tangazo

tangazo

Sunday, February 23, 2014

UHOLANZI NA ZANZIBARA KUSHIRIKIANA

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMEIHAKIKISHIA SERIKALI YA UHOLANZI KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR INA DHAMIRA YA KWELI YA KUENDELEZA NA KUIMARISHA USHIRIKIANO WAKE NA UHOLANZI.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALITOA KAULI HIYO JANA WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAZIRI WA BIASHARA ZA NJE WA NCHI HIYO BIBI LILIANNE PLOUMEN ALIYEMTEMBELEA IKULU.

“NINGEPENDA KUREJEA TENA DHAMIRA YETU YA KUENDELEZA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA UHOLANZI KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA MAENDELEO KWA FAIDA ZA NCHI ZETU NA WATU WAKE” DK. SHEIN ALIMUELEZA BIBI PLOUMEN.

ALIONGEZA KUWA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR WANASUBIRI KWA HAMU KUANZA UJENZI WA WODI MPYA YA KINAMA WAJAWAZITO NA WATOTO KATIKA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA AMBAYO ITAJENGWA KWA UFADHILI WA SERIKALI YA NCHI HIYO KUPITIA MPANGO WA ORIO.

DK. SHEIN ALIUELEZA MSAADA WA NCHI HIYO KATIKA SEKTA YA AFYA KUWA MUHIMU SANA KWA USTAWI WA WANANCHI WA ZANZIBAR NA HIYO INAONESHA JINSI ZANZIBAR NA UHOLANZI ZILIVYO MARAFIKI.

ALIMUELEZA WAZIRI HUYO KUWA AMEPATA FARAJA KUSIKIA KUWA SERIKALI YA UHOLANZI TAYARI IMELETA TIMU YA WATAALAMU HUMU NCHINI KUFANYA UTAFITI WA UWEZEKANO WA UJENZI WA BANDARI ZANZIBAR.

“TUNAHITAJI BANDARI YA KISASA HIVI SASA IWE KWA AJILI YA SHUGHUILI ZA ABIRIA NA MIZIGO AU HATA BANDARI YA MAFUTA NA GESI ZOTE NI MUHIMU KWA MAZINGIRA YA UCHUMI WA ZANZIBAR HIVI SASA” ALISISITIZA DK. SHEIN.

HALIKADHALIKA DK. SHEIN ALIMUELEZA BIBI PLOUMEN KUWA SERIKALI YA ZANZIBAR IMEFURAHISHWA NA TAARIFA KUWA UHOLANZI IMETENGA FEDHA MAALUM KWA AJILI YA KUIJENGEA UWEZO ZANZIBAR KATIKA KUENDELEZA RASILIMALI ZAKE IKIWEMO MAFUTA NA GESI.

KWA HIVYO ALIISHUKURU SERIKALI NA WANANCHI WA UHOLANZI KWA MISAADA YAKE HIYO NA MENGINE AMBAYO IMEKUWA IKICHANGIA NA KUHARAKISHA UFANIKISHAJI WA MALENGO MBALIMBALI YA MAENDELEO NCHINI.

DK. SHEIN ALIMSHUKURU WAZIRI HUYO KWA KUTEMBELEA ZANZIBAR KUFUATIA MAZUNGUMZO YAKE WALIYOFANYA AKIWA NCHINI UHOLANZI MWENZI AGOSTI MWAKA JANA WAKATI ALIPOFANYA ZIARA RASMI NCHINI HUMO.

“NILIFURAHI KUSIKIA UTAFANYA ZIARA NCHINI NA LEO NIMERAFIJIKA ZAIDI KUONA UJIO WAKO UMEAMBATANA NA UJUMBE MZITO WA MAKAMPUNI KUTOKA NCHINI UHOLANZI ”ALIELEZA DK. SHEIN NA KUONGEZA KUWA HATUA HIYO INAFUNGUA UKURASA MPYA WA MATUMAINI NA USHIRIKIANO WA MIAKA MINGI IJAYO KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI.

WAKATI HUO HUO WAZIRI WA BIASHARA ZA NJE WA UHOLANZI BIBI LILIANNE PLOUMEN ALISEMA KUWA SERIKALI YA NCHI YAKE IMEAINISHA MAENEO YA USHIRIKIANO NA ZANZIBAR KUFUATIA ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALIYOIFANYA NCHINI UHOLANZI MWEZI AGOSTI MWAKA JANA.

“TANGU ULIPOFANYA ZIARA YAKO NCHINI KWETU SERIKALI YETU IMEKUWA IKIANGALIA NAMNA BORA YA KUISAIDIA ZANZIBAR KATIKA KUENDELEZA RASILIMALI ZAKE IKIWEMO MAFUTA, GESI PAMOJA NA MIUNDOMBINU YA USAFARI WA BAHARINI IKIWEMO UJENZI WA BANDARI”ALIELEZA BIBI PLOUMEN.

KATIKA KUFANYA HIVYO ALIELEZA KUWA SERIKALI YA NCHI YAKE IMETENGA FEDHA MAALUM KWA AJILI YA MAFUNZO YA KUIJENGEA UWEZO ZANZIBAR KUENDELEZA RASILIMALI ZAKE IKIWEMO SEKTA YA MAFUTA NA GESI.

“TUMEBAINI (SERIKALI YA UHOLANZI)MAENEO YA KUSHIRIKIANA NA MAKAMPUNI UTAKAYOONANA NA LEO(JANA) YANA WELEDI MKUBWA KATIKA MAENEO HAYO AMBAYO NI PAMOJA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA USAFIRI WA BAHARINI, UJENZI WA BANDARI, MAFUTA NA GESI, MAPATO NA KODI KATIKA RASILIMALI NA TAASISI YA MAFUNZO”ALIFAFANUA BIBI PLOUMEN.

ALIELEZA KUWA UJIO WA MAKAMPUNI HAYO KUTOKA NCHINI KWAKE NI SEHEMU YA JITIHADA ZA SERIKALI YA NCHI YAKE NA ZANZIBAR YA KUIMARISHA UHUSIANO BAINA YA SERIKALI ZAO NA USHIRIKIANO BAINA YA SEKTA BINAFSI ZA NCHI MBILI HIZO.


MAZUNGUMZO HAYO YALIHUDHURIA PIA NA BAADHI YA MAWAZIRI NA MKATIBU WAKUU PAMOJA NA KATIBU MKUU KIONGOZI DK. ABDULHAMID YAHYA MZEE.

DOKTA SHEIN AKUTANA NA UJUMBE WA KUTENGENEZA MATREKTA KUTOKA INDIA

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN LEO AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA KAMPUNI YA KUTENGENEZA MATRETA YA MAHINDRA KUTOKA NCHINI INDIA.

ZIARA HIYO YA SIKU MBILI HUMU NCHINI INAFUATIA MWALIKO WA MHESHIMIWA RAIS KWA UONGOZI WA KAMPUNI HIYO WAKATI WA ZIARA YAKE NCHINI INDIAALIYOIFANYA HIVI KARIBUNI.

WAKATI WA ZIARA HIYO DK. SHEIN ALITEMBELEA KIWANDA HICHO NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA JUU WA KAMPUNI HIYO AMBAPO KAMPUNI HIYO ILIKUBALI OMBI LA KUISAIDIA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUENDELEZA KILIMO.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO UONGOZI WA KAMPUNI HIYO ULIAHIDI KUTUMA TUMI YA WATAALAMU NCHINI KUANGALIA NAMNA BORA KAMPUNI HIYO INAWEZA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUENDELEZA KILIMO.

KATIKA MAZUNGUMZO YAKE NA UJUMBE HUO YALIYOFANYIKA IKULU, RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI ALIUSHUKURU UONGOZI WA KAMPUNI YA MAHINDRA KWA KUITIKIA KWA HARAKA WITO WAKE KUTEMBELEA ZANZIBAR KUJUA MAHITAJI YA NCHI KATIKA SEKTA HIYO.

“NI SIKU 14 TU TANGU TULIPOONANA TAREHE 7 FEBRUARI, 2014 MJINI MUMBAI WAKATI WA ZIARA YANGU. KWA KASI HII NINA MATARAJIO MAKUBWA KUWA TUTAWEZA KUFANYA MABADILIKO YA HARAKA KWA WAKULIMA WETU” DK SHEIN ALIUELEZA UJUMBE HUO.

ALIFAFANUA KUWA MWITIKIO HUO WA HARAKA UNADHIHIRISHA PIA UTAYARI WA KAMPUNI YA MAHINDRA YA KUFANYAKAZI NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA KWAMBA KWA UPANDE WAKE ZANZIBAR IMEJIANDAA KUONA NI KWA NAMNA GANI INAWEZA KUJENGA USHIRIKIANO WA MUDA MREFU NA KAMPUNI HIYO KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO NCHINI.

DK. SHEIN ALIUELEZA UJUMBE HUO KUWA ZIARA YAO ITAONA JINSI KILIMO KILIVYOKUWA NA UMUHIMU KATIKA UCHUMI WA ZANZIBAR NA MCHANGO WAKE KATIKA KUINUA KIWANGO CHA MAISHA CHA WANANCHI WA ZANZIBAR.

