tangazo

tangazo

Saturday, February 8, 2014

WIZARA ZA KATIBA NA SHERIA ZATAKIWA KUSHIRIKIANA


MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, AMEZITAKA WIZARA ZA KATIBA NA SHERIA TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA ILI KUFANIKISHA SEHEMU ILIYOBAKIA YA MCHAKATO WA KATIBA.

AMESEMA TOKEA ZOEZI HILO LILIPOANZA, WIZARA YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMEKUWA IKISHIRIKIANA KWA KARIBU NA WIZARA YA KATIBA YA ZANZIBAR, HALI ILIYOLETA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA MCHAKATO HUO, HADI KUPATIKANA KWA RASIMU YA PILI AMBAYO ITAANZA KUJADILIWA KWENYE BUNGE LA KATIBA HIVI KARIBUNI.

MHE. MAALIM SEIF AMETOA MAELEZO HAYO NYUMBANI KWAKE MBWENI, WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. ASHA ROSE MIGIRO.

“HAPA TULIPOFIKA NI KUTOKANA NA MASHIRIKIANO MAZURI YA WIZARA ZETU ZA KATIBA, HIVYO NI VYEMA MASHIRIKIANO NA MASHAURIANO YAKAENDELEA ILI KUMALIZA NGWE ILIYOBAKIA KWA SALAMA NA AMANI, NA HATIMAYE KUPATA KATIBA MPYA ITAKAYORIDHIWA NA WATANZANIA”, ALITANABAHISHA MAALIM SEIF.

HATA HIVYO AMEMSHAURI WAZIRI MIGIRO KUKAA PAMOJA NA WAZIRI MWENZAKE WA ZANZIBAR MHE. ABUBAKAR KHAMIS BAKARI, KUANDAA MAZINGIRA YA KUFIKIA MAKUBALIANO KWENYE BUNGE LA KATIBA, IWAPO ZITATOKEA KASORO KWENYE MIJADALA YA BUNGE HIYO.

AIDHA AMEWASHAURI MAWAZIRI HAO WA KATIBA KUANDAA MAPENDEKEZO YA KANUNI ZA BUNGE LA KATIBA, ILI WAJUMBE WAWEZE KUYAPITIA NA KUYAREKEBISHA, BADALA YA KUSUBIRI BUNGE LENYEWE KUANDAA KANUNI, HATUA AMBAYO INAWEZA KUCHUKUA MUDA MWINGI WA VIKAO VYA BUNGE.

AMEMPONGEZA WAZIRI MIGIRO KWA KUTEULIWA KUSHIKA WADHIFA HUO, NA KUELEZEA MATUMAINI YAKE JUU YA UTENDAJI BORA WA KAZI ZAKE.

NAE MHE. ASHA ROSE MIGIRO AMBAYE ALIFIKA KWA AJILI YA KUJITAMBULISHA, AMEMUHAKIKISHIA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS KUWA MASHIRIKIANO YALIYOKUWEPO BAINA YA WIZARA HIZO YATAENDELEZWA KWA KARIBU ZAIDI, ILI KUWAWEZESHA WATANZANIA KUPATA KATIBA WANAYOITAKA.

AMESEMA NCHI IKO KATIKA HIPINDI MUHIMU CHA KUKAMILISHA MCHAKATO WA KATIBA, HIVYO UMAKINI ZAIDI UNAHITAHITAJIKA KATIKA KUFANIKISHA HATUA HIYO.

AMEAHIDI KUUFANYIA KAZI USHAURI ALIOPEWA, ILI KUHAKIKISHA KUWA MALENGO YA WATANZANIA YA KUPATA KATIBA MPYA YANAFIKIWA KWA MUDA ULIOPANGWA.

No comments:

Post a Comment