOKA CHUO KIKUU CHA
MZUMBE, MOROGORO AMBAE NI MKUFUNZI WA MAFUNZO HAYO DR, ANDREW SULLE
AMEWASISITIZA VIONGOZI HAO KUFANYA KAZI VIZURI ILI WANANCHI WAONE NA WAWEZE
KUFAIDIKA NA UTUMISHI WAO.
AIDHA AMESEMA KUWA VIONGOZI WANAHITAJIKA KUELEWA
MPANGO MKAKATI,DIRA NA MWELEKEO WA TAASISI ZAO KWA KUFANYA HIVYO WATAWEZA KUJUA
NAMNA YA SHUGHULI ZANAVYOENDESHWA KATIKA TAASISI ZAO.
PIA DR. ANDREW AMEWATAKA KUACHA KUJIFUNGIA NDANI
BADALA YAKE KUFIKIRIA KUBADILISHA MAMBO KIMAENDELEO KATIKA TAASISI ZAO NA KUTUMIA FURSA YA KUANGALIA UFANISI WA SEKTA NYENGINE
ZILIZOFAULU.
No comments:
Post a Comment