MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE.
MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEWAHIMIZA WAANDISHI WA HABARI KURIPOTI TAARIFA
ZINAZOGUSA MAENDELEO YA JAMII HASA KATIKA MAENEO YA VIJIJINI, ILI KUIWEZESHA
JAMII KUFAHAMU MAENDELEO NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WANANCHI WA VIJIJINI.
AMESEMA MARA NYINGI WAANDISHI WA HABARI
WAMEKUWA WAKIRIPOTI HABARI ZINAZOHUSU MAENDELEO YA MIJINI, NA KUSAHAU MCHANGO
UNAOTOLEWA NA WAKAAZI WA VIJIJINI, HALI INAYOPELEKEA MAENEO YA VIJIJINI KUACHWA
NYUMA KIMAENDELEO.
MHE. MAALIM SEIF AMETOA INDHARI HIYO WAKATI
AKIZUNGUMZA KWENYE MAHAFALI YA TANO YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA MAWASILIANO
YA UMMA, YALIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA WIZARA YA HABARI, MNAZI MMOJA.
AMESEMA MAENEO YA VIJIJINI YANA MIRADI MINGI
YA KIUCHUMI NA KIJAMII INAYOTEKELEZWA KWA NGUVU ZA WANANCHI, SERIKALI NA
WASHIRIKA WA MANDELEO, LAKINI MIRADI HIYO IMEKOSA KURIPOTIWA MAENDELEO YAKE NA
KUWAFANYA WATEKELEZAJI WAKE KURUDI NYUMA.
AMEFAHAMISHA KUWA VYOMBO VYA HABARI VINA
WAJIBU WA KUHAMASISHA MAENDELEO NA UMOJA KATIKA JAMII, NA KUVISHAJIISHA
KUELEKEZA NGUVU ZAO KATIKA MAENEO NA SEKTA ZOTE ZA MAENDELEO.
SAMBAMBA NA HILO MAALIM SEIF AMEWATAKA
WAANDISHI WA HABARI KUZIFANYIA UTAFITI HABARI WANAZOZIANDIKA, ILI KURIPOTI
TAARIFA SAHIHI NA KUEPUKA KUWAPOTOSHA WANANCHI.
AIDHA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AMEWASISITIZA
WAHITIMU HAO KUJIENDELEZA KATIKA TAALUMA MAHSUSI (SPECIALIZATION), ILI KUONGEZA
UPEO WA KURIPOTI KATIKA MAENEO HAYO.
AMEFAHAMISHA KUWA IWAPO WAANDISHI
WATAJIKITIKA KATIKA KURIPOTI KWENYE FANI TOFAUTI ZIKIWEMO AFYA, KILIMO,
MAZINGIRA, ELIMU NA UTALII, WATAKUWA NA UFANISI MKUBWA NA KUWEZA KUJIAMINI
ZAIDI KATIKA KAZI ZAO.
AMEWASISITIZA KUTUMIA KALAMU ZAO VIZURI KWA
KUSAIDIA JUHUDI ZA MAENDELEO, PAMOJA NA KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA VITENDO VYA
RUSHWA, UDHALILISHAJI WA KIJINSIA, UCHAFUZI WA MAZINGIRA NA MATUMIZI YA DAWA ZA
KULEVYA.
AMESEMA SERIKALI KWA UPANDE WAKE ITAENDELEA
KUKIJENGEA UWEZO CHUO HICHO CHA UANDISHI WA HABARI KWA KUKIPATIA BAJETI MUAFAKA
KADRI HALI YA FEDHA ITAKAVYORUHUSU, ILI KUKIJENGEA MAZINGIRA BORA ZAIDI YA
KUFUNDISHA TAALUMA HIYO.
KWA UPANDE WAKE, WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI,
UTALII NA MICHEZO MHE. SAID ALI MBAROUK, AMESEMA CHUO HICHO KINA UMUHIMU MKUBWA
KWA SEKTA YA HABARI NA MAENDELEO YA TAIFA KWA UJUMLA.
AMESEMA UFANISI UNAOONEKANA KWENYE VYOMBO VYA
HABARI BINAFSI, UNATOKANA NA MCHANGO WA CHUO HICHO KUTOA WAHITIMU BORA, AMBAO
HUAJIRIWA KUVITUMIKIA VYOMBO HIVYO PAMOJA NA VILE VYA SERIKALI.
AMEONGEZA KUWA KATIKA KUKIJENGEA UWEZO ZAIDI
CHUO HICHO, WIZARA YA HABARI IMEKUWA IKISHIRIKIANA KWA KARIBU NA BODI YA CHUO
HICHO, KATIKA KUTATUA BAADHI YA KERO ZINAZOKIKABILI, IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA
UTARATIBU WA KULIENDELEZA ENEO LA CHUO HICHO LILILOKO TUNGUU.
MWENYEKITI WA BODI YA CHUO HICHO ND. CHANDE
OMAR AMEIOMBA SERIKALI KUANGALIA UWEZEKANO WA KUANZISHA VITENGO VYA HABARI
KATIKA KILA IDARA YA SERIKALI, ILI KUSAIDIA UPATIKANAJI WA AJIRA KWA VIJANA
WANAOHITIMU TAALUMA YA HABARI.
MAPEMA AKISOMA RISALA YA WAHITIMU WA CHUO
HICHO, MWANAFUNZI MWAJUMA KHAMIS, AMEIOMBA WIZARA YA HABARI ISHIRIKIANE NA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI, KUWASAIDIA WANAFUNZI WA TAALUMA YA HABARI,
ILI NAO WANUFAIKE NA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR.
JUMLA YA WANAFUNZI 122 WAMEHITIMU MAFUNZO YA
CHETI NA STASHAHADA YA UANDISHI WA HABARI KATIKA CHUO HICHO, KATI YAO WAHITIMU
83 WAKIWA WANAWAKE.
No comments:
Post a Comment