“TUNATARAJIA MATOKEO YA ZIARA YENU YATAFUNGUA NJIA YA USHIRIKIANO WA MUDA MREFU KATI YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA KAMPUNI YA MAHINDRA KWA KUSAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO” ALISEMA DK. SHEIN.

KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI HIYO BWANA SANJAY JADHAR ALIELEZA KUWA ZIARA YAO HIYO NI MWITIKIO WA WITO WA MHE RAIS ALIUTOA KWA KAMPUNI YAO WAKATI ALIPOITEMBELEA HIVI KARIBUNI.KWA HIVYO WAMEKUJA NCHINI KUANGALIA NAMNA KAMPUNI YAKE INAVYOWEZA KUSAIDIA KUIMARISHA KILIMO NCHINI NA KUBADILI HALI YA WAKULIMA WA ZANZIBAR.

ALIFAFANUA KUWA UJUMBE HUO WAKIWA NA WENYEJI WAO UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO UTAMBELEA SEHEMU MBALIMBALI UNGUJA NA PEMBA YAKIWEMO MASHAMBA, KARAKANA YA MATREKTA PAMOJA NA  KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO.

ALIONGEZA KUWA BAADA YA ZIARA HIYO WATAKUWA NA MAZUNGUMZO YA PAMOJA NA WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI KUHUSU WALICHOKIONA WAKATI WA ZIARA NA KUPANGA NINI LA KUFANYA KUTIMIZA MALENGO YA ZIARA.

UJUMBE WA MAHINDRA ULISHIRIKISHA PIA BWANA SANDESH PARAB MAKAMU WA MKURUGENZI MKUU WA SHUGHULI ZA KIMATAIFA ZA KAMAPUNI HIYO, BWANA G.V. RAO MENEJA WA KANDA AGRO TRACTORS AND IMPLEMENTS NA BWANA MIHID TEREDESAI MENEJA MKUU AGRO TRACTORS AND IMPLEMENTS OFISI YA DAR ES SALAAM.  


MIONGONI MWA WALIOHUDHURIA MAZUNGUMZO HAYO NI PAMOJA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. MWINYIHAJI MAKAME, KATIBU MKUU KIONGOZI DK. ABDULHAMID YAHYA MZEE, MSHAURI WA RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UCHUMI NA UWEKEZAJI BALOZI MOHAMED RAMIA NA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM.

Friday, February 21, 2014

VIJANA WASAHAULIWA BUNGE LA KATIBA

ZANZIBAR

WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KUJADILI RASIMU YA PILI YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAMEOMBWA KUZIANGALIA KWA MAKINI NAFASI ZA VIJANA KATIKA KULETA MCHANGO KWA MAENDELEO YA TAIFA.

AKIZUNGUMZA NA RADIO ADHANA FM MWENYEKITI WA JUMUIYA YA ZANZIBAR YOUTH FORAM NGUGU DADI KOMBO MAALIM AMESMA KATIKA UTEUZI WA WABUNGE WA BUNGE HILO WANAOHUSIKA NA UTEUZI HAWAKUANGALIA NAFASI YA VIJANA NA KUSAHAU KUWA WANADHAMANA NA FUNGU KUBWA KATIKA KUISIMAMIA KATIBA HIYO.

AMSEMA KUWA KWA MUJIBU WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA ELFU MBILI NA KUMI IDADI YA VIJANA NI KUBWA ZAIDI YA ASILIMIA 52.4 KATIKA UTEUZI HUO VIJANA WALIPASWA KUPEWA KIPAOMBELE  KUPITIA TAASISI ZAO LAKINI CHA KUSIKITISHA HAWAKUCHAGULIWA KATIKA NAFASI ZA KUPITIA  MAKUNDI MAALUM.


AMEWEKA WAZI YA KUWA KUTOKANA NA HALI HIYO ENDAPO VIJANA WATAONA MASLAHI YAO HAYAKUZINGATIWA KATIKA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUNAWEZA KUZUKA MGOGORO MKUBWA NA  HATA KUPELEKEA KUFELISHA ZOEZI ZIMA LA UPATIKANAJI WA KATIBA HIYO KWA KUKATAA KWENYE HATUA YA UPIGAJI WA KURA KWA KUTUMIA WINGI WAO.

AFP WAIOMBA SERIKALI KUWAONGEZA MSHAHARA WAFANYA KAZI

ZANZIBAR

MWEYEKITI WA CHAMA CHA WAKULIMA ZANZIBAR (AFP) NDUGU SOUD SAID SOUD AMEIOMBA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUWAONGEZEA MSHAHARA WAFANYAKAZI WANAOPOKEA MSHAHARA WA KIMA CHA CHINI ILI WAWEZE KUJIKIMU KATIKA MAISHA YAO YA KILA SIKU.

MWENYEKITI SOUD AMEYASEMA HAYO WAKATI ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA RADIO ADHANA FM KUHUSIANA NA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI  WA ZANZIBAR.

AMESEMA HALI YA MAISHA YA ZANZIBAR INAKUWA GUMU SIKU HADI SIKU HIVYO IWAPO SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ITAWEZA KUWAONGEZEA WAFANYAKZI WA KIWANGO CHA CHINI MSHAHARA WATAWEZA KUKABILIANA NA UGUMU WA MAISHA.

AMEFAFANUA KUWA HALI HIYO YA UGUMU WA MAISHA IMESABABISWA NA SERIKALI KUPANDISHA BEI MAMBO MUHIMU KAMA VILE UMEME,MAJI  NA CHAKULA BILA KUZINGATIA HALI ZA WATU.


SAMBAMBA NA HAYO AMESEMA KUWA MAISHA YA ZANZIBAR KWA WAKATI HUU NI MAGUMU HAKUNA BUDI KWA SERIKALI KUBUNI MBINU BORA ZA KUBORESHA MAISHA YA WAZANZIBARI HUSUSAN WA VIJIJINI.

Saturday, February 15, 2014

MAAZIMIO KUMI NA MBILI YAJADILIWA OIC

TEHERAN
KAMATI MAALUMU ZA UMOJA WA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA USHIRIKIANO WA KIISLAMU OIC ZIMEPITISHA MAAZIMIO 12 YA AJENDA ZA MKUTANO WA TISA WA MASPIKA WA MABUNGE WA NCHI WANACHAMA UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMANNE NA JUMATANO  MJINI TEHRAN.
KAZEM JALALI, MSEMAJI WA MKUTANO WA TISA WA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA OIC AMESEMA, KAMATI MAALUMU ZA UMOJA WA MABUNGE YA KIISLAMU ZIMEJADILI NA KUPASISHA MAAZIMIO 12 KUPITIA KAMATI NNE ZA SERA ZA NJE, WANAWAKE, PALESTINA NA MASPIKA WA MABUNGE.
JALALI AMEONGEZA KUWA KAMATI HIZO ZIMEJADILI PIA JINSI YA KUZIDISHA MSHIKAMANO NA KUIMARISHA ZAIDI UMOJA KATI YA NCHI ZA KIISLAMU, KUPAMBANA NA TAASUBI NA UENEZAJI HOFU JUU YA UISLAMU NA KUPAMBANA NA VITENDO VYA KUFURUTU MPAKA KAMA ILIVYOPENDEKEZWA NA RAIS WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN KATIKA UMOJA WA MATAIFA NA KUPASISHWA NA BARAZA KUU LA UMOJA HUO, NA ZIKAPONGEZA PIA JUHUDI ZILIZOFANYWA NA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN.

JALALI AMEONGEZA KUWA AZIMIO MUHIMU ZAIDI LILILOPASISHWA NA KAMATI YA SERA ZA NJE ZA UMOJA WA MABUNGE YA OIC NI KUPAMBANA NA UGAIDI, KUTILIA MKAZO HAKI YA KISHERIA YA MAPAMBANO NA MUQAWAMA DHIDI YA UVAMIZI NA UKALIAJI WA MABAVU, KULAANI VIKWAZO VYA KILA AINA DHIDI YA NCHI ZA KIISLAMU NA SISITIZO JUU YA HAKI YA NCHI NA MATAIFA YOTE YA KUJIPATIA TEKNOLOJIA MPYA NA KUZITUMIA TEKNOLOJIA HIZO KWA MALENGO YA AMANI.

