DAR ES SALAAM
KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD,
AMEWAKUMBUSHA VIONGOZI WA MAJIMBO KUTEKELEZA AHADI WANAZOZITOA KWA WANANCHI,
ILI KUJIJENGEA UAMINIFU KATIKA MAENEO YAO.
MAALIM SEIF AMETOA KAULI HIYO KATIKA OFISI KUU YA CUF BUGURUNI, BAADA YA
KUPOKEA PIKIPIKI MBILI KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO LA CHAMBANI MHE. YUSSUF SALIM
HUSSEIN (CUF), KWA AJILI YA WILAYA ZA KISARAWE NA BAGAMOYO.
AMESEMA KUKABIDHIWA KWA PIKIPIKI HIZO ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI
TATU NA LAKI MBILI, KUNAONESHA JINSI MBUNGE HUYO ANAVYOFUATILIA NA KUTEKELEZA
AHADI ZAKE KWA WANANCHI, NA KUTAKA VIONGOZI WENGINE WAIGE MFANO WA MBUNGE HUYO.
MBUNGE HUYO WA CHAMBANI AMEKABIDHI PIKIPIKI HIZO KUFUATIA AHADI ALIYOITOA
KWA WANANCHI WA WILAYA ZA KISARAWE NA BAGAMOYO, AKIWA KATIKA ZIARA YA KATIBU
MKUU WA CHAMA HICHO MWEZI ULIOPITA.
AKIZUNGUMZA BAADA YA KUKABIDHI PIKIPIKI HIZO MHE. YUSSUF AMESEMA AMEAMUA
KUTEKELEZA AHADI HIYO KWA MUDA MFUPI, ILI KUJENGA MATUMAINI YA WANACHAMA KWA
VIONGOZI NA CHAMA CHAO.
AMESEMA ATAENDELEA KUTEKELEZA AHADI ALIZOZITOA KWA WANANCHI KATIKA MAENEO
MBALI MBALI, ILI KUHAKIKISHA KUWA CHAMA HICHO KINAZIDISHA MATUMAINI KWA
WANACHAMA WAKE NA WANANCHI KWA UJUMLA.
No comments:
Post a Comment