SERIKALI
YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA CHUO CHA BAREFOOT CHA INDIA ZIMEKUBALIANA KUANZISHA
CHUO CHA MAFUNZO YA AMALI KWA WANAWAKE WA ZANZIBAR WAISHIO VIJIJINI.
MAKUBALIANO HAYO
YAMEFIKIWA LEO WAKATI RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.
ALI MOHAMED SHEIN ALIPOTEMBELEA CHUO HICHO HUKO TILONIA, WILAYA YA AJMER KATIKA
JIMBO LA RAJASTAN AKIWA KATIKA SIKU YAKE YA PILI YA ZIARA YAKE YA SIKU TISA
NCHINI INDIA.
CHINI YA MAKUBALIANO
HAYO AMBAYO KWA UPANDE WA SERIKALI YA ZANZIBAR YALISAINIWA NA KATIBU MKUU
WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM NA MWANZILISHI WA CHUO CHA
BAREFOOT BWANA BUNCKER ROY CHUO HICHO KITATOA MAFUNZO HAYO KWA WANAWAKE WATU
WAZIMA ILI KUWAJENGEA UWEZO WAO KITAALUMA NA STADI ZA MAISHA ILI WAWEZE
KUPAMBANA NA UMASIKINI NA HATIMAE KUINUA KIWANGO CHAO CHA MAISHA.
CHUO HICHO KITATOA
MAFUNZO YA UFUNDI WA UMEME JUA PAMOJA NA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI IKIWEMO
UTENGENEZAJI WA BIDHAA KAMA CHAKI, MISHUMAA, VYANDARUA NA PEDI ZA WANAWAKE.
AKIZUNGUMZA MARA BAADA
YA KUSHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MAKUBALIANO HAYO, RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI
WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN ALISEMA KUTIWA SAINI MAKUBALIANO
HAYO NI HATUA NYINGINE MBELE KATIKA JITIHADA ZA SERIKALI ZA KUWAJENGEA UWEZO
WANAWAKE NA KUPAMBANA NA UMASKINI NCHINI.
AMESEMA KUJENGWA KWA
CHUO HICHO KUTATOA FURSA ZAIDI KWA JAMII ZA WATU WA VIJIJNII AMBAO BADO
HAWAJAPATA HUDUMA YA UMEME NCHINI KUPATA NISHATI HIYO KWA GHARAMA NAFUU NA KWA
WEPESI ZAIDI.
KWA UPANDE WAKE BIBI
MEAGAN FALLONE WA CHUO HICHO AMEELEZA KUWA CHUO HICHO KITAKACHOJENGWA ZANZIBAR
MBALI YA KUTOA MAFUNZO KWA WANAWAKE WA UNGUJA NA PEMBA KITATOA FURSA PIA KWA
WANAWAKE KUTOKA NCHI JIRANI KUJA KUJIFUNZA TAALUMA HIZO CHUO HAPO.
CHUO CHA BAREFOOT
AMBACHO KINATOA MAFUNZO MBALIMBALI YA KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE WATU WAZIMA
WAKIWEMO WAJANE KUTOKA MAENEO YA VIJIJINI KUTOKA NCHI ZINAZOENDELEA
KILIANZISHWA MWAKA 2004.
CHUO HICHO HUCHUKUA
WANAFUNZI KUTOKA NDANI NA NJE YA INDIA AMBAPO HIVI SASA KUNA WANAFUNZI KUTOKA
NJE 37 AMBAO WANATOKA ZANZIBAR, VISIWA VYA COMORO, TOGO, IVORY COAST, PANAMA,
INDONESIA, NEPAL, HONDURUS, BRAZIL, MEXICO NA BELIZE.
KWA UPANDE WA TANZANIA
TANGU KUANZISHWA KWAKE MWAKA 2004 HADI SASA JUMLA YA WANAWAKE 29 WAMEPATA
MAFUNZO YAO KATIKA CHUO HICHO AMBAPO KUTOKA TANZANIA BARA NI WANAWAKE 18 NA 11
KUTOKA ZANZIBAR AMBAO MIONGONI MWAO NI WANANWAKE WAWILI WALIOPO CHUO HAPO HIVI
SASA AMBAO WANATARAJIWA KUMALIZA MAFUNZO YAO MWEZI MACHI MWAKA HUU.
WANAWAKE WANAOPATA
MAFUNZO KATIKA CHUO HICHO HURUDI VIJIJINI KWAO AMBAKO HUSIMAMIA SHUGHULI ZA
KUSAMBAZA HUDUMA ZA UMEME JUA KUANZIA KUSAMBAZA, KUFANYA MATENGENZO PAMOJA NA
KUTENGENEZA BAADHI YA VIFAA VINAVYOTUMIKA KATIKA USAMBAZAJI HUO.
DK. SHEIN ATAMALIZA
ZIARA YAKE KATIKA JIMBO LA RAJASTAN LEO MCHANA KWA KUTEMBELEA MAENEO YA
HISTORIA YA HAWA MAHAL NA JUMBA LA MAKUMBUSHO LA ALBERT NA BAADAE JIONI
ATAONDOKA KWENDA NEW DELHI KUENDELEA NA ZIARA YAKE HAPO KESHO.
KATIKA ZIARA HIYO DK.
SHEIN AMEFUATANA NA MKE WAKE MAMA MWANAMWEMA, WAZIRI WA FEDHA OMAR YUSUF MZEE,
WAZIRI WA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO BIBI ZAINAB
OMAR MOHAMED, WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA NA MASOKO NASSOR AHMED MARZUI,
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DK. MAHADHI JUMA
MAALIM NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA INJINIA JOHN KIJAZI.
WENGINE KATIKA MSAFARA HUO NI KATIBU MKUU WIZARA YA
AFYA MOHAMED SALEH JIDAWI NA KATIBU MKUU KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN
MAALIM, MSHAURI WA RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UWEKEZAJI NA UCHUMI BALOZI
MOHAMED RAMIA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA UWEKEZAJI ZANZIBAR –ZIPA
SALUM KHAMIS
No comments:
Post a Comment