UNGANDA USHOGA KWISHA

KAMPALA
RAIS YOWERI MUSEVENI WA UGANDA AMESEMA KUWA, ATASAINI MUSWADA WA KUPIGA MARUFUKU VITENDO VICHAFU VYA NDOA ZA WATU WA JINSIA MOJA NCHINI HUMO.
MUSWADA AMBAO KAMA UTASAINIWA NA KUWA SHERIA UTAWAPA ADHABU YA KIFUNGO CHA MAISHA JELA WATU WATAKAOPATIKANA WAKIJIHUSISHA NA VITENDO HIVYO.
OFWONO OPONDO, MSEMAJI WA SERIKALI YA UGANDA AMESEMA KUWA, RAIS MUSEVENI AMETANGAZA UAMUZI HUO KATIKA MKUTANO WA CHAMA TAWALA CHA NRM.
OPONDO AMESEMA KWAMBA, UAMUZI WA RAIS MUSEVENI UMETEGEMEA RIPOTI YA WATAALAMU WA MASUALA YA TIBA AMBAYO INAONESHA KUWA, LIWATI NA USAGAJI SIO SUALA LA KIMAUMBILE, BALI CHIMBUKO LAKE NI TABIA YA MTU.
WIKI MBILI ZILIZOPITA RAIS MUSEVENI ALISEMA KUWA, ANGESAINI MUSWADA HUO NA KUWA SHERIA BAADA YA KUPATA MTAZAMO WA WATAALAMU.
MUSWADA HUO UNAOPIGA MARUFUKU NDOA ZA WATU WA JINSIA MOJA NA AMBAO ULIPIGIWA MAKELELE NA MADOLA YA MAGHARIBI PAMOJA NA MASHIRIKA YA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU ULIPASISHWA NA BUNGE LA UGANDA DISEMBA MWAKA JANA.
HATA HIVYO MWEZI ULIOPITA WA JANUARI RAIS MUSEVENI ALISEMA KWAMBA, MUSWADA HUO ULIPASISHWA BILA YA IDADI INAYOTAKIWA BUNGENI KWA AJILI YA KUPASISHA MUSWADA.

BADO HAIJAJULIKANA RAIS MUSEVENI ATAUSAINI LINI MUSWADA HUO ILI UWE SHERIA.

MBUNGE WA CHAMBANI ATEKELEZA AHADI ZAKE KISARAWE NA BAGAMOYO

DAR ES SALAAM                            

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEWAKUMBUSHA VIONGOZI WA MAJIMBO KUTEKELEZA AHADI WANAZOZITOA KWA WANANCHI, ILI KUJIJENGEA UAMINIFU KATIKA MAENEO YAO.

MAALIM SEIF AMETOA KAULI HIYO KATIKA OFISI KUU YA CUF BUGURUNI, BAADA YA KUPOKEA PIKIPIKI MBILI KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO LA CHAMBANI MHE. YUSSUF SALIM HUSSEIN (CUF), KWA AJILI YA WILAYA ZA KISARAWE NA BAGAMOYO.

AMESEMA KUKABIDHIWA KWA PIKIPIKI HIZO ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI TATU NA LAKI MBILI, KUNAONESHA JINSI MBUNGE HUYO ANAVYOFUATILIA NA KUTEKELEZA AHADI ZAKE KWA WANANCHI, NA KUTAKA VIONGOZI WENGINE WAIGE MFANO WA MBUNGE HUYO.

MBUNGE HUYO WA CHAMBANI AMEKABIDHI PIKIPIKI HIZO KUFUATIA AHADI ALIYOITOA KWA WANANCHI WA WILAYA ZA KISARAWE NA BAGAMOYO, AKIWA KATIKA ZIARA YA KATIBU MKUU WA CHAMA HICHO MWEZI ULIOPITA.

AKIZUNGUMZA BAADA YA KUKABIDHI PIKIPIKI HIZO MHE. YUSSUF AMESEMA AMEAMUA KUTEKELEZA AHADI HIYO KWA MUDA MFUPI, ILI KUJENGA MATUMAINI YA WANACHAMA KWA VIONGOZI NA CHAMA CHAO.


AMESEMA ATAENDELEA KUTEKELEZA AHADI ALIZOZITOA KWA WANANCHI KATIKA MAENEO MBALI MBALI, ILI KUHAKIKISHA KUWA CHAMA HICHO KINAZIDISHA MATUMAINI KWA WANACHAMA WAKE NA WANANCHI KWA UJUMLA.

Saturday, February 8, 2014

UNAKIJUA ALICHOZUNGUMZA MAALIM SEIF PEMBA


PEMBA

 

KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF, MAALIM SEIF SHARIF HAMAD AMEWATAKA WANACHAMA NA VIONGOZI WA CHAMA CUF WASIVUNJIKE MOYO NA MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KIEMBESAMAKI NA BADALA YAKE WAENDELEE NA JUHUDI ZA KUKIIMARISHA CHAMA, ILI KIWEZE KUKAMATA DOLA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MWAKANI.

 

AKIFUNGUA MKUTANO WA VIONGOZI WA MATAWI, MAJIMBO NA WILAYA KWA WILAYA ZA WETE NA MICHEWENI ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI WETE, MAALIM SEIF AMESEMA KILICHOTANGAZWA KIEMBESAMAKI SI MATAKWA YA WANANCHI, KWA VILE  KIMSINGI WANANCHI WA JIMBO HILO WALISUSIA UCHAGUZI HUO.

 

MAALIM SEIF AMESEMA IDADI KUBWA YA WAPIGA KURA WALIOSHIRIKI KATIKA UCHAGUZI HUO SI WAKAAZI WA ENEO HILO, AMBAO WALICHUKULIWA KATIKA MAENEO MBALI MBALI, BAADA YA KUBAINIKA WANANCHI WENYEWE HAWATASHIRIKI KWA SABABU HAWAKURIDHISHWA NA MAAMUZI YALIYOCHUKULIWA HADI KUFANYIKA UCHAGUZI HUO.

“KAMA KUNA WANANCHI WA KIEMBESAMAKI WALIOKWENDA KUPIGA KURA BASI HAWAZIDI 1000, WENGI WALICHUKULIWA KATIKA MAENEO TAFAUTI, KAMA VILE MAKUNDUCHI, MTENDE, KITOPE NA BUMBWINI NA WAKAPELEKWA KUPIGA KURA HUKU WAKILINDWA NA VIKOSI VYA SERIKALI”, ALISEMA MAALIM SEIF.

 

AMESEMA MBALI NA HAYO KUNA BAADHI YA WANANCHI WA KIEMBESAMAKI WALIPEWA VITISHO KABLA YA KUFANYIKA UCHAGUZI HUO, KWA KUTUMIWA UJUMBE UNAOWAONYA WASIJITOKEZE KWENDA KUPIGA KURA, VYENGINEVYO WATAPATWA NA MATATIZO MAKUBWA.

 

KATIKA UCHAGUZI HUO MDOGO WA KIEMBESAMAKI AMBAO ULIOFANYIKA FEBRUARI 2, MWAKA HUU, BAADA YA ALIYEKUWA MWAKILISHI WA JIMBO HILO, MANSOUR YUSSUF HIMID KUFUKUZWA UANACHAMA WA CCM, MGOMBEA WA CCM, MAHMOUD THABIT KOMBO ALITANGAZWA MSHINDI, AMBAPO VILE VILE IDADI KUBWA YA WAPIGA KURA HAWAKUJITOKEZA KWENDA KUPIGA KURA.

 

AKIZUNGUMZIA KATIBA MPYA, MAALIM SEIF AMEWAHIMIZA WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KUWEKA KANDO MASLAHI YA VYAMA AU MAKUNDI YAO, NA BADALA YAKE WAHAKIKISHE TANZANIA INAKUWA NA MUUNGANO WA HAKI, AMBAPO WAZANZIBARI NA WATANGANYIKA KILA UPANDE URIDHIKE KUWA UNAPATA HAKI SAWA NA MWENGINE.

“KWA UPANDE WETU WAZANZIBARI TUSISAHAU TUNA KILIO KIKUBWA CHA MIAKA MINGI KUTOTENDEWA HAKI NDANI YA MUUNGANO HUU, WAJUMBE WOTE WAJALI MASLAHI YA ZANZIBAR NA WAWEKE PEMBENI MASLAHI BINAFSI AU YA VYAMA VYAO”, ALIONYA MAALIM SEIF.

KUHUSU UCHAGUZI MKUU UNAOENDELEA NDANI YA CUF, KATIBU MKUU HUYO AMESEMA KWA WALE VIONGOZI AMBAO TAYARI WAMECHAGULIWA KATIKA NGAZI ZA MATAWI NA MAJIMBO WAJIEPUSHE NA TABIA YA KUWATENGA WALE AMBAO HAWAKUSHINDA, NA WAFANYEKAZI KWA PAMOJA KWA AJILI YA KUKIIMARISHA ZAIDI CHAMA.

AMESEMA KITENDO CHA KUWATENGA WALIOSHINDWA KATIKA SHUGHULI ZA KICHAMA ITAKUWA NI DHAMBI KUBWA AMBAYO ITASABABISHA MIFARAKANO NA KUPELEKEA HATA HAO WALIOSHINDA WASIWEZE KUFANYA KAZI KWA UFANISI NA MATOKEO YAKE NI KUDHOROTA UFANISI KATIKA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA CHAMA.

MAPEMA, NAIBU KATIBU MKUU WA CUF ZANZIBAR, HAMAD MASOUD AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO AMESEMA MATUMAINI YA USHINDI WA CHAMA HICHO YAPO KWA VIONGOZI HAO WAPYA, HIVYO WAJIPANGE VIZURI NA WADUMISHE MASHIRIKIANO YA HALI YA JUU NA HATIMAYE WAKIPE USHINDI CHAMA CHAO.

WIZARA ZA KATIBA NA SHERIA ZATAKIWA KUSHIRIKIANA


MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEZITAKA WIZARA ZA KATIBA NA SHERIA TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA ILI KUFANIKISHA SEHEMU ILIYOBAKIA YA MCHAKATO WA KATIBA.

