ZANZIBAR
MAKAMU
WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR ALHAJ MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEWANASIHI
WAZAZI NA WALEZI KUTUMIA HEKIMA NA BUSARA KATIKA MALEZI YA WATOTO, ILI
KUWAJENGA KATIKA MAADILI MEMA YA DINI YA KIISLAM.
AMESEMA WAZAZI NA WALEZI WANA NAFASI KUBWA YA KUREJESHA MAADILI BORA
KATIKA JAMII IWAPO WATAREJESHA UTAMADUNI WA MALEZI YA PAMOJA, KUPENDANA
NA KUACHA KUFARAKANA KWA MAMBO YASIYOKUWA YA MSINGI.
ALHAJ
MAALIM SEIF AMETOA NASAHA HIZO WAKATI AKIZUNGUMZA KATIKA MAULID YA KUSHAREHEKEA
KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (SAW), YALIYOANDALIWA NA MADRAST IMAN ISLAMIYA YA
JANG'OMBE MJINI ZANZIBAR.
AMEIPONGEZA MADRASA HIYO KWA MAFANIKIO MAKUBWA ILIYOPATA, IKIWA NI PAMOJA
NA KUONGEZA IDADI YA WANAFUNZI KUTOKA 12 MWAKA 1995 HADI 192 MWAKA HUU.
AMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA MADRASA HIYO KATIKA KUTAFUTA NAMNA YA KUZITATUA
KERO ZINAZOWAKABILI ZIKIWEMO UPUNGUFU WA VYUMBA VYA KUSOMEA.
KATIKA RISALA YA MADRASA HIYO ILIYOSOMWA NA MWALIMU HASSAN HASSAN
(HASANAYNI) WAMESEMA WANAKUSUDIA KUIJENGA UPYA MADRASA YAO YA ZAMANI, ILI KUTOA
NAFASI KWA WANAFUNZI ZAIDI KUPATA VYUMBA VYA KUSOMEA, NA KUWAOMBA WAFADHILI
KUJITOKEZA KUCHANGIA UJENZI HUO.
No comments:
Post a Comment