ZANZIBAR
MWEYEKITI WA CHAMA CHA WAKULIMA ZANZIBAR (AFP)
NDUGU SOUD SAID SOUD AMEIOMBA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUWAONGEZEA MSHAHARA
WAFANYAKAZI WANAOPOKEA MSHAHARA WA KIMA CHA CHINI ILI WAWEZE KUJIKIMU KATIKA
MAISHA YAO YA KILA SIKU.
MWENYEKITI SOUD AMEYASEMA HAYO WAKATI ALIPOKUWA
AKIZUNGUMZA NA RADIO ADHANA FM KUHUSIANA NA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA ZANZIBAR.
AMESEMA HALI YA MAISHA YA ZANZIBAR INAKUWA GUMU
SIKU HADI SIKU HIVYO IWAPO SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ITAWEZA
KUWAONGEZEA WAFANYAKZI WA KIWANGO CHA CHINI MSHAHARA WATAWEZA KUKABILIANA NA
UGUMU WA MAISHA.
AMEFAFANUA KUWA HALI HIYO YA UGUMU WA MAISHA
IMESABABISWA NA SERIKALI KUPANDISHA BEI MAMBO MUHIMU KAMA VILE UMEME,MAJI NA CHAKULA BILA KUZINGATIA HALI ZA WATU.
SAMBAMBA NA HAYO AMESEMA KUWA MAISHA YA ZANZIBAR
KWA WAKATI HUU NI MAGUMU HAKUNA BUDI KWA SERIKALI KUBUNI MBINU BORA ZA
KUBORESHA MAISHA YA WAZANZIBARI HUSUSAN WA VIJIJINI.
No comments:
Post a Comment