ZANZIBAR
WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KUJADILI RASIMU YA
PILI YA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAMEOMBWA KUZIANGALIA KWA MAKINI
NAFASI ZA VIJANA KATIKA KULETA MCHANGO KWA MAENDELEO YA TAIFA.
AKIZUNGUMZA NA RADIO ADHANA FM MWENYEKITI WA
JUMUIYA YA ZANZIBAR YOUTH FORAM NGUGU DADI KOMBO MAALIM AMESMA KATIKA UTEUZI WA
WABUNGE WA BUNGE HILO WANAOHUSIKA NA UTEUZI HAWAKUANGALIA NAFASI YA VIJANA NA KUSAHAU
KUWA WANADHAMANA NA FUNGU KUBWA KATIKA KUISIMAMIA KATIBA HIYO.
AMSEMA KUWA KWA MUJIBU WA SENSA YA WATU NA
MAKAZI YA MWAKA ELFU MBILI NA KUMI IDADI YA VIJANA NI KUBWA ZAIDI YA ASILIMIA
52.4 KATIKA UTEUZI HUO VIJANA WALIPASWA KUPEWA KIPAOMBELE KUPITIA TAASISI ZAO LAKINI CHA KUSIKITISHA
HAWAKUCHAGULIWA KATIKA NAFASI ZA KUPITIA
MAKUNDI MAALUM.
AMEWEKA WAZI YA KUWA KUTOKANA NA HALI HIYO
ENDAPO VIJANA WATAONA MASLAHI YAO HAYAKUZINGATIWA KATIKA UPATIKANAJI WA KATIBA
MPYA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUNAWEZA KUZUKA MGOGORO MKUBWA NA HATA KUPELEKEA KUFELISHA ZOEZI ZIMA LA
UPATIKANAJI WA KATIBA HIYO KWA KUKATAA KWENYE HATUA YA UPIGAJI WA KURA KWA
KUTUMIA WINGI WAO.
No comments:
Post a Comment