AMESEMA TOKEA ZOEZI HILO LILIPOANZA, WIZARA YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMEKUWA IKISHIRIKIANA KWA KARIBU NA WIZARA YA KATIBA YA ZANZIBAR, HALI ILIYOLETA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA MCHAKATO HUO, HADI KUPATIKANA KWA RASIMU YA PILI AMBAYO ITAANZA KUJADILIWA KWENYE BUNGE LA KATIBA HIVI KARIBUNI.

MHE. MAALIM SEIF AMETOA MAELEZO HAYO NYUMBANI KWAKE MBWENI, WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. ASHA ROSE MIGIRO.

“HAPA TULIPOFIKA NI KUTOKANA NA MASHIRIKIANO MAZURI YA WIZARA ZETU ZA KATIBA, HIVYO NI VYEMA MASHIRIKIANO NA MASHAURIANO YAKAENDELEA ILI KUMALIZA NGWE ILIYOBAKIA KWA SALAMA NA AMANI, NA HATIMAYE KUPATA KATIBA MPYA ITAKAYORIDHIWA NA WATANZANIA”, ALITANABAHISHA MAALIM SEIF.

HATA HIVYO AMEMSHAURI WAZIRI MIGIRO KUKAA PAMOJA NA WAZIRI MWENZAKE WA ZANZIBAR MHE. ABUBAKAR KHAMIS BAKARI, KUANDAA MAZINGIRA YA KUFIKIA MAKUBALIANO KWENYE BUNGE LA KATIBA, IWAPO ZITATOKEA KASORO KWENYE MIJADALA YA BUNGE HIYO.

AIDHA AMEWASHAURI MAWAZIRI HAO WA KATIBA KUANDAA MAPENDEKEZO YA KANUNI ZA BUNGE LA KATIBA, ILI WAJUMBE WAWEZE KUYAPITIA NA KUYAREKEBISHA, BADALA YA KUSUBIRI BUNGE LENYEWE KUANDAA KANUNI, HATUA AMBAYO INAWEZA KUCHUKUA MUDA MWINGI WA VIKAO VYA BUNGE.

AMEMPONGEZA WAZIRI MIGIRO KWA KUTEULIWA KUSHIKA WADHIFA HUO, NA KUELEZEA MATUMAINI YAKE JUU YA UTENDAJI BORA WA KAZI ZAKE.

NAE MHE. ASHA ROSE MIGIRO AMBAYE ALIFIKA KWA AJILI YA KUJITAMBULISHA, AMEMUHAKIKISHIA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS KUWA MASHIRIKIANO YALIYOKUWEPO BAINA YA WIZARA HIZO YATAENDELEZWA KWA KARIBU ZAIDI, ILI KUWAWEZESHA WATANZANIA KUPATA KATIBA WANAYOITAKA.

AMESEMA NCHI IKO KATIKA HIPINDI MUHIMU CHA KUKAMILISHA MCHAKATO WA KATIBA, HIVYO UMAKINI ZAIDI UNAHITAHITAJIKA KATIKA KUFANIKISHA HATUA HIYO.

AMEAHIDI KUUFANYIA KAZI USHAURI ALIOPEWA, ILI KUHAKIKISHA KUWA MALENGO YA WATANZANIA YA KUPATA KATIBA MPYA YANAFIKIWA KWA MUDA ULIOPANGWA.

MAALIM SEIF AKUTANA NA BALOZI MPYA WA TZ NCHINI MALAYSIA


MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEKUTANA NA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA DR. AZIZ PONELA MLIMA, NA KUMSISITIZA KUENDELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI, ILI KUKUZA UCHUMI WA ZANZIBAR NA TANZANIA KWA UJUMLA.

AMESEMA NCHI ZA ASIA ANAZOKWENDA KUIWAKILISHA TANZANIA ZIKIWEMO MALAYSIA, INDONESIA, PHILIPPINES, LAOS, BRUNEI NA CAMBODIA, NI MIONGONI MWA NCHI ZINAZOKUA KIUCHUMI KATIKA UKANDA HUO, NA KUMTAKA KUTUMIA FURSA HIYO KUITANGAZA ZANZIBAR HASA KATIKA SEKTA ZA UTALII, UVUVI NA VIWANDA VIDOGO VIDOGO.

AKIZUNGUMZA NA BALOZI HUYO NYUMBANI KWAKE MBWENI, MAALIM SEIF AMESEMA MABALOZI WANA NAFASI KUBWA YA KUTANGAZA FURSA ZA KIUCHUMI NA UWEKEZAJI TANZANIA, NA KUTAKA KUWASHAJIISHA WAWEKEZAJI WA NCHI HIZO KUJA KUWEKEZA ZANZIBAR.

AKIZUNGUMZIA KUHUSU SEKTA YA UTALII, MAALIM SEIF AMESEMA UKANDA HUO WA NCHI ZA ASIA UMEKUWA UKITOA WATALII WENGI KWENDA NCHI ZA KIGENI, LAKINI BADO TANZANIA HAIJAWEZA KUITUMIA KIKAMILIFU FURSA YA KUJITANGAZA KWA NCHI HIZO.

AMESEMA WAKATI UMEFIKA KWA MABALOZI KUWEKA WAZI  MIKAKATI YA TANZANIA KATIKA KUKUZA UCHUMI WAKE, IKIWA NI PAMOJA NA KUTANGAZA FURSA ZA KIUCHUMI, BIASHARA NA UWEKEZAJI.

KWA UPANDE WAKE BALOZI HUYO WA TANZANIA NCHINI MALAYSIA DR. AZIZ MLIMA, AMEAHIDI KUTUMIA FURSA HIYO KUITANGAZA TANZANIA ILI IWEZE KUKUZA UCHUMI NA UHUSIANO WAKE NA NCHI HIZO.

dokta sheni akutana na kampuni ya utengenezaji magari na zana za kilimo


KAMPUNI YA KUTENGENEZA MAGARI NA ZANA ZA KILIMO YA MAHIDRA YA MJINI MUMBAI, INDIA IMEKUBALI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUINUA KIWANGO CHA UZALISHAJI WA MAZAO YA KILIMO NCHINI ILI HATIMAE KUFIKIA LENGO LA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA IFIKAPO MWAKA 2020.

 

MTENDAJI MKUU WA HUDUMA ZA KIMATAIFA WA KAMPUNI HIYO BWANA RUZBEN IRANI AMESEMA HAYO WAKATI WA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ULIOONGOZWA NA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMBAYE ALITEMBELEA KIWANDA HICHO.

 

BWANA IRANI ALISEMA KAMPUNI YAKE INAAFIKI MAOMBI YA RAIS WA ZANZIBAR LA KUTAKA KAMPUNI YAKE ISAIDIE SEKTA YA KILIMO ILI IWEZE KUFIKIA MALENGO YA DIRA YA ZANZIBAR 2020 NA MKUZA II.

 

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN ALIITAKA KAMPUNI HIYO KUUNGA MKONO MAPANGO WA SERIKALI WA KULETA MAPINDUZI YA KIJANI ILI KUZALISHA MAHITAJI YA CHAKULA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO MWAKA 2015/2016 IKIWA NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI WA DIRA YA MAENDELEO ZANZIBAR 2020 AMBAYO INAELEKEZA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA IFIKAPO MWAKA 2020.

 

KATIKA KUTEKELELEZA MPANGO HUO ALIELEZA KUWA SERIKALI IMEKUWA IKITOA RUZUKU KWA WAKULIMA KWA KUWAPATIA PEMBEJEO NA ZANA ZA KILIMO LAKINI CHANGAMOTO KUBWA IMEKUWA MAHITAJI MAKUBWA YA ZANA ZA KILIMO HUSUSAN MATREKTA.

 

ALIBAINISHA KUWA DHAMIRA YA SERIKALI NI KUHAKIKISHA INABORESHA MAISHA YA WANANCHI WAKE WAKIWEMO WAKULIMA AMBAO NJIA BORA KWAO NI KUWAONDOA KUTOKA KILIMO ZA ZAMANI HADI MATUMIZI YA TEKINOLOJIA YA KISASA ILI KUONGEZA TIJA KATIKA UZALISHAJI NA HATIMAE KUONDOKANA NA UMASIKINI.

 

ALIFAFANUA KUWA KUWAWEZESHA WAKULIMA NCHINI NA KUFIKIA HATUA HIYO KUNAKWENDA SAMBAMBA NA LENGO KUU YA DIRA YA ZANZIBAR YA KUIFANYA ZANZIBAR KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI IFIKAPO MWAKA 2020.

 

DK. SHEIN ALIUELEZA UONGOZI WA KAMPUNI HIYO KUWA ZIARA YAKE KATIKA KIWANDA HICHO AMBAYO NI YA PILI, MARA YA KWANZA IKIWA NI MWAKA 2008 AKIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, INAONESHA KUTHAMINI UTAALAMU NA UWEZO WA KAMPUNI HIYO KATIKA KUENDELEZA KILIMO NA KUMUENDELEZA MKULIMA MBAYE NDIE MLENGWA MKUU.

