tangazo

tangazo

Sunday, December 29, 2013


WASOMI NCHINI WAMETAKIWA KUUTATHMINI NA KUUCHAMBUA MFUMO WA ELIMU PAMOJA NA SERA YA ELIMU YA MWAKA 2006, ILI KUONA IWAPO INAKIDHI MATARAJIO YA SEKTA YA ELIMU ZANZIBAR.

 

WITO HUO  UMETOLEWA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD, WAKATI AKIFUNGUA KONGAMANO LA ELIMU KUHUSU MFUMO WA ELIMU ZANZIBAR KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA MAPINDUZI.

 

KATIKA KONGAMANO HILO LILILOANDALIWA NA CHUO CHA UONGOZI WA FEDHA CHWAKA, MHE. MAALIM SEIFAMESEMA LICHA NA MAFANIKIO YA KUPIGIWA MFANO KATIKA SEKTA YA ELIMU, BADO YAPO MATATIZO YANAYOHITAJI KUFANYIWA TATHMINI KWA LENGO LA KUYATAFUTIA UFUMBUZI.

 

AMETAJA BAADHI YA MATATIZO HAYO KUWA NI PAMOJA NA UPUNGUFU WA VIFAA VYA KUFUNDISHIA, UKOSEFU WA WALIMU WENYE SIFA, PAMOJA NA UPUNGUFU WA VITABU VYA KUSOMEA.

 

SAMBAMBA NA HILO, MAALIM SEIF AMESEMA MFUMO WA ELIMU ULIOPO SASA UNAHITAJI KUFANYIWA MAPITIO, ILI KUWAWEZESHA VIJANA KUJIAJIRI NA KUAJIRIA WAPOMALIZA MASOMO.

AMEWASISITIZA WASOMI HAO KUENDELEA KUFANYA TAFITI NA KUTOA MATOKEO YAKE AMBAYO YATASAIDIA KUTATUA MATATIZO YANAYOIKABILI SEKTA YA ELIMU.

 

KAIMU MKUU WA CHUO HICHO IDDI HAJI MAKAME AMESEMA TAYARI CHUO HICHO KIMEANZA KUTOA SHAHADA ZA AINA NNE IKIWEMO YA USIMAMIZI WA FEDHA.

 

SHAHADA NYENGINE WANAZOTOA NI ICT NA UHASIBU, MANUNUZI NA USAMBAZAJI, PAMOJA NA HUDUMA ZA BENKI.

 

AMESEMA KATIKA KUHAKIKISHA MAENDELEO YA CHUO HICHO WAMEAMUA KUWAFUNDISHA WALIMU WAO KATIKA NGAZI YA UDAKTARI “PHD”, ILI WAWEZE KUTIMIZA LENGO LAO LA KUANZISHA SHAHADA WA UZAMILI KATIKA KIPINDI KIFUPI KIJACHO.

No comments:

Post a Comment