zanzibar.
viongozi wa ofisi za wilaya za unguja wamekipongeza
kitengo cha maleria zanzibar kwa kufanya tathmini mara baada ya zoezi la
upigaji dawa kukamilika.
pongezi hizo zimetolewa na wa wakuu wa wilaya mbali
mbali katika ziara maalumu ya zoezi la
upigaji dawa iliyokuwa na lengo lakufanya tathmini ya matokeo ya zoezi hilo
lililomalizika hivi karibuni kwa wilaya za unguja na pemba.
akizungumza na adhana fm mara baada ya ziara hizondugu
khamis ameir kutoka kitengo cha maleria zanzibar amesema kuwa walikusudia kupiga dawa nyumba 14554 sawa na asilimia
93.6 na nyumba 999 hazikupigwa dawa kutokana na sababu mbali mbali.
amefahamisha kuwa katika zoezi hilo lililopita wilaya
zilizopigwa dawa kisiwani pemba ni pamoja na wilaya ya mkoani na micheweni
ambapo kanda hiyo ilipata asilimia 97.
No comments:
Post a Comment