 

ALIELEZA KUWA AMEFURAHISHWA NA MIKAKATI YA KAMPUNI HIYO YA KUSAIDIA WAKULIMA IKIWEMO SUALA LA UTAFITI AMBALO ALIELEZA KUWA NI LA MSINGI HIVYO KUELEZA KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INGEPENDA PIA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI HIYO KATIKA ENEO HILO KUPITIA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO ZANZIBAR.

 

KATIKA KUTEKELEZA WITO WA RAIS, BWANA IRANI ALIELEZA KUWA KWA KUANZIA KAMPUNI YAKE ITATUMA TIMU YA WATAALAMU HIVI KARIBUNI ILI KUFANYA UTAFITI KUJUA MAHITAJI, AINA YA ZANA PAMOJA NA NYENZO NYINGINE MUHIMU ZA KILIMO ZINAZOHITAJIKA KWA MUJIBU WA MAZINGIRA YA ZANZIBAR.

 

ALIFAFANUA KUWA ILI KUPATA MATOKEO MAZURI MIONGONI WA WATAALAMU WATAOKWENDA ZANZIBAR NI WA KUFANYA UTAFITI WA UDONGO KUFAHAMU AINA YA UDONGO NA KUJUA HATUA ZA KITAALAMU ZINAZOTAKIWA KUCHUKULIWA KUONGEZA TIJA KATIKA UZALISHAJI NA PIA KUJUA AINA YA MATREKTA YANAYOLINGANA NA MAZINGIRA YA ZANZIBAR.

 

BWANA IRANI ALIONGEZA KUWA KAMPUNI YAKE INA KILA SABABU YA KUZIUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KULETA MAPINDUZI YA KILIMO KWA KUWA INAAMINI KUWA MAFANIKIO YAKE YATAKUWA MFANO KWA NCHI NYINGINE BARANI AFRIKA.

 

ALISISITIZA KUWA KAMPUNI YAKE ITAJIDHATITI KUTEKELEZA WAJIBU WAKE HARAKA IWEZEKANAVYO KWA KUWA MIAKA 6 KABLA YA KUFIKIA 2020 KULIFIKIA LENGO LA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA KUTOKA ASILIMIA 20 YA SASA HADI 100 NI CHANGAMOTO LAKINI AKAMUHAKIKISHIA HILO LINAWEZAKANA KWA KUWA NIA NA DHAMIRA NDIO MUHIMU.

 

AKIWA KIWANDANI HAPO DK. SHEIN NA UJUMBE WAKE ULITEMBELEA SEHEMU YA KUUNGANISHA INJINI ZA MATREKTA PAMOJA NA SEHEMU YA KUUNGANISHA MATREKTA TAYARI KWA KUPELEKWA KWENYE MASOKO.

ALIPATA FURSA PIA YA KUONA AINA MBALIMBALI ZA MATREKTA YANAYOTENGENEZWA NA KAMPUNI HIYO PAMOJA NA MAGARI NA PIKIPIKI. KAMPUNI HIYO HIVI KARIBUNI IMETOA TREKTA MPYA DOGO AINA YA YUVRAJ 215 LENYE NGUVU ZA 15-20 HP AMBALO LINAWEZA KUFANYA KAZI ZOTE KILIMO PAMOJA NA SHUGHULI NYINGINE ZISIZOKUWA ZA KILIMO.

KAMPUNI YA MAHINDRA AMBAYO ILIANZISHWA MWAKA 1945 NI KAMPUNI INAONGOZA ULIMWENGUNI KATIKA KUTENGENEZAJI MATREKA NA ZANA ZA KILIMO IKIWA NA SOKO KATIKA NCHI ZA ULAYA, MAREKANI, ASIA NA AFRIKA. MBALI YA MATREKTA INATENGENEZA MAGARI YA AINA MBALIMBALI PAMOJA NA PIKIPIKI.

KAMPUNI HIYO INAFANYA PIA INAFANYA TAFITI MBALIMBALI KATIKA KILIMO NA IMEKUWA MSTARI MBELE KATIKA KUBUNI NA KUENDELEZA TEKINOLOJIA RAHISI KWA WAKULIMA WA INDIA NA SASA IMEINGIA KATIKA MASOKO YA NJE.

DK. SHEIN AMBAYE AMBAYE YUKO NCHINI INDIA KWA ZIARA YA SIKU TISA ANAENDELEA NA ZIARA YAKE LEO KWA KUTEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA VIUNGO(SPICES) NA BAADAE ATAFANYA MAZUNGUMZO YA WAFANYABIASHARA WA VIUNGO HAPA MUMBAI.

KATIKA ZIARA HIYO DK. SHEIN AMEFUATANA NA MKE WAKE MAMA MWANAMWEMA, WAZIRI WA FEDHA OMAR YUSUF MZEE, WAZIRI WA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO BIBI ZAINAB OMAR MOHAMED, WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA NA MASOKO NASSOR AHMED MARZUI, NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DK. MAHADHI JUMA MAALIM NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA INJINIA JOHN KIJAZI.

WENGINE KATIKA MSAFARA HUO NI KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MOHAMED SALEH JIDAWI NA KATIBU MKUU KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM, MSHAURI WA RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UWEKEZAJI NA UCHUMI BALOZI MOHAMED RAMIA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA UWEKEZAJI ZANZIBAR –ZIPA SALUM KHAMIS NASSOR.

