tangazo

tangazo

Sunday, March 1, 2015

MKUU WA WILAYA YA WETE HASSAN KHATIB HASSAN AMELITAKA JESHI LA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KUTOWAVUNJA MOYO WAATHIRIWA WA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KINJISIA


WILAYA YA WETE.

 

MKUU WA WILAYA YA WETE HASSAN KHATIB HASSAN AMELITAKA JESHI LA MKOA WA KASKAZINI PEMBA KUTOWAVUNJA MOYO WAATHIRIWA WA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KINJISIA WANAPOFIKA KATIKA VITUO VYA POLISI.

KIONGOZI HUYO AMETOA WITO HUO KATIKA UKUMBI WA JAMHURI WETE ALIPOKUWA AKIFUNGA MAFUNZO YA SIKU TANO KWA ASKARI POLISI WA DAWATI LA JINSIA LA WANAWAKE NA WATOTO WA MKOA WA KASKAZINI, AMBAO NDIO WANAOJISHUGHULISHA NA UFUATILIAJI PAMOJA NA UPELELEZI WA KESI ZINAZOHUSIANA NA VITENDO VYA UKATILI NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.

AMESEMA KUWA KUWAVUNJA MOYO WAATHITRIWA KUNAJENGA MATUMAINI MABOVU KATI YA JAMII NA JESHI LA POLISI , HIVYO AMEWATAKA ASKARI HAO WAWE WAPIGANAJI NAMBA MOJA KATIKA KUONDOA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA.

AMEONGEZA KUWA  KUWAVUNJA MOYO WAATHIRIWA WA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA, KUNAWAATHIRI KISAIKOLOJIA WANAWAKE , WATOTO ,FAMILIA NA JAMII NZIMA.

 

KWA UPANDE WAKE MRATIBU WA MAFUNZO HAYO, AMBAE PIA NI MRATIBU WA DAWATI LA JINSIA LA WANAWAKE NA WATOTO KUTOKA MAKAO MAKUU YA POLISI ZANZIBAR, MAUA SALEH JUMA AMESEMA KUWA  MIONGONI MWA MALENGO YA MAFUNZO HAYO NI KUWAJENGEA UFAHAMU  WASHIRIKI KUBADILISHANA UZOEFU PAMOJA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOJITOKEZA KATIKA KUSHUGHULIKIA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA.

 

AMESEMA KUWA POLISI WANAOSHUGHULIKIA MADAWATI NDIO MLANGO PEKEE WA KUELEKEA KUYAMALIZA MATENDO HAYO NDANI YA JAMII.

NAE BI ZAINAB ABDALLA ALI AMBAE NI MSHIRIKI WA MAFUNZO HAYO, AMESEMA KUWA  MAFUNZO HAYO YATAWAPA FURSA YA KUFANYA KAZI ZAO KWA UHAKIKA NA UBORA KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA USTAWI WA JAMII WA WILAYA NA MKOA.

AKIMKARIBISHA MGENI RASMI, MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI MKOA WA KASKAZINI PEMBA MRAKIBU WA POLISI KHEIR MUSSA, AMESEMA KUWA MAFUNZO HAYO YATASAIDIA UHARAKISHAJI WA UPELELEZI NA KUTOKUWEPOUCHELEWESHAJI KWA KESI ZINAZOHUSIANA NA UNYANYASAJI NA UKATILI WA KIJINSIA .

MAFUNZO HAYO YAMEANDALIWA KWA USHIRIKIANO KATI  YA JESHI LA POLISI NA SHIRIKA LAKUHUDUMIA  WATOTO LA UMOJA WA MATAIFA UNICEF.

No comments:

Post a Comment