RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA
MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN LEO AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE
WA KAMPUNI YA KUTENGENEZA MATRETA YA MAHINDRA KUTOKA NCHINI INDIA.
ZIARA HIYO YA SIKU MBILI HUMU NCHINI INAFUATIA
MWALIKO WA MHESHIMIWA RAIS KWA UONGOZI WA KAMPUNI HIYO WAKATI WA ZIARA YAKE
NCHINI INDIAALIYOIFANYA HIVI KARIBUNI.
WAKATI WA ZIARA HIYO DK. SHEIN ALITEMBELEA
KIWANDA HICHO NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA JUU WA KAMPUNI HIYO AMBAPO
KAMPUNI HIYO ILIKUBALI OMBI LA KUISAIDIA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR
KUENDELEZA KILIMO.
KATIKA MAZUNGUMZO HAYO UONGOZI WA KAMPUNI HIYO
ULIAHIDI KUTUMA TUMI YA WATAALAMU NCHINI KUANGALIA NAMNA BORA KAMPUNI HIYO
INAWEZA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUENDELEZA KILIMO.
KATIKA MAZUNGUMZO YAKE NA UJUMBE HUO
YALIYOFANYIKA IKULU, RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI
ALIUSHUKURU UONGOZI WA KAMPUNI YA MAHINDRA KWA KUITIKIA KWA HARAKA WITO WAKE
KUTEMBELEA ZANZIBAR KUJUA MAHITAJI YA NCHI KATIKA SEKTA HIYO.
“NI SIKU 14 TU TANGU TULIPOONANA TAREHE 7
FEBRUARI, 2014 MJINI MUMBAI WAKATI WA ZIARA YANGU. KWA KASI HII NINA MATARAJIO
MAKUBWA KUWA TUTAWEZA KUFANYA MABADILIKO YA HARAKA KWA WAKULIMA WETU” DK SHEIN
ALIUELEZA UJUMBE HUO.
ALIFAFANUA KUWA MWITIKIO HUO WA HARAKA
UNADHIHIRISHA PIA UTAYARI WA KAMPUNI YA MAHINDRA YA KUFANYAKAZI NA SERIKALI YA
MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA KWAMBA KWA UPANDE WAKE ZANZIBAR IMEJIANDAA KUONA NI
KWA NAMNA GANI INAWEZA KUJENGA USHIRIKIANO WA MUDA MREFU NA KAMPUNI HIYO
KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO NCHINI.
DK. SHEIN ALIUELEZA UJUMBE HUO KUWA ZIARA YAO
ITAONA JINSI KILIMO KILIVYOKUWA NA UMUHIMU KATIKA UCHUMI WA ZANZIBAR NA MCHANGO
WAKE KATIKA KUINUA KIWANGO CHA MAISHA CHA WANANCHI WA ZANZIBAR.
“TUNATARAJIA MATOKEO YA ZIARA YENU YATAFUNGUA
NJIA YA USHIRIKIANO WA MUDA MREFU KATI YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA
KAMPUNI YA MAHINDRA KWA KUSAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO” ALISEMA DK. SHEIN.
KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI HIYO
BWANA SANJAY JADHAR ALIELEZA KUWA ZIARA YAO HIYO NI MWITIKIO WA WITO WA MHE
RAIS ALIUTOA KWA KAMPUNI YAO WAKATI ALIPOITEMBELEA HIVI KARIBUNI.KWA HIVYO
WAMEKUJA NCHINI KUANGALIA NAMNA KAMPUNI YAKE INAVYOWEZA KUSAIDIA KUIMARISHA
KILIMO NCHINI NA KUBADILI HALI YA WAKULIMA WA ZANZIBAR.
ALIFAFANUA KUWA UJUMBE HUO WAKIWA NA WENYEJI WAO
UONGOZI WA WIZARA YA KILIMO UTAMBELEA SEHEMU MBALIMBALI UNGUJA NA PEMBA
YAKIWEMO MASHAMBA, KARAKANA YA MATREKTA PAMOJA NA KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO.
ALIONGEZA KUWA BAADA YA ZIARA HIYO WATAKUWA NA
MAZUNGUMZO YA PAMOJA NA WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI KUHUSU WALICHOKIONA
WAKATI WA ZIARA NA KUPANGA NINI LA KUFANYA KUTIMIZA MALENGO YA ZIARA.
UJUMBE WA MAHINDRA ULISHIRIKISHA PIA BWANA
SANDESH PARAB MAKAMU WA MKURUGENZI MKUU WA SHUGHULI ZA KIMATAIFA ZA KAMAPUNI
HIYO, BWANA G.V. RAO MENEJA WA KANDA AGRO TRACTORS AND IMPLEMENTS NA BWANA
MIHID TEREDESAI MENEJA MKUU AGRO TRACTORS AND IMPLEMENTS OFISI YA DAR ES
SALAAM.
MIONGONI MWA WALIOHUDHURIA MAZUNGUMZO HAYO NI
PAMOJA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.
MWINYIHAJI MAKAME, KATIBU MKUU KIONGOZI DK. ABDULHAMID YAHYA MZEE, MSHAURI WA
RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UCHUMI NA UWEKEZAJI BALOZI MOHAMED RAMIA NA
KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM.
No comments:
Post a Comment