Tuesday, February 4, 2014

Saratani ya tezi dume au Prostate Cancer

Ni matumaini yangu kuwa hamjambo , karibuni katika kipindi kingine cha Ijue Afya Yako. Kama tulivyoahidi wiki hii tutazungumzia ugonjwa wa kansa ya tezi tume au Prostate Cancer kwa kimombo unaosababisha vifo vingi vya wanaume duniani kote. Ili kuujua vyema ugonjwa huo tafadhali usiondoke kando ya redio yako hadi mwisho wa kipindi.
&&&&&&&&
Saratani ya tezi dume inashika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, satarani ya tezi dume kwa sasa inawapata sana wanaume kuanzia miaka 25. Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu kwanza tujue tezi dume ni zipi. Kama tulivyosema neno saratani ni jina la gonjwa ambalo hutokea wakati chembe chembe za uhai au seli katika sehemu fulani ya mwili zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili na kutengeneza vijiuvimbe vidogo vidogo. Kwa kawaida seli huwa zinajigawa, kupevuka na baadaye kufa kwa kufuata taratibu za mfumo wa mwili. Lakini seli za saratani hazifuati mfumo huo. Badala ya kufa, zenyewe huishi muda mrefu kuliko chembe chembe za kawaida na wakati huo huo huendelea kutengeneza seli nyingine na kuwa uvimbe wa saratani au tumour. Tezi dume linapatikana katika mwili wa mamalia dume tu na pale seli katika kiungo hicho zinapoanza kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili hapo ndipo mtu hupata saratani ya tezi dume. Ugonjwa huu pia hujulikana kama saratani ya kipofu cha mkojo. Saratani ya tezi dume huwapata wanaume tu na hasa wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Kutokana na tafiti mbali mbali, saratani hii imethibitika kushika nafasi ya pili, ukiachia mbali saratani ya mapafu kwa kusababisha vifo vya wanaume wenye umri wa takribani miaka 50 na kuendelea. Tafiti za Chama cha Saratani cha Marekani (ACS) na cha Afrika Kusini (CANSA) zimebaini kuwa, mwanaume mmoja kati ya sita hupata saratani ya tezi dume katika uhai wake.  Kutokana na takwimu za mwaka 2010 za dunia nzima, malaria iliua watu laki tano, kifua kikuu watu milioni 2.1, Ukimwi watu milioni 1.8 na saratani watu milioni 9.9. Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani ni kubwa ikilinganishwa na ya magonjwa mengine. Dk Emmanuel Kandusi ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo, na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya '50 Plus Campaign' anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Ameongeza kuwa, kutokana na ugonjwa huo kuwa hatari nchini humo, ifikapo mwaka 2020 unatarajiwa kuua watu milioni 20.
&&&&&&&
Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake: Kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea. Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika hatarini ya kupata kansa hiyo kutokana na kurithi jeni za ugonjwa huo. Suala jingie ni lishe ambapo wanaume wanaopenda kula nyama au (red meat) na walaji wa chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama huwa katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume. Vilevile wataalamu wanatumbia kuwa, wanaume wasiopenda kufanya mazoezi, wanene na wenye upungufu wa virutubisho vya Vitamin E pia wako kwenye hatari zaidi ya kupata saratani ya kibofu cha mkojo. Wanaume wengine walio katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume ni pamoja na wale wenye asili ya Afrika (Weusi) ikilinganishwa na wazungu, wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea za kemikali, wanaofanya kazi katika viwanda vya kutengeneza matairi na wachimbaji madini, hususan aina ya cadmium.
Hayo yote yakiwa ni tisa, kumi ni je, dalili za saratani ya tezi dume ni zipi?Katika hatua zake za awali, dalili za saratani ya tezi dume hazitofautiani na zile za kuvimba kwa tezi dume au BPH. Dalili hizo ni pamoja na, 1) Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa. 2) Kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa. 3) Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu. 4) Kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku. 5) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote na 6) kutoa mkojo uliochanganyika na damu. Pamoja na kueleza dalili hizo wapenzi wasikilizaji wanapashwa kutambua kuwa, mwanaume anapoanza kuona na kuhisi baadhi ya dalili hizo, anapaswa kujua kuwa, seli za saratani katika tezi dume lake huwa zina umri wa takribani miaka saba na kuendelea.
Iwapo saratani imesambaa mwilini kiasi cha kuhusisha sehemu nyigine za mwili, mgonjwa anaweza kuwa na maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni. Aidha mgonjwa huwa na dalili nyingine zinazoweza kumpata mgonjwa mwingine yeyote wa saratani kama vile kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu na kadhalika.
&&&&&&&&&&
Wanaume wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya kibofu cha mkojo au prostate cancer kwa kuwa imegundulika kuwa wanaume wengi wakiziona na kuzihisi dalili hizo huona soni kwenda kumwona daktari na kufanyiwa uchunguzi. Baadhi ya watu huzihusisha na magonjwa ya zinaa au na dhana potofu za kishirikina. Wapo wanaokwenda mbali zaidi hata kuuita ugonjwa huo kuwa ni wa walawiti huku wengine wakiurahisisha kwa kuuita kuwa ni ugonjwa wa utu uzima kana kwamba saratani ya tezi dume ni jambo la kawaida kwa watu wazee. Mambo kama hayo hupelekea wanaume wengi kujinyanyapaa wenyewe na hata wengine kujitibu kwa uficho au kwa kutumia waganga wababaishaji mpaka pale mambo yanapokuwa yamewazidi ndipo hupelekwa mahospitalini na mara nyingine huwa wamechelewa na kupoteza maisha yao bure kwa ugonjwa ambao ungeweza kutibiwa mapema. Kwa ajili hiyo tunatoa wito kwa wanaume kutoona soni na kuwa na tabia ya kufanyiwa uchunguzi wa afya kwa ujumla, na hasa tezi dume angalau mara moja kwa mwaka.
Kuna vipimo viwili ambavyo daktari anaweza kumpima mwanaume ikiwa ni hatua ya kwanza ya kugundua ugonjwa huo. Vipimo hivyo vya kwanza ni "Digital Rectal Exam (DRE)" na cha pili ni "Prostate Specific Antigen (PSA)". DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume, lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au uvimbe katika tezi dume. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa. Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile transrectal ultrasound au prostatic needle biopsy. Tukumbuke kuwa kuwahi kugundua saratani mapema kabla ya dalili, kuna faida kubwa kwa muathirika kwani saratani ikigundulika mapema ni rahisi kutibika.
&&&&&&&&&&
Wapenzi Wasomaji wa kipindi hiki tokea mwanzoni mnajiuliza iwapo saratani ya tezi dume inatibika au la. Jibu ni ndiyo na kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani itumike unategemea ushauri na maoni ya daktari kulingana na hatua ya ugonjwa ulipofikia na umri wa mgonjwa husika. Katika hatua za awali za ugonjwa, daktari anaweza kushauri mgonjwa atibiwe kwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi. Hii ni katika hali ambayo kwa wagonjwa wazee, daktari anaweza kushauri mgonjwa kuwa chini ya uangalizi tu bila kufanyiwa upasuaji au bila kupatiwa tiba ya mionzi.
Iwapo saratani imesambaa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu au hormonal therapy, au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).  Naam wasikilizaji wapenzi hatuna la ziada kwa leo bali tukumbuke kuwa, saratani ya tezi dume ni ugonjwa  wa kawaida kama yalivyo magonjwa mengine na uchunguzi  na matibabu ya mapema huweza kuokoa maisha ya waathirika wengi wa ugonjwa huo.  Basi hadi wiki ijayo panapo maajaaliwa, ahsanteni kwa kututegea sikio na kwaherini.

RAIS SHEN NA MAKAMO WA RAISI WA INDIA WAFANYA MAZUNGUMZO


TANZANIA NA INDIA ZIMEELEZA KURIDHISHWA NA UHUSIANO NA USHIRIKIANO ULIOPO BAINA YAO NA KUSISITIZA DHAMIRA YA KWELI YA KUONA KUWA USHIRIKIANO HUO UNAZIDI KUIMARIKA KWA MANUFAA YA SERIKALI NA WANANCHI WA NCHI HIZO.

HAYO YAMEJITOKEZA JANA WAKATI WA MAZUNGUMZO KATI YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN NA MAKAMU WA RAIS WA INDIA MOHAMED HAMID ANSARI.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO VIONGOZI HAO WAMESEMA KUWA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA KATI YA NCHI HIZO ULIOANZISHWA MWANZONI MWA MIAKA YA SITINI UMEKUWA UKIIMARIKA MWAKA HADI MWAKA KWA KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA UCHUMI NA KIJAMII.

WAMEELEZA KUWA ZIARA ZA VIONGOZI WA NCHI HIZO PAMOJA NA ZIARA ZA MARA KWA MARA KATIKA NGAZI YA MAWAZIRI NI UTHIBITISHO WA UHUSIANO HUO MZURI KATI YA NCHI HIZO.

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN AMEUPONGEZA USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA ZANZIBAR NA INDIA NA AMEISHUKURU SERIKALI NA WANANCHI WA INDIA KWA MISAADA MBALIMBALI AMBAYO IMEKUWA IKIITOA KWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA WANANCHI WAKE.

DK. SHEIN ALIMUELEZA MAKAMU WA RAIS WA INDIA KUWA ZIARA YAKE NCHINI HUMU IMELENGA KUIMARISHA UHUSIANO HUO WA KIDIPLOMASIA ULIASISIWA MIAKA YA SITINI CHINI YA MISINGI IMARA YA URAFIKI ILIYOWEKWA NA WAASISI WAKE VIONGOZI WA KWANZA WA NCHI MBILI HIZO.

HALIKADHALIKA ALIMUELEZA KUWA ZIARA HIYO AMEDHAMIRIA KUKUKUZA USHIRIKIANO KATI YA ZANZIBAR NA INDIA KATIKA MAENEO YA ELIMU, MAFUNZO, BIASHARA, KILIMO PAMOJA NA KUHIMIZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA MBALIMBALI ZA UCHUMI.

ALIFAANUA KUWA UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATI YA WATU WA ZANZIBAR NA WATU WA INDIA NI WA KIHISTORIA ULIODUMU KWA KARNE NYINGI HIVYO KUUFANYA KUWA WA KIDUGU.

AMEMUELEZA BWANA ANSARI KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMEFURAHISHWA NA MSAADA WA UJENZI WA CHUO CHA MAFUNZO YA AMALI KITAKACHOJENGWA HUKO PEMBA PAMOJA NA MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA JANA YA KUANZISHA CHUO KAMA HICHO HUKO UNGUJA KUPITIA CHUO CHA BAREFOOT CHA TILONIA, JAIPUR.

AMEBAINISHA KUWA KATIKA MIAKA YA HIVI KARIBUNI KUMEKUWEPO NA WANANCHI WENGI WA ZANZIBAR WANAKWENDA INDIA KWA SABABU ZA KIMATIBABU HIVYO AMETAKA KUWEPO NA USHIRIKIANO ZAIDI WA NAMNA BORA YA KULETA WAGONJWA HAO NCHINI HUMU.

KWA UPANDE MWINGINE DK. SHEIN AMEIOMBA SERIKALI YA INDIA KUANGALIA NAMNA INAVYOWEZA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA ZANZIBAR KUISAIDIA UPATIKANAJI WA MADAWA KWA ZANZIBAR.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI AMETUMIA FURSA KUMUELEZA MAKAMU WA RAIS WA INDIA HAJA YA KUONGEZA FURSA ZAIDI ZA MASOMO YA MUDA MFUPI NA MUDA WA KATI KWA WANANCHI WA ZANZIBAR ILI KUJENGA UWEZO KATIKA TAALUMA MBALIMBALI ILI KUHARAKISHA MAENDELEO.

KWA UPANDE WAKE MAKAMU WA RAIS WA INDIA BWANA MOHAMED HAMID ANSARI AMEMHAKIKISHIA DK. SHEIN KUWA SERIKALI YA NCHI YAKE ITAENDELEA KUSAIDIA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR ZA KUJILETEA MAENDELEO.

BWANA ANSAR AMESEMA UHUSIANO WA KIHISTORIA WA WANANCHI WA INDIA NA ZANZIBAR ULIOANZA KARNE NYINGI TANGU ENZI ZA KUTEGEMEA PEPO ZA KUSI NA KASKAZI UMEKUWA IMARA NA KILA SIKU WANANCHI WAKE WAMEONYESHA ARI YA KUZIDI KUUIMARISHA.

MAPEMA ASUBUHI ALITEMBELEA MAKUMBUSHO YA MAHATMA GHANDI ILIYOPO MJINI NEW DELHI AMBAPO ALIWEKA SHADA LA MAUA PAMOJA NA KUSAINI KITABU CHA KUMBUKUMBU.

