ZANZIBAR.
WAZIRI WA AFYA WA ZANZIBAR RASHID SEIF SULEIMAN AMESEMA SIKIO,
MDOMO NA MACHO NI SEHEMU MUHIMU SANA KATIKA MAISHA YA
BINAADAMU HIVYO UNAPOKUWA NA WATAALAMU WA KUSHUGHULIKIA VIUNGO HIVYO NI
NEEMA KUBWA INAYOPASWA KUENZIWA.
WAZIRI HUYO AMEELEZWA HAYO KTIKA HOSPITALI KUU YA MNAZI MMOJA MJINI
ZANZIBAR WAKATI WA UZINDUZI WA KUWAPIMA USIKIVU WATOTO WACHANGA MARA
BAADAYA KUZALIWA ILI KUJUA MATATIZO YAO.
AMESEMAKUWA UCHUNGUZI WA
WATOTO WACHANGA KUJUA USIKIVU WAO MAPEMA NI MPANGO MZURI AMBAO
UTALISAIDIA TAIFA KUWA NA WATOTO WENYE USIKIVU MZURI NA NJIA
RAHISI YA KUWAPATIA MATIBABU KWA WATAKAOGUNDULIKA NA MATATIZO HAYO.
AMESEMA MARADHI YA USIKIVU YAMEKUWA YAKIWASUMBUA WATOTO WENGI
ZANZIBAR NA IWAPO KILA MZAZI ATATIMIZA WAJIBU WAKE WA KUMPELEKA MTOTO
WAKE KUPATA VIPIMO YATAWEZA KUPUNGUA.
WAZIRI WA AFYA ALIWATAKA WAZAZI KUWA NA UTAMADUNI WA KUZALIA
HOSPITALI ILI KUPATA HUDUMA HIYO KWA URAHISI NA WATAKAOZALIA MAJUMBANI
KUWAPELEKA WATOTO WAO KUCHUNGUZWA USIKIVU MARA BAADA YA KUZAA.
AIDHA WAZIRI HUYO ALIWATAKA MADAKTARI WALIOPATIWA MAFUNZO YA KUTOA
HUDUMA HIYO KUWA WAADILIFU KATIKA KUTEKELEZA KAZI ZAO KWANI HUDUMA ZA WATOTO
WACHANGA NA WAZAZI ZINAHITAJI UVUMILIVU.
WAZIRI ALISEMA TATIZO LA USKIVU HUAZIA MTOTO ANAPOCHELEWA KULIA
MARA BAADA YA KUZALIWA AMA WANAPOPATA HOMA YA MANJANO, KUTOPATIWA CHANJO, MZAZI
KUCHELEWA KUZAA BAADA YA UCHUNGU WA MUDA MREFU NA KUZALIWA MTOTO BILA YA
YA KUFIKA MUDA WA KUZALIWA.
NAO MADAKTARI WALIO PATIWA MAFUNZO HAYO WAMESEMA KUWA WANA UWEZO MZURI WA
KUWAPIMA USIKIVU WATOTO NA KUBAINI MATATIZO YAO NA KUISHAURI
SERIKALI KUANDAA UTARATIBU MZURI WA KUWAFIKIA WATOTO WATAKAOZALIWA VIJIJINI.
MRADI HUO WA KUPIMA WATOTO USIKIVU ULIPOKEA MSADA WA VIFAA VYA KISASA VYA
UCHUNGUZI KUTOKA JUMUIYA YA MADAKTARI WANOTOA HUDUMA ZA MATIBABU VIJIJINI (
ZOP) AMBAVYO VINA THAMANI VYA DOLA ELFU 50 ZA KIMAREKANI.
No comments:
Post a Comment