TEHERAN
KAMATI MAALUMU ZA UMOJA WA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA
USHIRIKIANO WA KIISLAMU OIC ZIMEPITISHA MAAZIMIO 12 YA AJENDA ZA MKUTANO WA
TISA WA MASPIKA WA MABUNGE WA NCHI WANACHAMA UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMANNE NA
JUMATANO MJINI TEHRAN.
KAZEM JALALI, MSEMAJI WA MKUTANO WA TISA WA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA
OIC AMESEMA, KAMATI MAALUMU ZA UMOJA WA MABUNGE YA KIISLAMU ZIMEJADILI NA
KUPASISHA MAAZIMIO 12 KUPITIA KAMATI NNE ZA SERA ZA NJE, WANAWAKE, PALESTINA NA
MASPIKA WA MABUNGE.
JALALI AMEONGEZA KUWA KAMATI HIZO ZIMEJADILI PIA JINSI YA KUZIDISHA
MSHIKAMANO NA KUIMARISHA ZAIDI UMOJA KATI YA NCHI ZA KIISLAMU, KUPAMBANA NA
TAASUBI NA UENEZAJI HOFU JUU YA UISLAMU NA KUPAMBANA NA VITENDO VYA KUFURUTU
MPAKA KAMA ILIVYOPENDEKEZWA NA RAIS WA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN KATIKA UMOJA
WA MATAIFA NA KUPASISHWA NA BARAZA KUU LA UMOJA HUO, NA ZIKAPONGEZA PIA JUHUDI
ZILIZOFANYWA NA JAMHURI YA KIISLAMU YA IRAN.
JALALI AMEONGEZA KUWA AZIMIO MUHIMU ZAIDI LILILOPASISHWA NA KAMATI YA
SERA ZA NJE ZA UMOJA WA MABUNGE YA OIC NI KUPAMBANA NA UGAIDI, KUTILIA MKAZO
HAKI YA KISHERIA YA MAPAMBANO NA MUQAWAMA DHIDI YA UVAMIZI NA UKALIAJI WA
MABAVU, KULAANI VIKWAZO VYA KILA AINA DHIDI YA NCHI ZA KIISLAMU NA SISITIZO JUU
YA HAKI YA NCHI NA MATAIFA YOTE YA KUJIPATIA TEKNOLOJIA MPYA NA KUZITUMIA
TEKNOLOJIA HIZO KWA MALENGO YA AMANI.
No comments:
Post a Comment