BAADAE MCHANA ANATARAJIWA KUKUTANA NA WATANZANIA ANAOISHI MJINI HAPA KATIKA UKUMBI WA URAFIKI KWENYE HOTELI YA ASHOK NA ATAKUTANA PIA NA WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA FAMILIA WA INDIA. JIONI ATAHUDHURIA CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA KWA HESHMA YAKE NA MWENYEJI WAKE MAKAMU WA RAIS WA INDIA.

HAPO JANA KABLA YA KUONDOKA JAIPUR, JIMBO LA RAJASTAN, KUJA NEW DELHI DK. SHEIN ALITEMBELEA MAKUMBUSHO YA HAWA MAHAL NA ALBERT YALIYOPO MJINI HUMO.

MIONGONI MWA WALIOFUATANA NA RAIS KATIKA ZIARA HIYO NI PAMOJA NA MKE WAKE MAMA MWANAMWEMA, WAZIRI WA FEDHA OMAR YUSUF MZEE, WAZIRI WA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO BIBI ZAINAB OMAR MOHAMED, WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA NA MASOKO NASSOR AHMED MARZUI, NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DK. MAHADHI JUMA MAALIM NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA INJINIA JOHN KIJAZI.

WENGINE NI KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MOHAMED SALEH JIDAWI, KATIBU MKUU KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM, MSHAURI WA RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UWEKEZAJI NA UCHUMI BALOZI MOHAMED RAMIA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA UWEKEZAJI ZANZIBAR –ZIPA SALUM KHAMIS NASSOR.

Monday, February 3, 2014

KESI ZA UBAKAJI KASKAZINI UNGUJA


MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

JUMLA YA KESI THELATHINI NA SITA ZA UBAKAJI ZIMERIPOTIWA KUTOKEA KATIKA MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA JANA.

AKIZUNGUMZA NA ADHANA FM REDIO KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI HASSAN MSANGI AMESEMA BADO TATIZO HILO LIMEKUWA LIKIENDELEA KUTOKANA NA MWAMKO MDOGO WA WANANCHI WA KURIPOTI TATIZO HILO.

AIDHA AMEFAHAMISHA KUWA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALI MBALI WAMEKUWA WAKIENDELEA KUIELIMISHA JAMII JUU YA UMUHIMU WA KURIPOTI MATENDO YA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA.

SAMBAMBA NA HAYO AMEWATAKA WANANCHI WAWE TAYARI KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUTOA USHAHIDI PINDI WANAPOTAKIWA KUFANYA HIVYO ILI WAWEZE KUTOKOMEZA TATIZO HILO KATIKA MKOA HUO.

WIZARA ZA ELIMU TZ ZAKUTANA


WILAYA YA MAGHARIBI

 

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TANZANIA BARA ZIMEKUTANA LEO KUJADILI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

 

AKIFUNGUA MKUTANO HUO WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR MHESHIMIWA ALI JUMA SHAMUHUNA OFISINI KWAKE MAZIZINI ,AMESEMA KIKAO HICHO KINA LENGO LA KUJADILI UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI HIYO KWA MWAKA HUU KAMA IMEPUNGUA AU LA A.

 

AIDHA AMESEMA KUWEPO KWA UTARATIBU WA KUKUTANA KILA MWAKA KUMESAIDIA KUPIGA HATUA KUBWA YA MASHIRIKIANO KATIKA SWALA LA ELIMU.

 

NA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI WA TANZANIA BARA DK SHUKURU KAWAMBWA AMESEMA KIKAO HICHO KITAJADILI ELIMU YA SEKONDARI NA YA MSINGI PAMOJA NA KUCHUNGUZA KASORO NA KUZIJADILI.

 

KIKAO HICHO NI CHA SIKU MOJA NA NI MARA YA PILI KUFANYIKA HAPA ZANZIBAR.

Sunday, February 2, 2014

ZANZIBAR NA JAPAN


SERIKALI YA JAPAN IMESEMA ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR KATIKA JITIHADA ZAKE ZA KUJIKWAMUA KIUCHUMI, KWA KUENDELEA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO IKIWEMO YA MAJI SAFI NA SALAMA, MIJINI NA VIJIJINI.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN BW. NORIO MITSUYA AMEELEZA HAYO WAKATI AKIZUNGUNGUMZA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, OFISINI KWAKE MIGOMBANI.

AMESEMA JAPAN NA ZANZIBAR ZINA UHUSIANO WA KIUCHUMI WA MUDA MREFU, NA KWAMBA UMEKUWA UKIIMARIKA SIKU HADI SIKU KUTOKANA NA NIA NJEMA YA NCHI HIZO.

BW. MITSUYA AKIONGOZA UJUMBE WA WATU SABA WA JAPAN, AMETAJA MAENEO MENGINE WANAYOWEZA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR KUWA NI PAMOJA NA SEKTA YA KILIMO, UVUVI, UTALII PAMOJA NA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA WASIOKUWA NA AJIRA.

AKIZUNGUMZIA KUHUSU SEKTA YA UTALII, AMESEMA WATALII KUTOKA JAPAN WAMESHAJIIKA KUITEMBELEA TANZANIA AMBAPO IDADI YA WATALII WA NCHI HIYO IMEONGEZEKA KUTOKA WATALII 4000 HADI 5000 KWA MSIMU ULIOPITA.

NAE MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMESEMA ZANZIBAR INATHAMINI MISAADA INAYOTOLEWA NA SERIKALI YA JAPAN, NA KUWASHAJIISHA WAWEKEZAJI WA NCHI HIYO KUJA KUWEKEZA ZANZIBAR HASA KATIKA MIRADI YA UJENZI WA HOTELI ZA KISASA.

AIDHA AMEIOMBA NCHI HIYO KUANGALIA UWEZEKANO WA KUCHANGIA UPATIKANAJI WA UMEME WA UHAKIKA ZANZIBAR, ILI KUEPUKA KUTEGEMEA MOJA KWA MOJA NISHATI HIYO KUTOKA TANZANIA BARA.

MAULIDI


ZANZIBAR

 

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEWANASIHI WAZAZI NA WALEZI KUTUMIA HEKIMA NA BUSARA KATIKA MALEZI YA WATOTO, ILI KUWAJENGA KATIKA MAADILI MEMA YA DINI YA KIISLAM.

 

AMESEMA WAZAZI NA WALEZI WANA NAFASI KUBWA YA KUREJESHA MAADILI BORA  KATIKA JAMII IWAPO WATAREJESHA UTAMADUNI WA MALEZI YA PAMOJA, KUPENDANA NA KUACHA KUFARAKANA KWA MAMBO YASIYOKUWA YA MSINGI.

 

ALHAJ MAALIM SEIF AMETOA NASAHA HIZO WAKATI AKIZUNGUMZA KATIKA MAULID YA KUSHAREHEKEA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (SAW), YALIYOANDALIWA NA MADRAST IMAN ISLAMIYA YA JANG'OMBE MJINI ZANZIBAR.

 

AMEIPONGEZA MADRASA HIYO KWA MAFANIKIO MAKUBWA ILIYOPATA, IKIWA NI PAMOJA NA KUONGEZA IDADI YA WANAFUNZI KUTOKA 12 MWAKA 1995 HADI 192 MWAKA HUU.

 

AMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA MADRASA HIYO KATIKA KUTAFUTA NAMNA YA KUZITATUA KERO ZINAZOWAKABILI ZIKIWEMO UPUNGUFU WA VYUMBA VYA KUSOMEA.

 

KATIKA RISALA YA MADRASA HIYO ILIYOSOMWA NA MWALIMU HASSAN HASSAN (HASANAYNI) WAMESEMA WANAKUSUDIA KUIJENGA UPYA MADRASA YAO YA ZAMANI, ILI KUTOA NAFASI KWA WANAFUNZI ZAIDI KUPATA VYUMBA VYA KUSOMEA, NA KUWAOMBA WAFADHILI KUJITOKEZA KUCHANGIA UJENZI HUO.

ZIARANI INDIA


SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA CHUO CHA BAREFOOT CHA INDIA ZIMEKUBALIANA KUANZISHA CHUO CHA MAFUNZO YA AMALI KWA WANAWAKE WA ZANZIBAR WAISHIO VIJIJINI.

MAKUBALIANO HAYO YAMEFIKIWA LEO WAKATI RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN ALIPOTEMBELEA CHUO HICHO HUKO TILONIA, WILAYA YA AJMER KATIKA JIMBO LA RAJASTAN AKIWA KATIKA SIKU YAKE YA PILI YA ZIARA YAKE YA SIKU TISA NCHINI INDIA.

CHINI YA MAKUBALIANO HAYO AMBAYO KWA UPANDE WA SERIKALI YA ZANZIBAR YALISAINIWA NA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM NA MWANZILISHI WA CHUO CHA BAREFOOT BWANA BUNCKER ROY CHUO HICHO KITATOA MAFUNZO HAYO KWA WANAWAKE WATU WAZIMA ILI KUWAJENGEA UWEZO WAO KITAALUMA NA STADI ZA MAISHA ILI WAWEZE KUPAMBANA NA UMASIKINI NA HATIMAE KUINUA KIWANGO CHAO CHA MAISHA.

