MKOA WA KASKAZINI UNGUJA
JUMLA
YA KESI THELATHINI NA SITA ZA UBAKAJI ZIMERIPOTIWA KUTOKEA KATIKA MKOA WA
KASKAZINI UNGUJA KATIKA KIPINDI CHA MWAKA JANA.
AKIZUNGUMZA
NA ADHANA FM REDIO KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI HASSAN MSANGI AMESEMA BADO
TATIZO HILO LIMEKUWA LIKIENDELEA KUTOKANA NA MWAMKO MDOGO WA WANANCHI WA
KURIPOTI TATIZO HILO.
AIDHA
AMEFAHAMISHA KUWA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALI MBALI
WAMEKUWA WAKIENDELEA KUIELIMISHA JAMII JUU YA UMUHIMU WA KURIPOTI MATENDO YA
UDHALILISHAJI WA KIJINSIA.
SAMBAMBA
NA HAYO AMEWATAKA WANANCHI WAWE TAYARI KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUTOA USHAHIDI
PINDI WANAPOTAKIWA KUFANYA HIVYO ILI WAWEZE KUTOKOMEZA TATIZO HILO KATIKA MKOA
HUO.
No comments:
Post a Comment