DAR-ES-SALAAM.
SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IMEIAGIZATUME YA HAKI ZA
BINADAMU NA UTAWALA BORA KUIBUA MASUALA YANAYOATHIRI UZINGATIAJI WA HAKI ZA
BINADAMU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE NA HIVYO KUIMARISHA MISINGI YA HAKI NA
UTAWALA BORA NCHINI.
AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA TUME HIYO MJINI DAR ES SALAAM, WAZIRI WA
KATIBA NA SHERIA DKT. ASHA–ROSE MIGIRO AMESEMA KUWA SERIKALI INA WAJIBU WA
KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAKE.
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA ILIANZISHWA MWAKA 2000 NA KUANZA
KAZI RASMI MWAKA 2002 ILI, KUTOA USHAURI KWA SERIKALI NA VYOMBO VINGINE VYA
UMMA NA VYA SEKTA BINAFSI KUHUSU HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA.
AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO, NAIBU WAZIRI WA WIZARAHIYO UMMY MWALIMU
AMESEMA KUWA NI MUHIMU KWA TUME HIYO KUONGEZA KASI YA KUTOA ELIMU KWA UMMA
KUHUSU UZINGATIAJI WA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWA KUTUMIA TEKNOLOJIA
YA KHABARI NA MAWASILIANO ILI KUWAFIKIA WANANCHI WENGI KWA KASI NA HARAKA.
No comments:
Post a Comment