CHUO HICHO KITATOA MAFUNZO YA UFUNDI WA UMEME JUA PAMOJA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI IKIWEMO UTENGENEZAJI WA BIDHAA KAMA CHAKI, MISHUMAA, VYANDARUA NA PEDI ZA WANAWAKE.

AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA KUSHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MAKUBALIANO HAYO, RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN ALISEMA KUTIWA SAINI MAKUBALIANO HAYO NI HATUA NYINGINE MBELE KATIKA JITIHADA ZA SERIKALI ZA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE NA KUPAMBANA NA UMASKINI NCHINI.

AMESEMA KUJENGWA KWA CHUO HICHO KUTATOA FURSA ZAIDI KWA JAMII ZA WATU WA VIJIJNII AMBAO BADO HAWAJAPATA HUDUMA YA UMEME NCHINI KUPATA NISHATI HIYO KWA GHARAMA NAFUU NA KWA WEPESI ZAIDI.

KWA UPANDE WAKE BIBI MEAGAN FALLONE WA CHUO HICHO AMEELEZA KUWA CHUO HICHO KITAKACHOJENGWA ZANZIBAR MBALI YA KUTOA MAFUNZO KWA WANAWAKE WA UNGUJA NA PEMBA KITATOA FURSA PIA KWA WANAWAKE KUTOKA NCHI JIRANI KUJA KUJIFUNZA TAALUMA HIZO CHUO HAPO.

CHUO CHA BAREFOOT AMBACHO KINATOA MAFUNZO MBALIMBALI YA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WATU WAZIMA WAKIWEMO WAJANE KUTOKA MAENEO YA VIJIJINI KUTOKA NCHI ZINAZOENDELEA KILIANZISHWA MWAKA 2004.

CHUO HICHO HUCHUKUA WANAFUNZI KUTOKA NDANI NA NJE YA INDIA AMBAPO HIVI SASA KUNA WANAFUNZI KUTOKA NJE 37 AMBAO WANATOKA ZANZIBAR, VISIWA VYA COMORO, TOGO, IVORY COAST, PANAMA, INDONESIA, NEPAL, HONDURUS, BRAZIL, MEXICO NA BELIZE.

KWA UPANDE WA TANZANIA TANGU KUANZISHWA KWAKE MWAKA 2004 HADI SASA JUMLA YA WANAWAKE 29 WAMEPATA MAFUNZO YAO KATIKA CHUO HICHO AMBAPO KUTOKA TANZANIA BARA NI WANAWAKE 18 NA 11 KUTOKA ZANZIBAR AMBAO MIONGONI MWAO NI WANANWAKE WAWILI WALIOPO CHUO HAPO HIVI SASA AMBAO WANATARAJIWA KUMALIZA MAFUNZO YAO MWEZI MACHI MWAKA HUU.

WANAWAKE WANAOPATA MAFUNZO KATIKA CHUO HICHO HURUDI VIJIJINI KWAO AMBAKO HUSIMAMIA SHUGHULI ZA KUSAMBAZA HUDUMA ZA UMEME JUA KUANZIA KUSAMBAZA, KUFANYA MATENGENZO PAMOJA NA KUTENGENEZA BAADHI YA VIFAA VINAVYOTUMIKA KATIKA USAMBAZAJI HUO.

DK. SHEIN ATAMALIZA ZIARA YAKE KATIKA JIMBO LA RAJASTAN LEO MCHANA KWA KUTEMBELEA MAENEO YA HISTORIA YA HAWA MAHAL NA JUMBA LA MAKUMBUSHO LA ALBERT NA BAADAE JIONI ATAONDOKA KWENDA NEW DELHI KUENDELEA NA ZIARA YAKE HAPO KESHO.

KATIKA ZIARA HIYO DK. SHEIN AMEFUATANA NA MKE WAKE MAMA MWANAMWEMA, WAZIRI WA FEDHA OMAR YUSUF MZEE, WAZIRI WA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO BIBI ZAINAB OMAR MOHAMED, WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA NA MASOKO NASSOR AHMED MARZUI, NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DK. MAHADHI JUMA MAALIM NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA INJINIA JOHN KIJAZI.
WENGINE KATIKA MSAFARA HUO NI KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MOHAMED SALEH JIDAWI NA KATIBU MKUU KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM, MSHAURI WA RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UWEKEZAJI NA UCHUMI BALOZI MOHAMED RAMIA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA UWEKEZAJI ZANZIBAR –ZIPA SALUM KHAMIS

RAIS SHEIN INDIA


4

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN ANAONDOKA NCHINI  KUANZA ZIARA YA SIKU TISA NCHINI INDIA KUFUATIA MWALIKO WA MAKAMU WA RAIS WA NCHI HIYO BWANA MOHAMMAD HAMID ANSARI.

AKIWA NCHINI HUMO DK. SHEIN ANATARAJIWA KUKUTANA NA VIONGOZI WA NCHI HIYO NA JUMUIYA ZA WAFANYABIASHARA KWA LENGO LA KUKUZA UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA INDIA PAMOJA NA KUHIMIZA USHIRIKIANO KATI YA ZANZIBAR NA INDIA KATIKA NYANJA ZA UCHUMI, BIASHARA, UWEKEZAJI, AFYA, KILIMO NA ELIMU.

KATIKA ZIARA HIYO MBALI NA MKE WAKE MAMA MWANAMWEMA, DK. SHEIN AMEFUATANA NA WAZIRI WA FEDHA OMAR YUSUF MZEE, WAZIRI WA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO BIBI ZAINAB OMAR MOHAMED, WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA NA MASOKO NASSOR AHMED MARZUI NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DK. MAHADHI JUMA MAALIM.

WENGINE KATIKA MSAFARA HUO NI KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MOHAMED SALEH JIDAWI NA KATIBU MKUU KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM, MSHAURI WA RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UWEKEZAJI NA UCHUMI BALOZI MOHAMED RAMIA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA UWEKEZAJI ZANZIBAR –ZIPA SALUM KHAMIS NASSOR.

AKIWA NCHINI INDIA JUMAPILI TAREHE 2 FEBRUARI, 2014 ATATEMBELEA CHUO CHA BAREFOOT KILICHOKO TILONIA AMBAKO SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INATARAJIWA KUSAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA CHUO HICHO AMBACHO KIMEJIEGEMEZA KATIKA KUWAJENGEA UWEZO KIUCHUMI, KIJAMII NA KIELIMU WANAWAKE WAZEE NA WAJANE WAISHIO VIJIJINI ILI KUINUA KIWANGO CHAO CHA MAISHA.

SIKU INAYOFUATA TAREHE 3 FEBRUARI, 2014 MAPEMA ASUBUHI ATAZURU KUMBUKUMBU YA MAHATMA GHANDHI AMBAKO ATAWEKA SHADA LA MAUA NA BAADAE ATAFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE MAKAMU WA RAIS.

BAADAE MCHANA SIKU HIYO ATAFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU WA INDIA BWANA MANMOHAN SINGH, ATAONANA NA WAZIRI ANAYESHUGHULIKIA DIASPORA NA WAZIRI WA AFYA NA FAMILIA WA NCHI HIYO. JIONI ATAKUTANA NA WATANZANIA WANAIOSHI DELHI NA BAADAE USIKU ATAHUDHURIA CHAKULA CHA USIKU KILICHOANDALIWA KWA HESHMA YAKE NA MWENYEJI WAKE MAKAMU WA RAIS WA INDIA.

TAREHE 4 FEBRUARI, 2014 ATATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI WA MAZAO YA KILIMO, ATAKUTANA NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA NA KUONDOA KWENDA MJI WA HYDERABAD AMBAKO SIKU INAYOFUATA ATAKUTANA NA MWENYEKITI WA HOSPILTALI ZA APPOLO NA KUSAIDIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO.

DK. SHEIN SIKU HIYO ATAKUTANA PIA NA BARAZA LA BIASHARA YA MADAWA NCHI ZA NJE LA INDIA NA BAADAE ATAPATA FURSA YA KUTEMBELEA KIWANDA CHA MADAWA AMBAPO BAADAE ATASAFIRI HADI MJI WA BANGALORE AMBAKO SIKU YA ALHAMISI TAREHE 6 FEBRUARI, 2014 ATATEMBELEA HOSPITALI YA MANIPAL NA KUTIA SAINI MAKUBALINO YA USHIRIKIANO NA HOSPITALI HIYO NA BAADAE KUONDOKA KWENDA MUMBAI.

AKIWA MUMBAI TAREHE 7 FEBRUARI, 2014 DK. SHEIN ATATEMBELEA KAMPUNI YA KUTENGENEZA MATREKTA YA MAHINDRA NA BAADAE JIONI ATAKUTANA NA MAKAMPUNI YA BIASHARA YA UTALII NA WAKALA WA SAFARI ZA KITALII.

JUMAMOSI TAREHE 8 FEBRUARI, 2014 RAIS NA UJUMBE WAKE UTATEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA VIUNGO (SPICES).

RAIS WA ZANZIBAR NAMWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI NA UJUMBE WAKE UTAONDOKA INDIA JUMAPILI TAREHE 9 FEBRUARI, 2014 KUREJEA NYUMBANI.