WILAYA YA KATI.
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR IMESEMA KUWA MARUFUKU YA
MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI KATIKA MAENEO YA SKULI KWA WANAFUNZI INAENDELEA.
HAYO YAMEELEZWA LEO NA AFISA WA ELIMU WILAYA YA KATI UNGUJA MAALIM MAKAME
HAJJI SRANLEY WAKATI AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA UMOJA WA SEREKALI ZA
WANAFUNZI ZANZIBAR USEWAZA KILICHOFANYIKA KATIKA VIUNGA VYA SKULI YA DUNGA.
AMESEMA KUWA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI KWA WANAFUNZI YANACHANGIA KUPUNGUA
KWA KIWANGO CHA UFAULU NAKUPELEKEA KUONGEZEKA KWA VIJANA WASIO NA TAALUMA.
AIDHA AFISA HUYO AMEBAINISHA KUWA TATIZO LA MATUMIZI YA SIMU ZA MKONONI
LINACHANGIA NA BAADHI YA WAZAZI KUTOHUDHURIA VIKAO VINAVYOITISHWA NA WALIMU
MASKULINI KWA LENGO LAKUJADILI NAKUTATUA KERO ZA WANAFUNZI.
KWA UPANDE WAKE KATIBU WA UMOJA WA SEREKALI ZA WANAFUNZI ZANZIBAR USEWAZA
NDUGU SALIM HUMOUD SALIM AMESEMA KUWA KWA MUJIBU WA SHERIA YA MWAKA 1982
KIFUNGU NO 06 NI MARUFUKU KWA MWANAFUNZI KUTUMIA SIMU AKIWA KATIKA MAZINGIRA YA
SKULI AMBAPO BAADHI YA WANAFUNZI WANAKWENDA KINYUME NA SHERIA HIYO.
HATA HIVYO KATIBU HUYO AMEFAFANUA KUWA WAZAZI WANA NAFASI KUBWA YAKUTOA
USHIRIKIANO KATIKA KAMATI ZA SKULI KWA LENGO LAKUTATUA TATIZO HILO.
NAO WANAFUNZI WALIOHUDHURIA KATIKA KIKAO HICHO WAMEIOMBA WIZARA YA ELIMU NA
MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR KUPANGA MIKAKATI YAKUDHIBITI VITAMBULISHO VYAKE ILI
VISITUMIKE KATIKA USAJILI WA SIMU KWA WANAFUNZI.
No comments:
Post a Comment