tangazo

tangazo

Sunday, March 1, 2015

MAOMBI YAENDELEA KWA SALMIN AWADHI


ZANZIBAR.

 

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ DK. ALI MOHAMED SHEIN  AMEUNGANA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA DINI, VYAMA NA SERIKALI PAMOJA NA WANANCHI KUTOKA MAENEO MBALI MBALI YA ZANZIBAR KATIKA HITMA YA KUMUOMBEA MAREHEMU SALMIN AWADH SALMIN ALIYEKUWA MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI .

 

HITMA HIYO ILIYOTAYARISHWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM )ZANZIBAR, ILISOMWA KATIKA MASJID MUSHAWAR, MWEMBESHAURI MJINI ZANZIBAR NA KUTANGULIWA NA  QUR-AN TUKUFU ILIYOSOMWA NA SHEIKH SHARIF ABDULRAHMAN.

 

VIONGOZI WA DINI NAO WALIPATA FURSA YA KUTOA MAWAIDHA KWA MNASABA WA TUKIO HILO AMBAPO KATIBU MKUU WA MUFTI SHEIKH FADHIL SORAGA ALITOA MAWAIDHA KUHUSU MADA YA MAUTI PAMOJA NA HAJA YA KUMUOMBEA DUA MAITI.

 

MIONGONI MWA VIONGOZI WALIOHUDHURIA NI KADHI MKUU WA ZANZIBAR SHEIKH KHAMIS HAJI, NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR VUAI ALI VUAI, MAWAZIRI, WABUNGE,WAWAKILISHI NA VIONGOZI WENGINE WA SERIKALI, DINI NA VYAMA VYA SIASA PAMOJA NA WANANCHI KUTOKA MIKOA YA UNGUJA KICHAMA NA KISERIKALI.

No comments:

Post a Comment