KAMPALA
RAIS YOWERI
MUSEVENI WA UGANDA AMESEMA KUWA, ATASAINI MUSWADA WA KUPIGA MARUFUKU VITENDO
VICHAFU VYA NDOA ZA WATU WA JINSIA MOJA NCHINI HUMO.
MUSWADA AMBAO KAMA
UTASAINIWA NA KUWA SHERIA UTAWAPA ADHABU YA KIFUNGO CHA MAISHA JELA WATU
WATAKAOPATIKANA WAKIJIHUSISHA NA VITENDO HIVYO.
OFWONO OPONDO,
MSEMAJI WA SERIKALI YA UGANDA AMESEMA KUWA, RAIS MUSEVENI AMETANGAZA UAMUZI HUO
KATIKA MKUTANO WA CHAMA TAWALA CHA NRM.
OPONDO AMESEMA
KWAMBA, UAMUZI WA RAIS MUSEVENI UMETEGEMEA RIPOTI YA WATAALAMU WA MASUALA YA
TIBA AMBAYO INAONESHA KUWA, LIWATI NA USAGAJI SIO SUALA LA KIMAUMBILE, BALI
CHIMBUKO LAKE NI TABIA YA MTU.
WIKI MBILI
ZILIZOPITA RAIS MUSEVENI ALISEMA KUWA, ANGESAINI MUSWADA HUO NA KUWA SHERIA
BAADA YA KUPATA MTAZAMO WA WATAALAMU.
MUSWADA HUO
UNAOPIGA MARUFUKU NDOA ZA WATU WA JINSIA MOJA NA AMBAO ULIPIGIWA MAKELELE NA
MADOLA YA MAGHARIBI PAMOJA NA MASHIRIKA YA KUTETEA HAKI ZA BINADAMU ULIPASISHWA
NA BUNGE LA UGANDA DISEMBA MWAKA JANA.
HATA HIVYO MWEZI
ULIOPITA WA JANUARI RAIS MUSEVENI ALISEMA KWAMBA, MUSWADA HUO ULIPASISHWA BILA
YA IDADI INAYOTAKIWA BUNGENI KWA AJILI YA KUPASISHA MUSWADA.
BADO HAIJAJULIKANA
RAIS MUSEVENI ATAUSAINI LINI MUSWADA HUO ILI UWE SHERIA.
No comments:
Post a Comment