tangazo

tangazo

Saturday, February 8, 2014

dokta sheni akutana na kampuni ya utengenezaji magari na zana za kilimo


KAMPUNI YA KUTENGENEZA MAGARI NA ZANA ZA KILIMO YA MAHIDRA YA MJINI MUMBAI, INDIA IMEKUBALI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR KUINUA KIWANGO CHA UZALISHAJI WA MAZAO YA KILIMO NCHINI ILI HATIMAE KUFIKIA LENGO LA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA IFIKAPO MWAKA 2020.

 

MTENDAJI MKUU WA HUDUMA ZA KIMATAIFA WA KAMPUNI HIYO BWANA RUZBEN IRANI AMESEMA HAYO WAKATI WA MAZUNGUMZO NA UJUMBE WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR ULIOONGOZWA NA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN AMBAYE ALITEMBELEA KIWANDA HICHO.

 

BWANA IRANI ALISEMA KAMPUNI YAKE INAAFIKI MAOMBI YA RAIS WA ZANZIBAR LA KUTAKA KAMPUNI YAKE ISAIDIE SEKTA YA KILIMO ILI IWEZE KUFIKIA MALENGO YA DIRA YA ZANZIBAR 2020 NA MKUZA II.

 

KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN ALIITAKA KAMPUNI HIYO KUUNGA MKONO MAPANGO WA SERIKALI WA KULETA MAPINDUZI YA KIJANI ILI KUZALISHA MAHITAJI YA CHAKULA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO MWAKA 2015/2016 IKIWA NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI WA DIRA YA MAENDELEO ZANZIBAR 2020 AMBAYO INAELEKEZA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA IFIKAPO MWAKA 2020.

 

KATIKA KUTEKELELEZA MPANGO HUO ALIELEZA KUWA SERIKALI IMEKUWA IKITOA RUZUKU KWA WAKULIMA KWA KUWAPATIA PEMBEJEO NA ZANA ZA KILIMO LAKINI CHANGAMOTO KUBWA IMEKUWA MAHITAJI MAKUBWA YA ZANA ZA KILIMO HUSUSAN MATREKTA.

 

ALIBAINISHA KUWA DHAMIRA YA SERIKALI NI KUHAKIKISHA INABORESHA MAISHA YA WANANCHI WAKE WAKIWEMO WAKULIMA AMBAO NJIA BORA KWAO NI KUWAONDOA KUTOKA KILIMO ZA ZAMANI HADI MATUMIZI YA TEKINOLOJIA YA KISASA ILI KUONGEZA TIJA KATIKA UZALISHAJI NA HATIMAE KUONDOKANA NA UMASIKINI.

 

ALIFAFANUA KUWA KUWAWEZESHA WAKULIMA NCHINI NA KUFIKIA HATUA HIYO KUNAKWENDA SAMBAMBA NA LENGO KUU YA DIRA YA ZANZIBAR YA KUIFANYA ZANZIBAR KUWA NCHI YA KIPATO CHA KATI IFIKAPO MWAKA 2020.

 

DK. SHEIN ALIUELEZA UONGOZI WA KAMPUNI HIYO KUWA ZIARA YAKE KATIKA KIWANDA HICHO AMBAYO NI YA PILI, MARA YA KWANZA IKIWA NI MWAKA 2008 AKIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, INAONESHA KUTHAMINI UTAALAMU NA UWEZO WA KAMPUNI HIYO KATIKA KUENDELEZA KILIMO NA KUMUENDELEZA MKULIMA MBAYE NDIE MLENGWA MKUU.

 

ALIELEZA KUWA AMEFURAHISHWA NA MIKAKATI YA KAMPUNI HIYO YA KUSAIDIA WAKULIMA IKIWEMO SUALA LA UTAFITI AMBALO ALIELEZA KUWA NI LA MSINGI HIVYO KUELEZA KUWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INGEPENDA PIA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI HIYO KATIKA ENEO HILO KUPITIA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO ZANZIBAR.

 

KATIKA KUTEKELEZA WITO WA RAIS, BWANA IRANI ALIELEZA KUWA KWA KUANZIA KAMPUNI YAKE ITATUMA TIMU YA WATAALAMU HIVI KARIBUNI ILI KUFANYA UTAFITI KUJUA MAHITAJI, AINA YA ZANA PAMOJA NA NYENZO NYINGINE MUHIMU ZA KILIMO ZINAZOHITAJIKA KWA MUJIBU WA MAZINGIRA YA ZANZIBAR.

