TANZANIA NA INDIA ZIMEELEZA KURIDHISHWA NA
UHUSIANO NA USHIRIKIANO ULIOPO BAINA YAO NA KUSISITIZA DHAMIRA YA KWELI YA
KUONA KUWA USHIRIKIANO HUO UNAZIDI KUIMARIKA KWA MANUFAA YA SERIKALI NA
WANANCHI WA NCHI HIZO.
HAYO YAMEJITOKEZA JANA WAKATI WA MAZUNGUMZO KATI
YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK. ALI MOHAMED SHEIN
NA MAKAMU WA RAIS WA INDIA MOHAMED HAMID ANSARI.
KATIKA MAZUNGUMZO HAYO VIONGOZI HAO WAMESEMA
KUWA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA KATI YA NCHI HIZO ULIOANZISHWA MWANZONI MWA MIAKA
YA SITINI UMEKUWA UKIIMARIKA MWAKA HADI MWAKA KWA KUONGEZA MAENEO YA
USHIRIKIANO KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA UCHUMI NA KIJAMII.
WAMEELEZA KUWA ZIARA ZA VIONGOZI WA NCHI HIZO
PAMOJA NA ZIARA ZA MARA KWA MARA KATIKA NGAZI YA MAWAZIRI NI UTHIBITISHO WA
UHUSIANO HUO MZURI KATI YA NCHI HIZO.
KATIKA MAZUNGUMZO HAYO DK. SHEIN AMEUPONGEZA
USHIRIKIANO ULIOPO KATI YA ZANZIBAR NA INDIA NA AMEISHUKURU SERIKALI NA
WANANCHI WA INDIA KWA MISAADA MBALIMBALI AMBAYO IMEKUWA IKIITOA KWA SERIKALI YA
MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA WANANCHI WAKE.
DK. SHEIN ALIMUELEZA MAKAMU WA RAIS WA INDIA
KUWA ZIARA YAKE NCHINI HUMU IMELENGA KUIMARISHA UHUSIANO HUO WA KIDIPLOMASIA
ULIASISIWA MIAKA YA SITINI CHINI YA MISINGI IMARA YA URAFIKI ILIYOWEKWA NA WAASISI
WAKE VIONGOZI WA KWANZA WA NCHI MBILI HIZO.
HALIKADHALIKA ALIMUELEZA KUWA ZIARA HIYO
AMEDHAMIRIA KUKUKUZA USHIRIKIANO KATI YA ZANZIBAR NA INDIA KATIKA MAENEO YA
ELIMU, MAFUNZO, BIASHARA, KILIMO PAMOJA NA KUHIMIZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA
MBALIMBALI ZA UCHUMI.
ALIFAANUA KUWA UHUSIANO NA USHIRIKIANO KATI YA
WATU WA ZANZIBAR NA WATU WA INDIA NI WA KIHISTORIA ULIODUMU KWA KARNE NYINGI
HIVYO KUUFANYA KUWA WA KIDUGU.
AMEMUELEZA BWANA ANSARI KUWA SERIKALI YA
MAPINDUZI ZANZIBAR IMEFURAHISHWA NA MSAADA WA UJENZI WA CHUO CHA MAFUNZO YA
AMALI KITAKACHOJENGWA HUKO PEMBA PAMOJA NA MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA JANA YA
KUANZISHA CHUO KAMA HICHO HUKO UNGUJA KUPITIA CHUO CHA BAREFOOT CHA TILONIA,
JAIPUR.
AMEBAINISHA KUWA KATIKA MIAKA YA HIVI KARIBUNI
KUMEKUWEPO NA WANANCHI WENGI WA ZANZIBAR WANAKWENDA INDIA KWA SABABU ZA
KIMATIBABU HIVYO AMETAKA KUWEPO NA USHIRIKIANO ZAIDI WA NAMNA BORA YA KULETA
WAGONJWA HAO NCHINI HUMU.
KWA UPANDE MWINGINE DK. SHEIN AMEIOMBA SERIKALI
YA INDIA KUANGALIA NAMNA INAVYOWEZA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA ZANZIBAR
KUISAIDIA UPATIKANAJI WA MADAWA KWA ZANZIBAR.
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA
MAPINDUZI AMETUMIA FURSA KUMUELEZA MAKAMU WA RAIS WA INDIA HAJA YA KUONGEZA
FURSA ZAIDI ZA MASOMO YA MUDA MFUPI NA MUDA WA KATI KWA WANANCHI WA ZANZIBAR
ILI KUJENGA UWEZO KATIKA TAALUMA MBALIMBALI ILI KUHARAKISHA MAENDELEO.
KWA UPANDE WAKE MAKAMU WA RAIS WA INDIA BWANA
MOHAMED HAMID ANSARI AMEMHAKIKISHIA DK. SHEIN KUWA SERIKALI YA NCHI YAKE
ITAENDELEA KUSAIDIA JITIHADA ZINAZOFANYWA NA SERIKALI NA WANANCHI WA ZANZIBAR
ZA KUJILETEA MAENDELEO.
BWANA ANSAR AMESEMA UHUSIANO WA KIHISTORIA WA
WANANCHI WA INDIA NA ZANZIBAR ULIOANZA KARNE NYINGI TANGU ENZI ZA KUTEGEMEA
PEPO ZA KUSI NA KASKAZI UMEKUWA IMARA NA KILA SIKU WANANCHI WAKE WAMEONYESHA
ARI YA KUZIDI KUUIMARISHA.
MAPEMA ASUBUHI
ALITEMBELEA MAKUMBUSHO YA MAHATMA GHANDI ILIYOPO MJINI NEW DELHI AMBAPO ALIWEKA
SHADA LA MAUA PAMOJA NA KUSAINI KITABU CHA KUMBUKUMBU.
BAADAE MCHANA ANATARAJIWA KUKUTANA NA
WATANZANIA ANAOISHI MJINI HAPA KATIKA UKUMBI WA URAFIKI KWENYE HOTELI YA ASHOK
NA ATAKUTANA PIA NA WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA FAMILIA WA INDIA. JIONI
ATAHUDHURIA CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA KWA HESHMA YAKE NA MWENYEJI WAKE
MAKAMU WA RAIS WA INDIA.
HAPO JANA KABLA YA KUONDOKA JAIPUR, JIMBO LA
RAJASTAN, KUJA NEW DELHI DK. SHEIN ALITEMBELEA MAKUMBUSHO YA HAWA MAHAL NA
ALBERT YALIYOPO MJINI HUMO.
MIONGONI MWA WALIOFUATANA NA RAIS KATIKA ZIARA
HIYO NI PAMOJA NA MKE WAKE MAMA MWANAMWEMA, WAZIRI WA FEDHA OMAR YUSUF MZEE,
WAZIRI WA UWEZESHAJI, USTAWI WA JAMII, VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO BIBI ZAINAB
OMAR MOHAMED, WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA NA MASOKO NASSOR AHMED MARZUI,
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA DK. MAHADHI JUMA
MAALIM NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA INJINIA JOHN KIJAZI.
WENGINE NI KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MOHAMED
SALEH JIDAWI, KATIBU MKUU KILIMO NA MALIASILI AFFAN OTHMAN MAALIM, MSHAURI WA
RAIS USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, UWEKEZAJI NA UCHUMI BALOZI MOHAMED RAMIA NA
MKURUGENZI MTENDAJI WA MAMLAKA YA UWEKEZAJI ZANZIBAR –ZIPA SALUM KHAMIS NASSOR.
No comments:
Post a Comment