tangazo

tangazo

Monday, March 16, 2015

UONGOZI WA KAMISHENI YA WAKFU NA MALI YA AMANA PEMBA YAONYWA


PEMBA.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuonya Uongozi wa Kamisheni ya Wakfu na Mali Amana Kisiwani Pemba kusitisha zoezi la uwekaji wa Mabango  ya kuzuia ujenzi wa Nyumba katika eneo la ardhi lenye mzozo liliopo Kifoi – Limbani Wete pamoja na la Junguni Gando Kisiwani Pemba.

Balozi Seif aMEtoa onyo hilo alipofanya ziara fupi kukagua eneo hilo ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya Kamisheni ya Wakfu na wananchi waliopewa viwanja na mamlaka husika kujenga nyumba za kuishi.

Amesema KUWA  iwapo Uongozi huo wa Wakfu na Mali ya Amana ulikuwa ukitekeleza agizo uliLopewa na Kiongozi yeyote  suala hilo litajadiliwa katika Vikao vya Baraza la Mapinduzi Zanzibar hapo baadaye.

AMEsemaKUWA  eneo hilo la Kifoi Limbani Wete Pemba ni miongoni mwa Maeneo ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyagawa kwa Wananchi eka tatu tatu mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ili waendeleze shughuli za Kilimo.

AMEfahamisha kwamba Hati zote zilizotolewa na kutumika kuhusu umiliki wa matumizi ya Ardhi katika Visiwa vya Zanzibar kabla ya mwaka 1964 hazitumiki tena na kwa sasa ni batili.

Balozi Seif alisisitiza kwamba ardhi yote ya Visiwa vya Zanzibar ni mali ya Serikali, Hivyo mipango yoyote itakayoamuliwa na Serikali katika matumizi ya ardhi hiyo popote pale ndani ya Zanzibar ni lazima iheshimiwe na Wananchi pamoja na Taasisi za umma na binafsi.

Akitoa ufafanuzi  Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Pemba Ndugu Said Iddi Hamad alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Wizara hiyo kupitia Idara ya Ardhi na Mipango Miji ilikata viwanja na kugaWa KWA Wananchi kwa lengo la kujenga nyumba za Kuishi.

NdUGU  Said aMEsema KUWA  hatua hiyo imekuja baada ya eneo hilo kuanza kuvamiwa na kuanzishwa ujenzi holela jambo ambalo Taasisi ya Ardhi  ikalazimika kuchukuwa hatua za kitaalamu za kulipima eneo hilo katika mfumo unazingatia mipango miji.

No comments:

Post a Comment