SERIKALI YA JAPAN IMESEMA ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR KATIKA
JITIHADA ZAKE ZA KUJIKWAMUA KIUCHUMI, KWA KUENDELEA KUCHANGIA MIRADI YA
MAENDELEO IKIWEMO YA MAJI SAFI NA SALAMA, MIJINI NA VIJIJINI.
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN BW. NORIO MITSUYA AMEELEZA HAYO
WAKATI AKIZUNGUNGUMZA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF
SHARIF HAMAD, OFISINI KWAKE MIGOMBANI.
AMESEMA JAPAN NA ZANZIBAR ZINA UHUSIANO WA KIUCHUMI WA MUDA MREFU, NA
KWAMBA UMEKUWA UKIIMARIKA SIKU HADI SIKU KUTOKANA NA NIA NJEMA YA NCHI HIZO.
BW. MITSUYA AKIONGOZA UJUMBE WA WATU SABA WA JAPAN, AMETAJA MAENEO MENGINE
WANAYOWEZA KUSHIRIKIANA NA ZANZIBAR KUWA NI PAMOJA NA SEKTA YA KILIMO, UVUVI,
UTALII PAMOJA NA KUWAJENGEA UWEZO VIJANA WASIOKUWA NA AJIRA.
AKIZUNGUMZIA KUHUSU SEKTA YA UTALII, AMESEMA WATALII KUTOKA JAPAN
WAMESHAJIIKA KUITEMBELEA TANZANIA AMBAPO IDADI YA WATALII WA NCHI HIYO
IMEONGEZEKA KUTOKA WATALII 4000 HADI 5000 KWA MSIMU ULIOPITA.
NAE MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD,
AMESEMA ZANZIBAR INATHAMINI MISAADA INAYOTOLEWA NA SERIKALI YA JAPAN, NA
KUWASHAJIISHA WAWEKEZAJI WA NCHI HIYO KUJA KUWEKEZA ZANZIBAR HASA KATIKA MIRADI
YA UJENZI WA HOTELI ZA KISASA.
AIDHA AMEIOMBA NCHI HIYO KUANGALIA UWEZEKANO WA KUCHANGIA UPATIKANAJI WA
UMEME WA UHAKIKA ZANZIBAR, ILI KUEPUKA KUTEGEMEA MOJA KWA MOJA NISHATI HIYO
KUTOKA TANZANIA BARA.
No comments:
Post a Comment