Aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,
Shamsi Vuai Nahodha amesema KUWA licha ya kuvuliwa uwaziri ataendelea kuwa
kiongozi wa kisiasa na kukitumikia chama chake na wananchi bila ya kuvunjika
moyo.
Nahodha, ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa NA MWAKILISHI WA
JIMBO LA MWANAKWEREKWE ametoa kauli hiyo
siku chache baada ya kuondolewa kATIKA Baraza la Mawaziri na Rais Jakaya
Kikwete kutokana na matatizo yaliyotokea katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza
Ujangili.
Akihutubia wanachama wa CCM waliomlaki na kumsikiliza
kATIKA Ofisi ya chama hicho Mkoa wa
Mjini Magharibi, Nahodha aMEsema yaliyomtokea ni mambo ya kawaida katika medani
za utumishi wa umma.
AMEBAINISHA KUWA amewajibika serikalini kutokana na
matakwa ya wajibu katika utendaji wa pamoja na kusema kitendo hicho ni mfano wa
ajali inayoweza kumkuta mtu yeyote katika safari ya maisha.
AMEsema KUWA
alikabidhiwa dhamana na viongozi wake ili kulitumikia taifa na kutimiza wajibu
ipasavyo katika nyadhifa mbalimbali na yaliyomtokea ameyapokea kwa mikono
miwili na hana kinyongo.
Kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Nahodha
aMEsema KUWA angependa ubaki katika
mfumo na Serikali mbili na kusema pamoja na uzuri wake, zipo changamoto na
kasoro zinazohitaji kurekebishwa na kuwa na muungano wenye nguvu za kiuchumi.
No comments:
Post a Comment