 

ALIFAFANUA KUWA ILI KUPATA MATOKEO MAZURI MIONGONI WA WATAALAMU WATAOKWENDA ZANZIBAR NI WA KUFANYA UTAFITI WA UDONGO KUFAHAMU AINA YA UDONGO NA KUJUA HATUA ZA KITAALAMU ZINAZOTAKIWA KUCHUKULIWA KUONGEZA TIJA KATIKA UZALISHAJI NA PIA KUJUA AINA YA MATREKTA YANAYOLINGANA NA MAZINGIRA YA ZANZIBAR.

 

BWANA IRANI ALIONGEZA KUWA KAMPUNI YAKE INA KILA SABABU YA KUZIUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KULETA MAPINDUZI YA KILIMO KWA KUWA INAAMINI KUWA MAFANIKIO YAKE YATAKUWA MFANO KWA NCHI NYINGINE BARANI AFRIKA.

 

ALISISITIZA KUWA KAMPUNI YAKE ITAJIDHATITI KUTEKELEZA WAJIBU WAKE HARAKA IWEZEKANAVYO KWA KUWA MIAKA 6 KABLA YA KUFIKIA 2020 KULIFIKIA LENGO LA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA KUTOKA ASILIMIA 20 YA SASA HADI 100 NI CHANGAMOTO LAKINI AKAMUHAKIKISHIA HILO LINAWEZAKANA KWA KUWA NIA NA DHAMIRA NDIO MUHIMU.

 

AKIWA KIWANDANI HAPO DK. SHEIN NA UJUMBE WAKE ULITEMBELEA SEHEMU YA KUUNGANISHA INJINI ZA MATREKTA PAMOJA NA SEHEMU YA KUUNGANISHA MATREKTA TAYARI KWA KUPELEKWA KWENYE MASOKO.

ALIPATA FURSA PIA YA KUONA AINA MBALIMBALI ZA MATREKTA YANAYOTENGENEZWA NA KAMPUNI HIYO PAMOJA NA MAGARI NA PIKIPIKI. KAMPUNI HIYO HIVI KARIBUNI IMETOA TREKTA MPYA DOGO AINA YA YUVRAJ 215 LENYE NGUVU ZA 15-20 HP AMBALO LINAWEZA KUFANYA KAZI ZOTE KILIMO PAMOJA NA SHUGHULI NYINGINE ZISIZOKUWA ZA KILIMO.

KAMPUNI YA MAHINDRA AMBAYO ILIANZISHWA MWAKA 1945 NI KAMPUNI INAONGOZA ULIMWENGUNI KATIKA KUTENGENEZAJI MATREKA NA ZANA ZA KILIMO IKIWA NA SOKO KATIKA NCHI ZA ULAYA, MAREKANI, ASIA NA AFRIKA. MBALI YA MATREKTA INATENGENEZA MAGARI YA AINA MBALIMBALI PAMOJA NA PIKIPIKI.

KAMPUNI HIYO INAFANYA PIA INAFANYA TAFITI MBALIMBALI KATIKA KILIMO NA IMEKUWA MSTARI MBELE KATIKA KUBUNI NA KUENDELEZA TEKINOLOJIA RAHISI KWA WAKULIMA WA INDIA NA SASA IMEINGIA KATIKA MASOKO YA NJE.

DK. SHEIN AMBAYE AMBAYE YUKO NCHINI INDIA KWA ZIARA YA SIKU TISA ANAENDELEA NA ZIARA YAKE LEO KWA KUTEMBELEA KIWANDA CHA KUSINDIKA VIUNGO(SPICES) NA BAADAE ATAFANYA MAZUNGUMZO YA WAFANYABIASHARA WA VIUNGO HAPA MUMBAI.

KATIKA ZIARA HIYO DK. SHEIN AMEFUATANA NA MKE WAKE MAMA MWANAMWEMA, WAZIRI WA FEDHA OMAR YUSUF MZEE, WAZIRI WA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO BIBI ZAINAB OMAR MOHAMED, WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA NA MASOKO NASSOR AHMED MARZUI, NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DK. MAHADHI JUMA MAALIM NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA INJINIA JOHN KIJAZI.

WENGINE KATIKA MSAFARA HUO NI KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MOHAMED SALEH JIDAWI NA KATIBU MKUU KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM, MSHAURI WA RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UWEKEZAJI NA UCHUMI BALOZI MOHAMED RAMIA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA UWEKEZAJI ZANZIBAR –ZIPA SALUM KHAMIS NASSOR.

No comments:

Post a Comment