4
RAIS
WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN
ANAONDOKA NCHINI KUANZA ZIARA YA SIKU TISA NCHINI INDIA KUFUATIA MWALIKO WA
MAKAMU WA RAIS WA NCHI HIYO BWANA MOHAMMAD HAMID ANSARI.
AKIWA NCHINI HUMO DK.
SHEIN ANATARAJIWA KUKUTANA NA VIONGOZI WA NCHI HIYO NA JUMUIYA ZA
WAFANYABIASHARA KWA LENGO LA KUKUZA UHUSIANO KATI YA TANZANIA NA INDIA PAMOJA
NA KUHIMIZA USHIRIKIANO KATI YA ZANZIBAR NA INDIA KATIKA NYANJA ZA UCHUMI,
BIASHARA, UWEKEZAJI, AFYA, KILIMO NA ELIMU.
KATIKA ZIARA HIYO MBALI
NA MKE WAKE MAMA MWANAMWEMA, DK. SHEIN AMEFUATANA NA WAZIRI WA FEDHA OMAR YUSUF
MZEE, WAZIRI WA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO BIBI
ZAINAB OMAR MOHAMED, WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA NA MASOKO NASSOR AHMED
MARZUI NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DK. MAHADHI
JUMA MAALIM.
WENGINE KATIKA MSAFARA
HUO NI KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MOHAMED SALEH JIDAWI NA KATIBU MKUU KILIMO NA
MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM, MSHAURI WA RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
UWEKEZAJI NA UCHUMI BALOZI MOHAMED RAMIA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA
UWEKEZAJI ZANZIBAR –ZIPA SALUM KHAMIS NASSOR.
AKIWA NCHINI INDIA
JUMAPILI TAREHE 2 FEBRUARI, 2014 ATATEMBELEA CHUO CHA BAREFOOT KILICHOKO
TILONIA AMBAKO SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INATARAJIWA KUSAINI
MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA CHUO HICHO AMBACHO KIMEJIEGEMEZA KATIKA
KUWAJENGEA UWEZO KIUCHUMI, KIJAMII NA KIELIMU WANAWAKE WAZEE NA WAJANE WAISHIO
VIJIJINI ILI KUINUA KIWANGO CHAO CHA MAISHA.
SIKU INAYOFUATA TAREHE 3
FEBRUARI, 2014 MAPEMA ASUBUHI ATAZURU KUMBUKUMBU YA MAHATMA GHANDHI AMBAKO
ATAWEKA SHADA LA MAUA NA BAADAE ATAFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE MAKAMU WA
RAIS.
BAADAE MCHANA SIKU HIYO
ATAFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI MKUU WA INDIA BWANA MANMOHAN SINGH, ATAONANA NA
WAZIRI ANAYESHUGHULIKIA DIASPORA NA WAZIRI WA AFYA NA FAMILIA WA NCHI HIYO.
JIONI ATAKUTANA NA WATANZANIA WANAIOSHI DELHI NA BAADAE USIKU ATAHUDHURIA
CHAKULA CHA USIKU KILICHOANDALIWA KWA HESHMA YAKE NA MWENYEJI WAKE MAKAMU WA
RAIS WA INDIA.
TAREHE 4 FEBRUARI, 2014
ATATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI WA MAZAO YA KILIMO, ATAKUTANA NA JUMUIYA YA
WAFANYABIASHARA NA KUONDOA KWENDA MJI WA HYDERABAD AMBAKO SIKU INAYOFUATA
ATAKUTANA NA MWENYEKITI WA HOSPILTALI ZA APPOLO NA KUSAIDIA MAKUBALIANO YA
USHIRIKIANO.
DK. SHEIN SIKU HIYO
ATAKUTANA PIA NA BARAZA LA BIASHARA YA MADAWA NCHI ZA NJE LA INDIA NA BAADAE
ATAPATA FURSA YA KUTEMBELEA KIWANDA CHA MADAWA AMBAPO BAADAE ATASAFIRI HADI MJI
WA BANGALORE AMBAKO SIKU YA ALHAMISI TAREHE 6 FEBRUARI, 2014 ATATEMBELEA
HOSPITALI YA MANIPAL NA KUTIA SAINI MAKUBALINO YA USHIRIKIANO NA HOSPITALI HIYO
NA BAADAE KUONDOKA KWENDA MUMBAI.
AKIWA MUMBAI TAREHE 7
FEBRUARI, 2014 DK. SHEIN ATATEMBELEA KAMPUNI YA KUTENGENEZA MATREKTA YA
MAHINDRA NA BAADAE JIONI ATAKUTANA NA MAKAMPUNI YA BIASHARA YA UTALII NA WAKALA
WA SAFARI ZA KITALII.
JUMAMOSI TAREHE 8
FEBRUARI, 2014 RAIS NA UJUMBE WAKE UTATEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA VIUNGO
(SPICES).
RAIS WA ZANZIBAR
NAMWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI NA UJUMBE WAKE UTAONDOKA INDIA JUMAPILI
TAREHE 9 FEBRUARI, 2014 KUREJEA NYUMBANI.
No comments:
Post a Comment